January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

ipi???sio kila MTU ameiona..kama vipi weka picha so tushachoka na vi post nusunusu
 
Nimeamua kuleta hili jibu kwenye uzi mpya kwa faida ya wengi ,
Ni jibu la swali liloulizwa kwenye uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-hizi-picha-unamaanisha-nini-maakubwa-7.html


Wengi tumebaki kumtukana January Makamba , na hata ukiingia kwenye page yake Instagram hakuna mtu mpaka sasa aliye na clue yoyote kuhusu ana chojaribu kueleza January .

Mi mwenyewe zilinichanganya baada ya kuziona , lakin baada ya kukaa na kuzichunguza kwa mda mrefu , angalau kidogo nikapata mwangaza na maudhui ya ujumbe wa hizi picha alizoweka January kwenye page yake ya InstaGRAM

Disclamer : Mimi simjui January na wala sijawahi kuongea nae , hichi ntachoandika hapa ni kwa maoni yangu mwenyewe .

Tuanze kwanza na January . Kwa wale ambao hamumjui , January ana elim ya Uzamili katika Uchambuzi wa Migogoro na Azimio ( MSc in Conflict Analysis and Resolution ) na pia alishawahi kusomea Mafunzo ya Amani .

Picha za January

Kwenye picha 3 alizoweka January , kwanza kabisa katumia mbinu ya tashtit ( satire ) kuleta maudhui ya ujumbe wa picha , anachofanya January ni kuleta maana fulani inayomaanisha maana nyingine kabisa na ile wewe audience unayoweza kufikiria , Kwa kifupi January anatumia michoro ya Paweł Kuczyński mchoraji kutoka Poland anayejihusissha sana na kuchora picha kwa kutumia mbinu ya tashiti ( satire ) zenye kutoa maoni juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia tashtit. Unaweza kuona collection ya picha zake nyingine hapa

attachment.php

Maana ya picha za January kwa kufuata mtiririko wa tarehe alizoweka.

Picha namba 1 :
Dont burn your opportunities for a temporary comfort ( Usichome fursa yako kwa ajili ya faraja ya muda )

Ukiangalia vizuri hizo picha , ya kwanza inamuonyesha mtoto akiwa amewasha moto kwa kutumia kuni ambazo chanzo chake ni ngazi anayotakiwa kutumia kutokea nje ( juu ).Huu ni ujumbe mkubwa unaoonekana kwenye picha namba 1 ambao wengi wetu tutajaribu kuuchukulia kijuu juu na bila shaka kufikiri jamaa anawapiga madongo watu fulani kwa kuunganisha na matukio mawili matatu yaliyotokea hivi karibuni.

Picha namba 2 : If Only Animals Were Given the Red Carpet Treatment That Humans Get. ( Kama wanyama tu wangekuwa wanapata heshima ya zulia jekundu ambayo binadam anapata ) .

Ujumbe huu unaweza kuuona kama wa ajabu , wengine kwa tafsiri za haraka unaweza kuuona kama una chembechembe za udini ( Fikra ambayo hata mimi niipata mwanzoni ) , sabab ukijaribu kuangalia kwa jicho la mbele hii picha inaonyesha gari kama ya kiongozi mkubwa au mtu maarufu , mlango umefunguliwa na hao wanyama wametoka ndani , wakatembea juu ya zulia jekundu na kwenda kula huku mlinzi akiwa anawasubiri aweze kuwarudisha heshima ambayo huwa wanapewa viongozi na watu maarufu tu . Tatizo ni hao wanyama ambao ni aina ya nguruwe , kiongozi mkubwa wa nchi alikua wa dini ile ya itikadi kali , Sitaki uingie kwenye udini kama mimi nlivyofikiria mara ya kwanza bali tumia IQ yako ya ziada kuubadilisha huu ujumbe , uuweke kwenye uhalisia wa jamii yetu ya Tanzania. nakuachia wewe uanganishe viulizo ( kwa lugha ya kitashi wanasema Connect the dots ) .

