January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

Mtu aje hapa na ushahidi kuonyesha utendaje wa kukumbukwa wa January Makamba

Fitina za kuirudisha ccm madarakani ,zaidi ya hilo hata shule aliyomaliza anakumbukwa kwa fitina alizofanya kufaulu
 
Hiyo picha ya kitimoto na red carpet hata chizi lazma aelewe maudhui, wewe unahangaika bure kupotosha maana.
 
1. Kama ni family level, inamaana ndani ya familia ya akina February kuna mtu analindwa kama rais + mlinzi?

2. Anawafumbia nini watu wa mataifa mengine wakti yeye hata hayupo kwenye level ya urais? ili useme kuwa marais wenzie huwa wanapitia pitia instgrm yake au ukuta wake wowote?

3. Lakini kwakuwa yeye ni mtanzania na ni mwanasiasa na alishawahi kuwa kiongozi, kila anachokifanya lazima kihusishwe na mustakabali wa siasa za humu nchini!

4. Je, haikuiingii akilini ukiangalia hizo picha utaona ni mmoja wa nguruwe wale anasubiriwa aingie kwnye gari la kiongozi na mlinz pembeni? Mwingine atafikiria kwamba, tulidhania ni "MTU" huyo kiongozi, kumbe ni sawa na "NGURUWE"?

5. Hiyo ya Nyani, naona kama Manyani wakubwa "walio kwepa mishale mingi" wanamshangaa nyani kijana anadanga danda kwenye nyaya za umeme badala ya kwenye miti na tena, ana mkia wenye herufi kadhaa!
- Je, ni kiongozi anayefanya mambo Fulani ya hatari kama kushika nyaya za umeme ambzo zinaweza kumsababishia hata kifo, bila kuiga mfano wa nyani wazee wanaomshangaa sasa.......kwa akili ya kawaida kabisa ujumbe huu unaenda kwa nani?
-Kwa nafasi alionayo, alishindwa kumfuata muhusika na kwemwelezea wasiwasi wake badla ya kuvaa kanga zenye mipasho?
-Amegundua nini hadi aandike hayo sasa, au huyo "nyani" katika kudanda danda kwake, amekata waya wa umeme unaoenda kwa jm au kwa mzee ym?

WANANCHI kwa ITIKADI ZOTE, kwa DINI ZOTE, TUPO NYUMA YA MAGUFULI na TUNAMWOMBEA MAISHA MAREFU! Na akienda na moto huu, tutaomba ikifika 2025 kipengele husika cha katiba kibadilishwe ili {kama KAGAME} aongoze miaka mingine KUMI!

Unaongea kitu chenye maana kubwa saana hongera mkuu... u are good..
 
Nguruwe ina maana ya kuwa Magufuli alikuwa hana hili wala lile na hakutegemewa kupata nafasi ya urais na alikuwa hajulikani sana kwenye chama. Wakamtoa uko chini yani sawa na alikuwa kwenye mabanda ya Nguruwe akila uchafu. Wakamtoa huko kwenye mabanda ya Nguruwe mpaka kwenye kapeti nyekundu ndani ya BMW. Yani wakampatia Urais.

Aiseee huu mtazamo umetisha Mkuu
 
Moja nimeielewa kuwa Magufuli atashushwa kwenye red carpet na kwenda kula na nguruwe na hadhi ya kula Ikulu itakuwa imeishia hapo. Hii vita ni ngumu tumuombee raisi wetu

Kama hata Kinana ana ICD na ni katibu mkuu wa chama na saizi wamembana Azam mwenye container 50 tu hao wengine huwezi jua, labda Kinana yumo

Ama kweli watu mna vipaji
 
January alikiri kuwa kazi za sanaa zinaweza kuwa na tafsiri tofauti tofauti. Hivyo tusiwe closed minded....kila mtu anaweza akaitazama kazi ya sanaa na kuja na tafsiri yake na watu wakaipima wakaona inaingia akilini na ikawa hivyo. Nakupongeza mleta mada kwa tafsiri zako mujarabu na binafsi nimeona zimekubaliana kabisa na picha zote hapo.

