January Makamba akataa bahasha za milioni moja za "Lunch"

Bado,bado,tena bado sana.Hatuwezi kumuamini simply like this,mtoto wa nyoka ni nyoka,babaye(mropokaji)was frontline kuhakikisha mafisadi wanarudi bungen,au tumesahau jamani?ni kwel kabisa JM anatafuta huruma ya watz akubalike countrywide na hizi ni mbinu azitumiazo.JM anasaka umaarufu kwa udi na uvumba lkn sis si mataahira as he thinks,I believ hilo si wazo lake kuna mtu nyuma yake.Na ikitokea dingi yake akaaga mashindano(kafa)umaarufu utakuwa umepotea,nan asiyejua dogo kapita kwa hila za dingi yake akisaidiana na mkwere?Simwamini mbunge wa ccm,never.
Huna lolote lakuchangia kuhusu wajumbe wa Kamati ya nishati na Madini kupewa posho ya
1M tena na Tanesco leo Tanesco inashindwa kuwahudumia Watanzania kwakuwapa umeme wa uhakika,Bili ya umeme imepanda kwa asilimia 18,Tanesco inajiendesha kwa Hasara ya Bil30 kwa mwaka.We unafikiri haya yote chanzo chake nin kama sio huu upuuzi.Hapa Ishu ni 1M ya Posho huo umbea mwingine cjui JM what an what sio ishu,tumtumie JM kama source ya hii newz ya 1M kwaajili ya posho ya Wajumbe.
 
Wakati huo huo Kamati ya Bunge inayoshughulikia Nishati na Madini imelazimika kuanza kazi mapema kutokana na makali ya mgao wa umeme.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi za Bunge mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo January Makamba alisema lengo ni kubaini kwa haraka sababu za kukosekana kwa umeme nchini.


Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema kesho wajumbe wa kamati hiyo watakwenda Mtera kutizama hali halisi ya uzalishaji umeme kutoka kwenye chanzo hicho.


Akizungumzia safari hiyo alisema imegharamiwa na ofisi za Bunge ingawa awali ziara za namna hiyo zilikuwa zikigharamiwa na serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.


“Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch’ ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge,” alisema January.


Kwa habari kamili soma hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=23734


Hongera January kwa mwanzo wenye picha nzuri,Mungu akutangulie uonyeshe utofauti.
 
Michezo hiii wabunge wengi wanafanya kwenye kamati zao. Wanapewa bahasha kwenye maofisi mengi wanayokwenda

Mnakumbuka mwakyembe mbunge wa CMM tunayemwamini naye aliwai kulamba bahasha mara mbili mbili. TAKUKURU walitaka kumuhoji akagoma kwa mgongo wa anatafutwa. sababu ya richmond.

Ebu fikiria mtu awe mbunge alafu waziri alafu awe kwenye bodi kama tatu hivi. Teh teh teh.

some "talented" politician are getting a lot of money.

BTN
Heko January Makamba.
 
Mnyonge munyonge lakini haki yake umpe, kufikia sasa mh.January Makamba ...
Wa kumpongeza ni yule aliyeamua kwamba kuanzia sasa hela ya kuisimamia TANESCO isitoke TANESCO. Wabongo tumejaza turkey stuffing kwenye vichwa. Oversight committee ya TANESCO inalipwa na yuleyule anaefanyiwa oversight.

Makamba msanii, anasema anawaomba wenzake wakatae hela, wakati tayari mfumo umeshabadilishwa, malipo hayatoki tena TANESCO. Sasa anaomba nini, au mimi ndio sielewi?
 
Wa kumpongeza ni yule aliyeamua kwamba kuanzia sasa hela ya kuisimamia TANESCO isitoke TANESCO. Wabongo tumejaza turkey stuffing kwenye vichwa. Oversight committee ya TANESCO inalipwa na yuleyule anaefanyiwa oversight.