Picha namba 3 : Evolution facebook ( Mageuzi ya Facebook )

Kama zilivyo hizo picha zingine , ujumbe wa picha hii ni mgumu kidogo kuupata , kwanza kuna mambo matatu hapo . Kwanza ni hao watu wawili hapo chini walioko kama sokwe mtu wakiwa wamevalia suti ( hawa nimewaita sokwe wajanja ) na pili ni huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula peke yake , na la tatu ni huo mkia wa huyo huyo mtu aliyevalia kaptula unaonekana umebadilika na kwenda kuwa na alama ya facebook. Sasa unaweza kujiuliza mbona mkia una alama ya facebook , Sasa kwa nini facebook , kwa haraka utapata jibu ya kuwa facebook ni mtandao wa kijamii ambao unakuwezesha kukuunganisha na watu , Sasa kwa nini Facebook ? ni ujumbe gani anajaribu kuuficha January hapa .? Anachojaribu kuongelea January hapa hakiusiani na facebook kabisa , Bali anamaanisha kizazi cha sasa na teknolojia ya mawasiliano ambayo kwa sasa imekuwa kubwa kushinda kipindi cha zama za zamani kidogo , sasa hapa unatakiwa kuweka mitandao yote ya kijamii dunian ( Facebook , Twitter , WhatsAPP etc ) , Huyo mtu baada ya kurukia iyo kamba ambayo ukiangalia kwa umakini unaweza kuona vitu kama nyaya nyingi za umeme na vifaa kwa juu , inamaanisha baada ya kurukia hiyo kamba kwanza alikua amekamata kwa mkono , lakin alipoweka mkia kwenye waya akaanza kupata ufahama wa habari wa mtandao baada ya mkia kuanza kubadilika kuwa na alama na rangi ya facebook ( Facebook evolution ) . na ukiangalia vizuri inaonyesha ya kuwa huo mkia uko kwenye stage ya mwanzo kabisa , maana yake kama ni ufaham basi ndo ameenza kuujua , Je itakuaje akija kubadilika na kuwa facebook kabisa , nikiwa na maana huyu mtu apo juu akija kupata access ya kila punje ya information iliyowawezesha hao sokwe wajanja hapo chini kuvaa suti na kumwacha yeye na kaptula atachukua hatua gani kama akigundua hawo sokwe walivaa suti zao kijanja ? na ukumbuke wakati ye anapata ufaham wa yote hayo hao sokwe hapo chini watabaki kuwa sokwe nikiwa namaanisha bado wamebaki na sura ya mnyama wakati yeye keshapata ufaham ( amekuwa binadam ) , Sasa jiulize ni adhab gani binadam huwapa wanyama ?

Sasa Je ni nini maudhui ya ujumbe katika picha hizi huu .?

Siko hapa kwa ajili ya kutoa maana ya picha , bali ninachojaribu kueleza ni maudhui ya hizo picha , kwa hiyo nitayasema kwa kifupi sana

Picha ya kwanza na ya pili January kazielekeza kwa viongozi wakubwa waliotangulia, sasa kwa yale niliyokwisha ongea hapo juu , unaweza pata picha mwenyewe ni mambo gani January anayojaribu kuwaeleza hawa watu ,

Picha ya tatu inajaribu kuwaambia sokwe wajanja ya kwamba jamaa bado kidogo anakwenda kujua ukweli
Baada ya kuumiza sana kichwa ili kujua ni kwa nini January ameamua kutumia picha kuufikisha ujumbe huu , ilibidi kuanza kumchambua , Mwaka 2014 alishanakiliwa na gazeti la mwananchi akisema Tanzania inahitaji Raisi ambaye atakua dikteta , baada tu ya kutangaza nia ya kugombea urais na moja ya vitu alivyoongelea ilikua ni kuhusu kuanzisha mahakama maalumu itakayoshugulikia ufisadi na mengine mengi. ( Nakuomba kama una mda nenda kasome hiyo habari ), ambapo watu wengi walimpinga wakiongozwa na jarida la Business Times la 24 Oct 2014 pia mwaka 2010 alishawahi kuandikwa na Jarida la economics la marekani akiponda utawala unaotoa ahadi kila siku bila kutekeleza . Baada ya kusoma hayo , mengine mengi na kupitia hizo picha za January Makamba ndipo nikapata hasa maudhui ya ujumbe ambayo amejaribu kuufikisha . Nao unasema

WEWE MWANASIASA ULIYETUMIA UONGOZI WAKO VIBAYA KWA KUWABAGUA , KUNYANYASA NA KUWANYIMA HAKI ZAO WANANCHI , JITAYARISHE MAANA SIKU ZAKO ZIMEKARIBIA KUFIKA MWISHO .