A leader must communicate to his followers in the simplest language possible. Sasa January yuko wapi zaidi? Msanii au kiongozi?
 
Mwaka huu kazi ipo ngoja tusubiri tuone,
Wengine tusiokuwa na utaalamu wa kutafisiri picha yetu macho ngoja tuone kama atajitokeza kutoa ufafanuzi.
 
1. Nyani wawili wametulia eti wanamshangaa mr nyani akicheza mchezo asioujua. Alaf mchezo uchezwa msituni yeye anadandia nyaya za umeme. Wanamshangaa.


2. Wajamaa wamemtengenezea mazingira mazuri yeye anashuka kwenda kuchezea tope na nguruwe. Hapa nguruwe ni viumbe haramu ...kwenye biblia ndio vilivotupiwa majini na Yesu baada ya kumponya the possessed. Kiislam ni mdudu haramu pia. Ieleweke kwa wote.

3. Ile nyingine jamaa kavalishwa minyororo sasa anajaribu kuipaka rangi bila kujua kuwa anaingarisha ila kizuizi/spidi gavana iko pale pale.
Ujue kila mwanachama ana kadi ya chama ivo ikiitajika kurudi inarudi na ww kubaki common soldier!

Ni lugha ya picha wala msiniulize chochote kuhusiana na makamba ....
 
Tetesi ni kuwa Dogo kapigwa chini uwaziri so kaanza mafumbo ya kipwani
 
Mkiambiwa huyu bado ana akili ya kitoto wala hamuelewi ......eti anafaa kua waziri kamili na sio naibu waziri.......huyu ni kituko kabisa , angalieni jinsi alivyo mjinga, ndo nn sasa kuweka picha za kumkejeli prezida.
 
Kama kampeni manager wadau wanajaribu kuinterpret
👇👇👇👇
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿 MAANA YA IZO PICHA ALIZOPOST JANUARY MAKAMBA

Nyani wawili ni Makamba na JK (kumbuka kwa Makamba kupata ujasiri wa kupost hayo lazima kuna uzito nyuma yake)...binadamu mwenye mkia ni Makufuli...Tafsiri sasa..
Nyani wawili wako pembeni wakimuangalia/shangaa binadamu kujidai nyani na kucheza mchezo wa Nyani bila kuomba ushauri, alafu kwenye makazi/mjini wakati wenye mchezo wapo na ni mchezo wa kuchezwa porini.

Ya pili, hilo ni tusi...anasema walimfanyia kila kitu yeye alitakiwa kuja na kuenjoy the ride, little do they know wanamtandikia nguruwe red carpet...na unajua nguruwe wanavyojua kujigalagaza kwenye matope na hawajui thamani ya chochote..😜😜

! Hizo chain zina wakilisha chama na huyo mtu ni Makufuli.
Anachojaribu kusema chochote atakacho fanya/jaribu kufanya, rangi yoyote atakayo paka...bado amefungwa na minyororo hawezi kutoroka, sana sana ataing'arisha minyororo iliomfunga wakati yeye akiendelea kua mtumwa...😎

Ni kweli kwani hata choice ya Kikwete baada ya Membe kuangukia pua ilikua ni Makamba..lakini Edo akaharibu mchezo wote wakaishia kwa Makufuli wakitwgemea Kikwete ataendelea kua mwenyekiti na atamcontrol...

Ile ya ngazi ina maanisha,
Mchezo wa porini....mfano wake ni pale unapopewa majina ya wauza madawa na kuwaita chemba hakuna anaejua ulichofanya ukirudi mjini unashusha mkwala mbuzi...😎😎

Ila pia hiyo ngazi inaonyesha mpandaji hatofika anakotaka kufikia nafikiri anamaanisha hiyo ngazi ni system huwezi jitengenezea ngazi bila kuwashirikisha wanasystem😃

Ukiangalia post zake zote maana yake ni karibia ile ile..!! Kwani anafeel kua alifanya kazi kubwa sana kwenye kampaini na anahisi kama kwa asilimia kubwa amewezesha Makufuli kua katika nafasi hio. So anaona kama Mheshimiwa kishapata sasa anamuona hafai..ana muignore, as they say alitegemea kua Waziri mkuu.
 