Makamba msanii, anasema anawaomba wenzake wakatae hela, wakati tayari mfumo umeshabadilishwa, malipo hayatoki tena TANESCO. Sasa anaomba nini, au mimi ndio sielewi?

Ambacho hujaelewa ni hivi nakupa mfano

Ofisi yetu imetutma auditors wawili kufanya kazi mtwara kwa siku tatu.Imetuipa per diem zote may be za siku saba .

Kufika kule mtwara ile ofisi tuliyotumwa kufanya kazi nayo tunakuta wameshatutaftua na kulipia nyumba ya kulala wageni wameshalipa chakula. na zaidi tunapewa "bahasha" za kujikimu tukiwa mtwara

Hope umeelewa hapo.

Politician tena wale wa ngazi za juu wanakamata doubledouble kwa style hii. Ni kitu cha kawaida. lakini sio ethical

Wakati wewe unamshangaa January basi naamin wenzake(wabunge/wanakamati) wengi watakuwa wanamshangaa kuwa huyu Janury vipi hajui mambo yanavyokwendaga.

I just wish isiwe nguvu ya soda tu.
 
Jamani tusiwe wajinga kiasi hiki.haya ndio yale yale ya kumshabikia Jk ka mazuzu mwaka 2005 sasa embu tazameni anayotufanyia.Januari ni mnafiki tu,angalieni kafikaje hapo alipo,yuko kwenye kundi lile lile la mafisadi.Tuwe waangalifu sana wandugu.Tuna kasumba mbaya sana ya kushabikia vitu bila kuangalia upande wa pili kuna nini,yameshatugharimu haya na yataendelea...
 
Aaaaah hii kali, ila kwa ujumla wake tz sio maskini, hata huu mgao wa umeme/stima kama Wakenya wasemavyo huenda kuna njama, mnakumbuka kipindi fulani tanesco walisema tatizo ni maji, shelukindo alipofuatilia na kukuta maji mengi, wakasema mzee tatizo sio maji ni mitambo mibovu, labda kuna watu wanafaidika na huu mgao wa stima. Haiwezekani nchi iwe na mgao kwa miaka zaidi ya kumi bila ufumbuzi,miaka yote hiyo kilio kilio kilio ni mgao mgao mgao mgao mgao mgao!!!!!!!!!!!! Tumechoka na huo wimbo:a s 20::a s 20::a s 20::a s 20:
 
Think about a million for lunch plus parliametary allawances mind you this pratice has been going on unbated ever since Lakini masikini watoto wa walalahoi vyuo vikuu wakiomba walau waongezewe shs elf kumi kutoka shs elfu tano IGP Mwema kwa kushinikiza na watawala anamwaga FFU wanatandaza mabomu ya machozi nakumimina maji ya upupu katika mkanganyiko huo watoto wa masikini wanaumizwa na wengine mimba zinatoka bila kusahau muda wa masomo unaopotea Kuna kipindi wakati wa Mkapa waziri wa mambo ya ndani aliliambia Bunge kuwa gharama ya kumlisha mfungwa mmoja ni shs 4000/= kwa siku kiasi ambacho nadhani kitakuwa kimepanda zaidi ya mara mbili kwa sasa Kama mlo wa mfungwa ni wa ghali kuliko wa wanafunzi wa chuo ni moja wapo ya maajabu ya dunia kwenye GUINESS BOOK Walalahoi inabidi tutafakari na tuchukue hatua Hosea hana ubavu wakuwakoromea mabwana zake after all he should have been fired a long time ago after Richmond saga so is there to safeguard the intrest of his boss
 
Milioni ya lunch?Lunch ya milioni ikoje kwanza??Kwa style hii maendeleo yatabaki kua hadithi Tanzania!