Nimekusoma mgosi January.
 
attachment.php
 

Attachments

  • 12308658_1033701033346580_7839871259565892699_n.jpg
    12308658_1033701033346580_7839871259565892699_n.jpg
    39.2 KB · Views: 1,142
Picha 1: usitukane wakunga na uzazi bado ungalipo. Anamwambia Nani?
Picha 2: ALiyekupa wewe ndiye aliyeninyima Mimi. Hapa kunamtu kapata anadharau alikotoka. Je ni nani anaambiwa hivyo.
Picha 3: Aliye juu mngoje chini. Nani anasubiriwa ashuke baada kupanda juu na akishuka atafanywa nini?
 
Mie mwenyewe ni mtaalam wa ku analyse lugha za picha....na nimeweza ku connect dots kwa kiasa fulani naweza kubaliana na wewe kwa asilimia kubwa....na amefikisha huo ujumbe kwa lugha hiyo kwa kuwa ni ujumbe mzito ambao unagusa watu wakubwa.

Ni wenye akili na wadadisi pekee ndo wanaweza kuvunja vunja mantiki ya picha hizo na sio kutafsiri kijuu juu.

Ni watu wanaojiuliza maswali sana na sio kurukia hitimisho kwa juu tu....ni watu ambao wanaweza ku think outside the box na ku focus from different angles......
 
Wajamaa wamemtengenezea mazingira mazuri yeye anashuka kwenda kuchezea tope na nguruwe. Hapa nguruwe ni viumbe haramu ...kwenye biblia ndio vilivotupiwa majini na Yesu baada ya kumponya the possessed. Kiislam ni mdudu haramu pia. Ieleweke kwa wote.....

January hakuwa na haja ya kupost kitu controversial namna hii. Najua Magufuri ataziona/ataonyeshwa na lazima rungu lake limshukie January. It is about time.
 
Kama kampeni manager wadau wanajaribu kuinterpret
👇👇👇👇
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿 MAANA YA IZO PICHA ALIZOPOST JANUARY MAKAMBA

Nyani wawili ni Makamba na JK (kumbuka kwa Makamba kupata ujasiri wa kupost hayo lazima kuna uzito nyuma yake)...binadamu mwenye mkia ni Makufuli...Tafsiri sasa..
Nyani wawili wako pembeni wakimuangalia/shangaa binadamu kujidai nyani na kucheza mchezo wa Nyani bila kuomba ushauri, alafu kwenye makazi/mjini wakati wenye mchezo wapo na ni mchezo wa kuchezwa porini.

Ya pili, hilo ni tusi...anasema walimfanyia kila kitu yeye alitakiwa kuja na kuenjoy the ride, little do they know wanamtandikia nguruwe red carpet...na unajua nguruwe wanavyojua kujigalagaza kwenye matope na hawajui thamani ya chochote..😜😜

! Hizo chain zina wakilisha chama na huyo mtu ni Makufuli.
Anachojaribu kusema chochote atakacho fanya/jaribu kufanya, rangi yoyote atakayo paka...bado amefungwa na minyororo hawezi kutoroka, sana sana ataing'arisha minyororo iliomfunga wakati yeye akiendelea kua mtumwa...😎

Ni kweli kwani hata choice ya Kikwete baada ya Membe kuangukia pua ilikua ni Makamba..lakini Edo akaharibu mchezo wote wakaishia kwa Makufuli wakitwgemea Kikwete ataendelea kua mwenyekiti na atamcontrol...

Ile ya ngazi ina maanisha,
Mchezo wa porini....mfano wake ni pale unapopewa majina ya wauza madawa na kuwaita chemba hakuna anaejua ulichofanya ukirudi mjini unashusha mkwala mbuzi...😎😎

Ila pia hiyo ngazi inaonyesha mpandaji hatofika anakotaka kufikia nafikiri anamaanisha hiyo ngazi ni system huwezi jitengenezea ngazi bila kuwashirikisha wanasystem😃

Ukiangalia post zake zote maana yake ni karibia ile ile..!! Kwani anafeel kua alifanya kazi kubwa sana kwenye kampaini na anahisi kama kwa asilimia kubwa amewezesha Makufuli kua katika nafasi hio. So anaona kama Mheshimiwa kishapata sasa anamuona hafai..ana muignore, as they say alitegemea kua Waziri mkuu.

Hiyo ya ngazi. .nimekukubali kiongoz
 
maana ya ile picha ni kwamba wamemtandikia Magufuli kapeti ili akaishi maisha mazuri na kuinjoy lakini amegeuka na kuwa Nguruwe,huo ni udini achukuliwe hatau haraka sana


Kwani mama yake makamba ni dini gani? Na mkewe ni dini gani na je yeye ni dini gani?
 