January alikiri kuwa kazi za sanaa zinaweza kuwa na tafsiri tofauti tofauti. Hivyo tusiwe closed minded....kila mtu anaweza akaitazama kazi ya sanaa na kuja na tafsiri yake na watu wakaipima wakaona inaingia akilini na ikawa hivyo. Nakupongeza mleta mada kwa tafsiri zako mujarabu na binafsi nimeona zimekubaliana kabisa na picha zote hapo.

Januari ni mchoraji?
 
Kutumia picha ya nguruwe, red carpet na Gari la Rais na mlinzi ina maana zaidi ya ulivyoeleza. Kila mtu anatafsiri anavyoona.

Anyway ni Mungu tu ajuae mawazo ya moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu atamlipa kila mtu SAWASAWA na mawazo Yake na na NIA ya moyo wake ikifuatiwa na matendo.


Mungu muumba mbingu na nchi mbariki Rais wetu mpendwa JPM na kumficha chini ya mbaya zako.

Queen Esther

Nimeamua kuleta hili jibu kwenye uzi mpya kwa faida ya wengi ,
Ni jibu la swali liloulizwa kwenye uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-hizi-picha-unamaanisha-nini-maakubwa-7.html


Wengi tumebaki kumtukana January Makamba , na hata ukiingia kwenye page yake Instagram hakuna mtu mpaka sasa aliye na clue yoyote kuhusu ana chojaribu kueleza January .

Mi mwenyewe zilinichanganya baada ya kuziona , lakin baada ya kukaa na kuzichunguza kwa mda mrefu , angalau kidogo nikapata mwangaza na maudhui ya ujumbe wa hizi picha alizoweka January kwenye page yake ya InstaGRAM

Disclamer : Mimi simjui January na wala sijawahi kuongea nae , hichi ntachoandika hapa ni kwa maono yangu mwenyewe .

Tuanze kwanza na January . Kwa wale ambao hamumjui , January ana elim ya Uzamili katika Uchambuzi wa Migogoro na Azimio ( MSc in Conflict Analysis and Resolution ) na pia alishawahi kusomea Mafunzo ya Amani .

Picha za January

Kwenye picha 3 alizoweka January , kwanza kabisa katumia mbinu ya tashtit ( satire ) kuleta maudhui ya ujumbe wa picha , anachofanya January ni kuleta maana fulani inayomaanisha maana nyingine kabisa na ile wewe audience unayoweza kufikiria , Kwa kifupi January anatumia michoro ya Paweł Kuczyński mchoraji kutoka Poland anayejihusissha sana na kuchora picha kwa kutumia mbinu ya tashiti ( satire ) zenye kutoa maoni juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia tashtit. Unaweza kuona collection ya picha zake nyingine hapa

attachment.php

Maana ya picha za January kwa kufuata mtiririko wa tarehe alizoweka.

Picha namba 1 :
Dont burn your opportunities for a temporary comfort ( Usichome fursa yako kwa ajili ya faraja ya muda )

Ukiangalia vizuri hizo picha , ya kwanza inamuonyesha mtoto akiwa amewasha moto kwa kutumia kuni ambazo chanzo chake ni ngazi anayotakiwa kutumia kutokea nje ( juu ).Huu ni ujumbe mkubwa unaoonekana kwenye picha namba 1 ambao wengi wetu tutajaribu kuuchukulia kijuu juu na bila shaka kufikiri jamaa anawapiga madongo watu fulani kwa kuunganisha na matukio mawili matatu yaliyotokea hivi karibuni.

Picha namba 2 : If Only Animals Were Given the Red Carpet Treatment That Humans Get. ( Kama wanyama tu wangekuwa wanapata heshima ya zulia jekundu ambayo binadam anapata ) .

Ujumbe huu unaweza kuuona kama wa ajabu , wengine kwa tafsiri za haraka unaweza kuuona kama una chembechembe za udini ( Fikra ambayo hata mimi niipata mwanzoni ) , sabab ukijaribu kuangalia kwa jicho la mbele hii picha inaonyesha gari kama ya kiongozi mkubwa au mtu maarufu , mlango umefunguliwa na hao wanyama wametoka ndani , wakatembea juu ya zulia jekundu na kwenda kula huku mlinzi akiwa anawasubiri aweze kuwarudisha heshima ambayo huwa wanapewa viongozi na watu maarufu tu . Tatizo ni hao wanyama ambao ni aina ya nguruwe , kiongozi mkubwa wa nchi alikua wa dini ile ya itikadi kali , Sitaki uingie kwenye udini kama mimi nlivyofikiria mara ya kwanza bali tumia IQ yako ziada kuubadilisha huu ujumbe , uuweke kwenye uhalisia wa jamii yetu ya Tanzania . nakuachia wewe uanganishe viulizo ( kwa lugha ya kitashi wanasema Connect the dots ) .

Picha namba 3 : Evolution facebook ( Mageuzi ya Facebook )

Kama zilivyo hizo picha zingine , ujumbe wa picha hii ni mgumu kidogo kuupata , kwanza kuna mambo matatu hapo . Kwanza ni hao watu wawili hapo chini walioko kama sokwe mtu wakiwa wamevalia suti ( hawa nimewaita sokwe wajanja ) na pili ni huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula peke yake , na la tatu ni huo mkia wa huyo huyo mtu aliyevalia kaptula unaonekana umebadilika na kwenda kuwa na alama ya facebook. Sasa unaweza kujiuliza mbona mkia una alama ya facebook , Sasa kwa nini facebook , kwa haraka utapata jibu ya kuwa facebook ni mtandao wa kijamii ambao unakuwezesha kukuunganisha na watu , Sasa kwa nini Facebook ? ni ujumbe gani anajaribu kuuficha January hapa .? Anachojaribu kuongelea January hapa hakiusiani na facebook kabisa , Bali anamaanisha kizazi cha sasa na teknolojia ya mawasiliano ambayo kwa sasa imekuwa kubwa kushinda kipindi cha zama za zamani kidogo , sasa hapa unatakiwa kuweka mitandao yote ya kijamii dunian ( Facebook , Twitter , WhatsAPP etc ) , Huyo mtu baada ya kurukia iyo kamba ambayo ukiangalia kwa umakini unaweza kuona vitu kama nyaya nyingi za umeme na vifaa kwa juu , inamaanisha baada ya kurukia hiyo kamba kwanza alikua amekamata kwa mkono , lakin alipoweka mkia kwenye waya akaanza kupata ufahama wa habari wa mtandao baada ya mkia kuanza kubadilika kuwa na alama na rangi ya facebook ( Facebook evolution ) . na ukiangalia vizuri inaonyesha ya kuwa huo mkia uko kwenye stage ya mwanzo kabisa , maana yake kama ni ufaham basi ndo ameenza kuujua , Je itakuaje akija kubadilika na kuwa facebook kabisa , nikiwa na maana huyu mtu apo juu akija kupata access ya kila punje ya information iliyowawezesha hao sokwe wajanja hapo chini kuvaa suti na kumwacha yeye na kaptula atachukua hatua gani kama akigundua hawo sokwe walivaa suti zao kijanja ? na ukumbuke wakati ye anapata ufaham wa yote hayo hao sokwe hapo chini watabaki kuwa sokwe nikiwa namaanisha bado wamebaki na sura ya mnyama wakati yeye keshapata ufaham ( amekuwa binadam ) , Sasa jiulize ni adhab gani binadam huwapa wanyama ?

Sasa Je ni nini maudhui ya ujumbe katika picha hizi huu .?

Siko hapa kwa ajili ya kutoa maana ya picha , bali ninachojaribu kueleza ni maudhui ya hizo picha , kwa hiyo nitayasema kwa kifupi sana

Picha ya kwanza na ya pili January kazielekeza kwa viongozi wakubwa waliotangulia, sasa kwa yale niliyokwisha ongea hapo juu , unaweza pata picha mwenyewe ni mambo gani January anayojaribu kuwaeleza hawa watu ,

Picha ya tatu inajaribu kuwaambia sokwe wajanja ya kwamba jamaa bado kidogo anakwenda kujua ukweli
Baada ya kuumiza sana kichwa ili kujua ni kwa nini January ameamua kutumia picha kuufikisha ujumbe huu , ilibidi kuanza kumchambua , January 2014 alishakaririwa na gazeti la mwananchi akisema Tanzania inahitaji Raisi ambaye atakua dikteta ambapo watu wengi walimpinga wakiongozwa na jarida la Business Times la 24 Oct 2014 pia mwaka 2010 alishawahi kuandikwa na Jarida la economics la marekani akiponda utawala unaotoa ahadi kila siku bila kutekeleza . Baada ya kusoma hayo , mengine mengi na kupitia hizo picha za January Makamba ndipo nikapata hasa maudhui ya ujumbe ambayo amejaribu kuufikisha . Nao unasema

WEWE MWANASIASA ULIYETUMIA UONGOZI WAKO VIBAYA KWA KUWABAGUA , KUNYANYASA NA KUWANYIMA HAKI ZAO WANANCHI , JITAYARISHE MAANA SIKU ZAKO ZIMEKARIBIA KUFIKA MWISHO .
 
Yaani we tafsiri zako ni za kiwogawoga, kwanini hukujibu kwenye uzi uleule? Au ndio njia ya kujikomba ili akufikirie kwenye ufalme wake!
 
Mungu wangu!!

Queen Esther

1. Nyani wawili wametulia eti wanamshangaa mr nyani akicheza mchezo asioujua. Alaf mchezo uchezwa msituni yeye anadandia nyaya za umeme. Wanamshangaa.


2. Wajamaa wamemtengenezea mazingira mazuri yeye anashuka kwenda kuchezea tope na nguruwe. Hapa nguruwe ni viumbe haramu ...kwenye biblia ndio vilivotupiwa majini na Yesu baada ya kumponya the possessed. Kiislam ni mdudu haramu pia. Ieleweke kwa wote.

3. Ile nyingine jamaa kavalishwa minyororo sasa anajaribu kuipaka rangi bila kujua kuwa anaingarisha ila kizuizi/spidi gavana iko pale pale.
Ujue kila mwanachama ana kadi ya chama ivo ikiitajika kurudi inarudi na ww kubaki common soldier!

Ni lugha ya picha wala msiniulize chochote kuhusiana na makamba ....
 
January alikiri kuwa kazi za sanaa zinaweza kuwa na tafsiri tofauti tofauti. Hivyo tusiwe closed minded....kila mtu anaweza akaitazama kazi ya sanaa na kuja na tafsiri yake na watu wakaipima wakaona inaingia akilini na ikawa hivyo. Nakupongeza mleta mada kwa tafsiri zako mujarabu na binafsi nimeona zimekubaliana kabisa na picha zote hapo.

Sawa. Next time basi ajitaidi kueleweka. Msomi mzuri sio yule anayejielewa yeye peke yake bali anayeeleweka kwa wanaompima. Icho ndio kigezo kikuu cha kumaward mtu hata kwenye PhD ....

Mbona masudi ibn kipanya anaeleweka vizuri tu? Lugha ya picha haina kamusi.Unachomaanisha ndicho unachomaanisha!
 
Hilo la nguruwe mimi naichukulia hivi ,kwanza kwa imani ya dini fulani Nguruwe ni Haramu ,kwa maana hiyo huyo anayetoka kwenye hilo gari amepewa mamlaka ya kuwatawala Nguruwe hivyo na yeye ni nguruwe tu kama nguruwe wengine
 
Back
Top Bottom