January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Kuna picha nimeziona kule Instagram, ni za January Makamba kwa ID zake! Sikujua anamaanisha nini ila zina ujumbe mkubwa sana na kama ni kwelihiyo ID ni verified basi Magufuli anahitaji zaidi ya Maombi.

Najaribu kuziweka humu zinanigomea naomba kama kuna mwanaJF Mwingine aliyechungulia inst anisaidie kuziweka humu.

IMG-20151129-WA0011.jpg


=======
Nimeamua kuleta hili jibu kwenye uzi mpya kwa faida ya wengi ,
Ni jibu la swali liloulizwa kwenye uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-hizi-picha-unamaanisha-nini-maakubwa-7.html


Wengi tumebaki kumtukana January Makamba , na hata ukiingia kwenye page yake Instagram hakuna mtu mpaka sasa aliye na clue yoyote kuhusu ana chojaribu kueleza January .

Mi mwenyewe zilinichanganya baada ya kuziona , lakin baada ya kukaa na kuzichunguza kwa mda mrefu , angalau kidogo nikapata mwangaza na maudhui ya ujumbe wa hizi picha alizoweka January kwenye page yake ya InstaGRAM

Disclamer : Mimi simjui January na wala sijawahi kuongea nae , hichi ntachoandika hapa ni kwa maoni yangu mwenyewe .

Tuanze kwanza na January . Kwa wale ambao hamumjui , January ana elim ya Uzamili katika Uchambuzi wa Migogoro na Azimio ( MSc in Conflict Analysis and Resolution ) na pia alishawahi kusomea Mafunzo ya Amani .

Picha za January

Kwenye picha 3 alizoweka January , kwanza kabisa katumia mbinu ya tashtit ( satire ) kuleta maudhui ya ujumbe wa picha , anachofanya January ni kuleta maana fulani inayomaanisha maana nyingine kabisa na ile wewe audience unayoweza kufikiria , Kwa kifupi January anatumia michoro ya Paweł Kuczyński mchoraji kutoka Poland anayejihusissha sana na kuchora picha kwa kutumia mbinu ya tashiti ( satire ) zenye kutoa maoni juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kupitia tashtit. Unaweza kuona collection ya picha zake nyingine hapa

attachment.php



Maana ya picha za January kwa kufuata mtiririko wa tarehe alizoweka.​

Picha namba 1 : Dont burn your opportunities for a temporary comfort ( Usichome fursa yako kwa ajili ya faraja ya muda )


Ukiangalia vizuri hizo picha , ya kwanza inamuonyesha mtoto akiwa amewasha moto kwa kutumia kuni ambazo chanzo chake ni ngazi anayotakiwa kutumia kutokea nje ( juu ).Huu ni ujumbe mkubwa unaoonekana kwenye picha namba 1 ambao wengi wetu tutajaribu kuuchukulia kijuu juu na bila shaka kufikiri jamaa anawapiga madongo watu fulani kwa kuunganisha na matukio mawili matatu yaliyotokea hivi karibuni.

Picha namba 2 : If Only Animals Were Given the Red Carpet Treatment That Humans Get. ( Kama wanyama tu wangekuwa wanapata heshima ya zulia jekundu ambayo binadam anapata ) .

Ujumbe huu unaweza kuuona kama wa ajabu , wengine kwa tafsiri za haraka unaweza kuuona kama una chembechembe za udini ( Fikra ambayo hata mimi niipata mwanzoni ) , sabab ukijaribu kuangalia kwa jicho la mbele hii picha inaonyesha gari kama ya kiongozi mkubwa au mtu maarufu , mlango umefunguliwa na hao wanyama wametoka ndani , wakatembea juu ya zulia jekundu na kwenda kula huku mlinzi akiwa anawasubiri aweze kuwarudisha heshima ambayo huwa wanapewa viongozi na watu maarufu tu . Tatizo ni hao wanyama ambao ni aina ya nguruwe , kiongozi mkubwa wa nchi alikua wa dini ile ya itikadi kali , Sitaki uingie kwenye udini kama mimi nlivyofikiria mara ya kwanza bali tumia IQ yako ya ziada kuubadilisha huu ujumbe , uuweke kwenye uhalisia wa jamii yetu ya Tanzania. nakuachia wewe uanganishe viulizo ( kwa lugha ya kitashi wanasema Connect the dots ) .

Picha namba 3 : Evolution facebook ( Mageuzi ya Facebook )