Makamba ni mtu anayependa giza kuliko nuru, ni wa uzao wa wana wa Mungu na wanadamu ambao Mungu aliwagharikisha na maji, huyu makamba ni remnant.
 
Tafsiri sahihi anaweza kuitoa yeye Mwenyewe sisi wengine tunaweza kuwa na hisia tu za maana tofauti. Kazi iliyopo mbele yetu ni kumuunga mkono mh. Rais kwenye Mapambano yake dhidi ya Dhulma kwa Taifa letu na Wanyonge. January si Mwislam kama wengi wanavyofikiria Mkewe nI Mkristo wa Afrika Magharibi Mama yake MZAZI ni MKRISTO. WATOTO WOTE WA JANUARY NI WAKATOLIKI SIDHANI KAMA.NI rahisi kuchukia familia yake kwa sababu za kisiasa
 
January alikiri kuwa kazi za sanaa zinaweza kuwa na tafsiri tofauti tofauti. Hivyo tusiwe closed minded....kila mtu anaweza akaitazama kazi ya sanaa na kuja na tafsiri yake na watu wakaipima wakaona inaingia akilini na ikawa hivyo. Nakupongeza mleta mada kwa tafsiri zako mujarabu na binafsi nimeona zimekubaliana kabisa na picha zote hapo.

Tunakujua CCM fuata bendera hata kwenye ukweli unapinga sana.
 
Mie mwenyewe ni mtaalam wa ku analyse lugha za picha....na nimeweza ku connect dots kwa kiasa fulani naweza kubaliana na wewe kwa asilimia kubwa....na amefikisha huo ujumbe kwa lugha hiyo kwa kuwa ni ujumbe mzito ambao unagusa watu wakubwa.

Ni wenye akili na wadadisi pekee ndo wanaweza kuvunja vunja mantiki ya picha hizo na sio kutafsiri kijuu juu.

Ni watu wanaojiuliza maswali sana na sio kurukia hitimisho kwa juu tu....ni watu ambao wanaweza ku think outside the box na ku focus from different angles......

Kwa hio sie hatuna huo utaalam u must be kidding
 
Uwaziri unaota mbawa,January Kapaniki Tu.
Magufuli ni mzoefu wa Serikali na anaijua fitna vizuri kuliko watu wa pwani wanavyojidhani kuwa wanaijua Fitna.
Chato ipo kati ya makabila makubwa mawili ya mkoa wa Kagera na Mkoa Wa Mwanza. Watu wa Chato ni jamii ya watu very flexible wanaoijua fitna na ku-adjust na mazingira.
So January Usipaniki, JPM anajua ukweli wa siasa za TZ na yooote uliyofanya si ajabu anayajua and the Guy has a verrry long Memory.
 
Nilimpa za uso huku huko insta,kishaniblock,halafu anajifanya much know sana

Victoire,

Kwa kuwa wewe ni mwanamke sikulaumu sana. Ila nakushauri tu: Get a life. Stop comparing yourself to January Makamba, he's way too higher than you!
 
Last edited by a moderator:
Kitendo cha January Makamba kupost picha twitter ambazo zina maana tata kimeibua minong'ono kuwa mbunge huyo wa Bumbuli amepigwa chini kwenye baraza la mawaziri.

Hivyo atabaki mbunge tu kama wabunge wengine.

Endapo itakuwa ni kweli basi hii moja ya mambo ambayo wananchi hawakutegemea kabisa huku wachache waliamini angeweza kuwa waziri mkuu na wengi wakiamini angeweza kuwa waziri na si naibu waziri.

Huyu kijana hatufai kabisa, hana nia ya dhati ya kuwasaidia watz, watu kama hawa wanapaswa kulaaniwa
 
UKAWA aka UKIWA.....kwani nini january makamba, Nape na comrade abdala bulembo wanawakereketa sana? hawa jamaa wana sifa zifuatazo zinazofanana na nina imani ndio sababu kubwa ya machawi ya UKIWA kuchanganyikiwa....
1) walijitoa mhanga kuhakikisha MAGUFULI anamgalagaza MAMVI
2) Walikuwa wanamchana hadharani MAMVI
3) Walikuwa wanaifanya UKAWA ionekane UTOPIA mbele ya Watanzania na Dunia kwa ujumla.

Sasa nani wanaolialia? Ukawa au CCM? Huna hoja
 
Back
Top Bottom