Mzee Msemakweli
Senior Member
- Oct 12, 2010
- 159
- 34
Serikali yawaangukia Waislamu
Walimu 108 waenguliwa kwenye semina ya Sensa Dar
na Waandishi wetu
Tanzania Daima
WAKATI shinikizo la baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutaka kususia sensa likishika kasi, serikali imewaomba radhi Waislamu kutokana na matangazo yaliyorushwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), yaliyoonesha kwamba idadi ya Wakristo nchini ni kubwa kuliko Waislamu.
TBC ilirusha matangazo hayo siku ya Sikukuu ya Muungano (Aprili 26) mwaka huu na kuonesha idadi ya Wakristo ni asilimia 52, Waislamu asilimia 32 na madhehebu mengine asilimia 14.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana alisema kuwa matangazo hayo yalitolewa kwenye mtandao wa Wikipedia na kurushwa hewani kimakosa.
Alisema baada ya kurushwa kwa matangazo hayo kimakosa, TBC walipokea barua nyingi kutoka Chama cha Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (Tanzania Muslim Professional Association) zikieleza kukerwa na taarifa hiyo.
Mshana Alisema katika barua hiyo, chama hicho kilitaka ufafanuzi jinsi takwimu hizo zilivyopatikana na TBC iwaombe radhi Watanzania.
Alisema Mei 15, TBC ilimwandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho cha Waislamu, Pazi Mwinyimvua na kuomba radhi kwa kasoro iliyotokea na kueleza kwamba shirika lake limemwonya mfanyakazi aliyerusha hewani takwimu hizo kimakosa.
Nichukue fursa hii tena kuwaomba radhi ndugu zetu wa dini ya Kiislamu kutokana na maumivu waliyopata kutokana na takwimu hizo. Na kwa kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na moja ya mahitaji wakati wa mfungo ni kusameheana, naomba waumini wote wa dini ya Kiislamu wapokee kwa moyo wa upendo ombi hili la kuwataka radhi, alisema Mshana.
Aliongeza kwamba kwa kuwa suala hili limehusishwa na sensa ya watu na makazi, anawaomba waumini wa dini ya Kiislamu kusamehe kilichotokea na washiriki katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Wakati serikali ikiendelea kuhimiza wananchi kushiriki sensa, kuna kundi la Waislamu limejitokeza kupinga tukio hilo.
Kundi hilo limekuwa likipita sehemu mbalimbali nchini kueneza sumu ya kuwataka Waislamu wasishiriki sensa kwa madai kuwa serikali imelenga kuwabagua kwa kutangaza takwimu zinazoonesha Wakristo ni wengi zaidi ya Waislamu.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Issa Sadick, hivi karibuni alizitaja baadhi ya sababu za kukataa kuhesabiwa kuwa ni serikali kuendelea kuwabagua Waislamu katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hata hivyo Sheikh Mkuu Mufti Shabaan bin Simba hivi karibuni aliwataka Waislamu kushiriki sensa na walipuuze kundi la masheikh linalozunguka nchini kutaka wasusie.
Wakati huo huo, walimu 108 walioteuliwa kuhudhuria semina ya makarani wa sensa, wameenguliwa na nafasi zao kuzibwa na watu wengine.
Utafiti wa gazeti hili umebaini kuwa, walioenguliwa ni walimu wa Kituo cha Mafunzo cha Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa habari hizo, walimu hao wameenguliwa kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa majaribio.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya walimu hao walisema wanapinga kuondolewa kwao kwani walikwishakubaliana katika mkataba wa malipo, na tayari walishaanza mafunzo kwa ajili ya kazi ya ukarani wa sensa.
Walisema kuwa wahusika wamekuwa wakiwaleta ndugu zao na kuwapunguza walimu ambao tayari walishaanza mafunzo kwa siku nne sasa.
Walimu hao walisema wanaitaka serikali iwalipe fedha zao za siku nne ambazo tangu waanze mafunzo hayo hawajalipwa.
Taarifa hii imeandaliwa na Zawadi Chogogwe, Agness Newa na Stella Mushi.
Mimi binafsi sioni SABABU ya kuwaomba radhi hawa ndugu zetu Waislam. Wanachotaka wao wambiwe Tanzania kuna Waislam wengi kuliko Wakristo na sijui itawasaidia nini katika Uislam wao. Kitendo tu cha kusema Wakristo ni 52% na Waislam ni 32% na DINI zingine ni 14% kwao inawasumbua sana. Kwamtazamo wao kipengere cha DINI kikiwekwa kwenye dodosa la sensa; haitamaliza matatizo yao. Lazima watakuja na lingine.
Kuondoa ubishi wakijinga basi tuseme hivi NCHI YA TANZANIA INA WAISLAM 100% WAKRISTO 0% na DINI ni 0%. Hapo sasa mmeridhika? Au bado mnalialia tena? Acheni jamani wakubwa nyinyi.