Hawa watu wapumb...... sana yaani wanadriki kutoa "Lunch" ya milioni 1 kweli!!! Ama kweli waTZ tutaendelea kunufaisha wachache huku walalahoi tunaumia! Ndo maana tunarundikiwa gharama kwenye umeme kumbe wanalipa kiajabu hivi? Kwenye madini nako bla bla tu hakuna cha maana tunachopata kama Taifa. Kwa kweli uongozi wa Mkwele hawana lolote la kujivunia, yaani Mkulu amelala fofofo huku nchi inaliwa. Sasa hiyo Milioni si ya kuwanyamazisha ili wakikuta kuna uozo wafunike kombe mwanakharamu apite!!!

Wa-TZ tumekwisha! Bila kuchukua hatua kama za Waarabu tutaendelea kunyonywa huku wachache wanajilimbikizia mali.
 
Kama ni kweli vizuri sana na waliotoa washughulikiwe.

Ila wasiwasi wangu huyu jamaa asije kuwa anajikosha pengine kaona ndogo alitaka kubwa zaidi sasa kaamua kuchafua:msela: na wengine wasipokee.

Mie binafsi siasa za kobongo naziona za kinafiki nafiki sana.

Kama ile ya PM kukataa shangingi kwani hakujua tangu mwanzo akazuia manunuzi?

kwa nini hatujifunzi toka kwa majirani zetu kenya jamani? mie inaniuma sana.
 
Wabunge wetu wanasikitisha!
Kumbe wao ndio wanaoongoza kufuja keki ya nchi hii!...halafu tunategemea watetee wananchi...ni tofauti ya mbingu nanchi!
Hizo ni posho za nini, zinatolewa na nani, kwa bajaeti gani, a kwa manufaa ya nani!:A S 20:
System overhAul might work...Ndio maana wachina wanatwanga risasi watu wahuni kama hawa!

January Makamba unaonyesha mwanzo mzuri sana!...Ujue umewafanya wananchi wengi sana wakuamini kwa hilo tu!...Yako mengi ambayo unaweza kuyakataa...take a break, slowly and slowly, u may be our hope young man!
 
Kuzuia hizo pesa, maana yake anataka aende kufanya huo uchunguzi huko mtela wakiwa clean, ili wasiwe na hofu na woga ksia wamepewa mil1
Mipango mingi ya maendeleo TZ haifanyiki kisa ni hicho kila ngazi ni rishwa na wapokeaji hawawezi kuwawajibisha wahusika hata kama kuna tatizo.
Hizo bahasha zinatoka bajeti gani?

Tanzania zaid ya tuijuavyo, Kweli Lunch ya million moja!!!!

January hivi kuzuia hizo hela ni kuwaomba wabunge wazikatae???
 
safi kwa kijana huyu kuonyesha mfano, lakini ingependeza zaidi kama atagombea next time akiwa nje ya chama cha mafisadi

Anaandaliwa huyu aje kuchukua nchi, keshaambiwa atafute umaarufu kwanza kwa kusema na kutenda yasiyo moyoni mwake, nina uhakika si mpiganaji wa kweli.
 
Hizo bahasha zinatoka bajeti gani?

Tanzania zaid ya tuijuavyo, Kweli Lunch ya million moja!!!!

January hivi kuzuia hizo hela ni kuwaomba wabunge wazikatae???

Kazikataa ili iweje?
Kwamba yeye ni mmoja wa wenye uchungu na wafujaji wa pesa na rasilimali za nchi hii?
Njia anayoitumia sio!
 
Mwanzo Mzuri January!. Lakini Usiishie kutoa ushauri tu, kama bahasha zikitoka hakikisha Unawaripoti wahusika TAKUKURU ili tujue kwamba kweli una mean Bussiness otherwise tutakuona msanii tu!.
 
Kwa ujumla alichofanya JM sio issue kubwa lakini tumpongeze kwa siasa za 'looking good' - huko mbele ya safari atujui lengo lake.

My point is inakuaje siri-kali inampa mtu hela zetu 1m kwa ajali ya msosi? Na unaweza kuta ni ya siku moja tu. Wa ngapi wanakubali haya ma 'bribe' ya chakula ambaye hawajatajwa? Yani hapa ni uwizi mtupu.
 
Back
Top Bottom