Japo Godbless Lema ametangaza nia ya kurudi nyumbani, na kwamba yuko tayari kwa lolote, naamini Mbowe atamtaka asirudi nyumbani

Na Tundu Lissu nae arudi.. aje kupambana na hawa majaji wa serikali.

Nakumbuka Lissu ndio alitushauri Watanzania tusikubali kupimwa Mkojo
Arudi tu ila tunamkumbusha siku ya maandamano yasiyokoma hatukumuona wakati ndo aliyaitisha.Tukamuona Yuko ubalozi wa Germany.
 
Akiongea kupitia MariaSpaces, Godbless Lema amesema:

"Nafikiri niko tayari kurudi nyumbani. Nafikiri natakiwa kuwa on the ground kuliko wakati wowote.Nafikiri natakiwa kumuona Mwenyekiti jela au mahakamani kumtia nguvu..Nafikiri I am ready now, I am ready for any consequences."

My opinion:
Habari hii ikimfikia Mbowe, Mbowe atamshauri/atamtaka Lema asirudi nyumbani kwani namuona Mbowe ni mtu wa kuhurumia wengine kuliko hata anavyojihurumia.

Hata hivyo, Lema atarudi tu hasa ikitokea Mwenyekiti anafungwa jela ingawa nae pia anaweza kupata upinzani kutoka kwa ndugu zake wakimsihi asirudi.

Lema anatumia akili familia yake tayari iko sawa wamepewa ukimbizi wote na watoto tayari wanauhakika wa kusoma Canada bila gharama zozote. Yeye mwenyewe tayari kapata makaratasi ya Canada. Hivyo harudi kwa kukurupuka kashajipanga vizuri.
 
Waje lakini wawe makini na hatua zao, naamini watatafutiwa sababu yoyote na hii serikali dhalimu ilimradi wafungwe mdomo, we are in a critical stage in a do or die situation at the moment.

Uwepo wake utasaidia kuamsha hari ya wengine kwenye kulaani ukandamizaji unaofanywa na CCM kupitia mahakama, na jeshi la polisi, naamini na Lissu nae atafikiria hatma yake ni ipi kama akiendelea kuwa nje ya nchi muda mrefu kwa siasa zetu.

Kina Sugu naona baada ya Samia kuingia madarakani wakaanza kumsifia anafungua milango matokeo yake amejifunga kisaikolojia sasa hivi yuko kimya hawezi kukemea lolote analinda biashara yake.
Hapana yupo swala jana limemuumiza sana mpaka presha ikamka.
Kuendana na maelezo ya Lema kwenye maria spesi.
Kwa ujumla ninaamini bado hicho chama kina wapambanaji wengi ndo maana tunawahofia sana kwa usajili wao
 
Waje lakini wawe makini na hatua zao, naamini watatafutiwa sababu yoyote na hii serikali dhalimu ilimradi wafungwe mdomo, we are in a critical stage in a do or die situation at the moment.

Uwepo wake utasaidia kuamsha hari ya wengine kwenye kulaani ukandamizaji unaofanywa na CCM kupitia mahakama, na jeshi la polisi, naamini na Lissu nae atafikiria hatma yake ni ipi kama akiendelea kuwa nje ya nchi muda mrefu kwa siasa zetu.

Kina Sugu naona baada ya Samia kuingia madarakani wakaanza kumsifia anafungua milango matokeo yake amejifunga kisaikolojia sasa hivi yuko kimya hawezi kukemea lolote analinda biashara yake.
Ungekuwa wewe ungechagua maslahi ya familia au Mbowe? Mnaojifanya kuwapigania hawana habari na nyinyi mnaonekana Matapeli tuu na waroho wa madaraka.
 
Kina Sugu naona baada ya Samia kuingia madarakani wakaanza kumsifia anafungua milango matokeo yake amejifunga kisaikolojia sasa hivi yuko kimya hawezi kukemea lolote analinda biashara yake.
Hawa sasa akina Sugu ndiyo wanasiasa makini wanapanga siasa zao kadri ya CCM ilivyo kwa wakati huo. Kwa nini ukariri kumtukana Rais muungwana kama Samia? Na hayo ndiyo makosa ya Mbowe na Lissu
 
Lema akitaka kuwa mwanasiasa zaidi ni muhimu arudi nyumbani.

Akitaka kuwa mkimbizi zaidi ni muhimu akae nje.
Enzi za utawala wa Kayafa Lema pamoja na Lissu walikuwa kwenye hit list.Chief Hangaya amerithi maovu yote aliyoyaacha Kayafa ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa Mbowe.Sioni Lema akibakia kuwa hai kama atarudi Tanzania.
 
Kipindi cha Kayafa Lema pamoja na Lissu walikuwa kwenye hit list.Chief Hangaya amerithi yote aliyoyaacha Kayafa ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa Mbowe.Sioni Lema akibakia kuwa hai kama atarudi Tanzania.
Lema anajua hata huko aliko hayuko hai, ndiyo maana anataka kurudi Tanzania.
 
It is strange kwamba usalama wa maisha ya Lema ulipungua/tishiwa mara tu baada ya uchaguzi kuisha. Waliotaka kumuua sijui kwanini hawakutishia wakati wote au kabla ya campaigns kuanza?

Siasa (both sides) ni kitu cha ajabu sana.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom