Japo Godbless Lema ametangaza nia ya kurudi nyumbani, na kwamba yuko tayari kwa lolote, naamini Mbowe atamtaka asirudi nyumbani

Maisha yako yakiwa magumu usifikirie na wengine wote wana maisha kama yako.
Maisha ya kuishi ukimbizini hayajawahi mpa mtu raha ya rohoni,acha kujifariji.
Lema hakuwa na sifa za ukimbizi na hivyo kwa kiasi kikubwa anaishi kwa kutegemea mfuko wake binafsi.
Lema pia hana kiwango chochote cha elimu kuweza kumruhusu kufanya kazi nchini Canada.
Hii imebuma yeye arudi asote mtaani kama kina Heche na wenzake kina Msigwa na kampuni yote.

CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO.
 
Kina Lema walitaka kuanzisha vuguvugu fulani la kuichafua serikali ya Jiwe baada ya uchaguzi. Alianza Lissu, akaja Lema, akataka kuunga na Nyalandu bahati akadhibitiwa.

Pengine angefuatia msigwa, sugu, heche na wengine. Baada ya kuona serikali imewashtukia mpango wao ikabidi watulie tu lakini hata sasa hakuna hata mmoja aliyetishiwa kuuawa au kuuliwa kama lema alivyosema baada ya kuondoka.

Siasa za bongo huwa tamu ukiwa uwanjani yaani bongo. Ukishakuwa mbali hata ukitoa maoni watu wanakupuuza sababu wanaamini kama ungekuwa unamaanisha basi ungekuwepo ama nchini au kwenye battle field.

Lema amenusa hiyo kitu na amegundua fimbo ya mbali haiui nyoka. Jana kaona kina sugu na kina msigwa wapo mahakamani. Ametamani kuwa sehemu ya kusanyiko. Sasa anataka kurudi ila tatizo ni namna ya kurudi. Maana aliondoka kwa kelele. Anasema yupo tayari ku face any consequence..ipi? Kutoka kwa nani na kwa ajili gani? Hiyo ni njia tu ya kutaka kurudi. Ye arudi maana ameshaona muda unakaribia wa uchaguzi.

Muda wa uchaguzi umekaribia? Ww utakuwa ni mzee, au mpiga propaganda fala.
 
Waje lakini wawe makini na hatua zao, naamini watatafutiwa sababu yoyote na hii serikali dhalimu ilimradi wafungwe mdomo, we are in a critical stage in a do or die situation at the moment.

Uwepo wake utasaidia kuamsha hari ya wengine kwenye kulaani ukandamizaji unaofanywa na CCM kupitia mahakama, na jeshi la polisi, naamini na Lissu nae atafikiria hatma yake ni ipi kama akiendelea kuwa nje ya nchi muda mrefu kwa siasa zetu.

Kina Sugu naona baada ya Samia kuingia madarakani wakaanza kumsifia anafungua milango matokeo yake amejifunga kisaikolojia sasa hivi yuko kimya hawezi kukemea lolote analinda biashara yake, Msigwa niliona tangazo anarudi kanisani.
Kumbe shida hakuwa Uncle???
 
Akiongea kupitia MariaSpaces, Godbless Lema amesema:

"Nafikiri niko tayari kurudi nyumbani. Nafikiri natakiwa kuwa on the ground kuliko wakati wowote.Nafikiri natakiwa kumuona Mwenyekiti jela au mahakamani kumtia nguvu..Nafikiri I am ready now, I am ready for any consequences."

My opinion:
Habari hii ikimfikia Mbowe, Mbowe atamshauri/atamtaka Lema asirudi nyumbani kwani namuona Mbowe ni mtu wa kuhurumia wengine kuliko hata anavyojihurumia.

Hata hivyo, Lema atarudi tu hasa ikitokea Mwenyekiti anafungwa jela ingawa nae pia anaweza kupata upinzani kutoka kwa ndugu zake wakimsihi asirudi.
Mbwembwe tu, aje alipe madeni hakuna kingine
 
Manategemea muujiza gani? Watu ni hawa hawa, Bunge ni hovyo la kizuzu,Serikali ndio hivyo tena hohehahe, halafu eti Mahakama iwe super,hao watu watatoka wapi maana ni miongoni mwa watu wa serikali
 
Back
Top Bottom