Kama zilivyo hizo picha zingine , ujumbe wa picha hii ni mgumu kidogo kuupata , kwanza kuna mambo matatu hapo . Kwanza ni hao watu wawili hapo chini walioko kama sokwe mtu wakiwa wamevalia suti ( hawa nimewaita sokwe wajanja ) na pili ni huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula peke yake , na la tatu ni huo mkia wa huyo huyo mtu aliyevalia kaptula unaonekana umebadilika na kwenda kuwa na alama ya facebook. Sasa unaweza kujiuliza mbona mkia una alama ya facebook , Sasa kwa nini facebook , kwa haraka utapata jibu ya kuwa facebook ni mtandao wa kijamii ambao unakuwezesha kukuunganisha na watu , Sasa kwa nini Facebook ? ni ujumbe gani anajaribu kuuficha January hapa .? Anachojaribu kuongelea January hapa hakiusiani na facebook kabisa , Bali anamaanisha kizazi cha sasa na teknolojia ya mawasiliano ambayo kwa sasa imekuwa kubwa kushinda kipindi cha zama za zamani kidogo , sasa hapa unatakiwa kuweka mitandao yote ya kijamii dunian ( Facebook , Twitter , WhatsAPP etc ) , Huyo mtu baada ya kurukia iyo kamba ambayo ukiangalia kwa umakini unaweza kuona vitu kama nyaya nyingi za umeme na vifaa kwa juu , inamaanisha baada ya kurukia hiyo kamba kwanza alikua amekamata kwa mkono , lakin alipoweka mkia kwenye waya akaanza kupata ufahama wa habari wa mtandao baada ya mkia kuanza kubadilika kuwa na alama na rangi ya facebook ( Facebook evolution ) . na ukiangalia vizuri inaonyesha ya kuwa huo mkia uko kwenye stage ya mwanzo kabisa , maana yake kama ni ufaham basi ndo ameenza kuujua , Je itakuaje akija kubadilika na kuwa facebook kabisa , nikiwa na maana huyu mtu apo juu akija kupata access ya kila punje ya information iliyowawezesha hao sokwe wajanja hapo chini kuvaa suti na kumwacha yeye na kaptula atachukua hatua gani kama akigundua hawo sokwe walivaa suti zao kijanja ? na ukumbuke wakati ye anapata ufaham wa yote hayo hao sokwe hapo chini watabaki kuwa sokwe nikiwa namaanisha bado wamebaki na sura ya mnyama wakati yeye keshapata ufaham ( amekuwa binadam ) , Sasa jiulize ni adhab gani binadam huwapa wanyama ?

Sasa Je ni nini maudhui ya ujumbe katika picha hizi huu .?

Siko hapa kwa ajili ya kutoa maana ya picha , bali ninachojaribu kueleza ni maudhui ya hizo picha , kwa hiyo nitayasema kwa kifupi sana

Picha ya kwanza na ya pili January kazielekeza kwa viongozi wakubwa waliotangulia, sasa kwa yale niliyokwisha ongea hapo juu , unaweza pata picha mwenyewe ni mambo gani January anayojaribu kuwaeleza hawa watu ,

Picha ya tatu inajaribu kuwaambia sokwe wajanja ya kwamba jamaa bado kidogo anakwenda kujua ukweli
Baada ya kuumiza sana kichwa ili kujua ni kwa nini January ameamua kutumia picha kuufikisha ujumbe huu , ilibidi kuanza kumchambua , Mwaka 2014 alishanakiliwa na gazeti la mwananchi akisema Tanzania inahitaji Raisi ambaye atakua dikteta , baada tu ya kutangaza nia ya kugombea urais na moja ya vitu alivyoongelea ilikua ni kuhusu kuanzisha mahakama maalumu itakayoshugulikia ufisadi na mengine mengi. ( Nakuomba kama una mda nenda kasome hiyo habari ), ambapo watu wengi walimpinga wakiongozwa na jarida la Business Times la 24 Oct 2014 pia mwaka 2010 alishawahi kuandikwa na Jarida la economics la marekani akiponda utawala unaotoa ahadi kila siku bila kutekeleza . Baada ya kusoma hayo , mengine mengi na kupitia hizo picha za January Makamba ndipo nikapata hasa maudhui ya ujumbe ambayo amejaribu kuufikisha . Nao unasema

WEWE MWANASIASA ULIYETUMIA UONGOZI WAKO VIBAYA KWA KUWABAGUA , KUNYANYASA NA KUWANYIMA HAKI ZAO WANANCHI , JITAYARISHE MAANA SIKU ZAKO ZIMEKARIBIA KUFIKA MWISHO .
 
Kwani wewe umezielewaje? Kwa picha uliyoweka ina tafsiri nyingi tofauti! Yategemeana na mtu anavyootafsiri. Wewe umeihusisha na Magufuli, mimi nimeihusisha na Afrika na nchi za magharibi. Pia nimeihusisha na mtu anayetakiwa kutoka ila alichotakiwa kukitumia ili kutoka hakimwezeshi kutoka! Hii ipo hadi ktk family level!
 
Kwani wewe umezielewaje? Kwa picha uliyoweka ina tafsiri nyingi tofauti! Yategemeana na mtu anavyootafsiri. Wewe umeihusisha na Magufuli, mimi nimeihusisha na Afrika na nchi za magharibi. Pia nimeihusisha na mtu anayetakiwa kutoka ila alichotakiwa kukitumia ili kutoka hakimwezeshi kutoka! Hii ipo hadi ktk family level!
Umesomeka mkuu kwa mawazo yako wala usipate shida.
 
Mtu unaifwatilia account na post za watu bila sababu za msingi na kutaka mtu asiwe huru ku express mambo yake ndiyo Utoto na Upumbavu. Kwani shida nini hapo we piga kazi fanya yako
 
Kwani wewe umezielewaje? Kwa picha uliyoweka ina tafsiri nyingi tofauti! Yategemeana na mtu anavyootafsiri. Wewe umeihusisha na Magufuli, mimi nimeihusisha na Afrika na nchi za magharibi. Pia nimeihusisha na mtu anayetakiwa kutoka ila alichotakiwa kukitumia ili kutoka hakimwezeshi kutoka! Hii ipo hadi ktk family level!

Inawezekana na ww umeelewa ila unapindsha tu ubongo!
 
ati anachoma nyumbae wakati yupo ndani na ngazi za kupandia zishapukutika!....../
UTOTO UNAMSUMBUA HUYO...
MAGUFULI SONGA MBELE,DUNIA INAONA JUHUDI ZAKO!
NO ONE TO RESIST YOU! SONGA BABA!
 
Back
Top Bottom