January Makamba akataa bahasha za milioni moja za "Lunch"

Wakati huo huo Kamati ya Bunge inayoshughulikia Nishati na Madini imelazimika kuanza kazi mapema kutokana na makali ya mgao wa umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi za Bunge mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo January Makamba alisema lengo ni kubaini kwa haraka sababu za kukosekana kwa umeme nchini.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema kesho wajumbe wa kamati hiyo watakwenda Mtera kutizama hali halisi ya uzalishaji umeme kutoka kwenye chanzo hicho.

Akizungumzia safari hiyo alisema imegharamiwa na ofisi za Bunge ingawa awali ziara za namna hiyo zilikuwa zikigharamiwa na serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.

“Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch’ ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge,” alisema January.

Kwa habari kamili soma hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=23734

Huyo aliyeweka vijisenti ndani ya bahasha ni nani? Ni Ngeleja au Rostam? TAKUKURU wako wapi washughulikie uchafu huu?
 
Nilichojifunza ni kuwa kumbe ugomvi wa kuwania kamati una siri nyingi nyuma ya pazia. Daah, mi nilijua wabunge wanagombea kuwasaidia wapiga kura wao, kuumbe!
 
Ninaangalia na kukodoa macho yangu kwa nguvu ili nione na kukielewa kinachoendelea nitawahabarisha wakati muafaka. Maana mazingaombwe kama fani ni sanaa yenye kuamini sha vitu visivyokuwepo. Lakini kama inavyosema si "uchawi" bali wepesi wa vidole.
 
"Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch' ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge," alisema January.

wandugu,

..nilivyoelewa mimi ni hivi:

..January Makamba anazungumzia matukio yaliyotokea kwa Kamati ya Nishati na Madini ya zamani siyo hii ya sasa.

..zaidi, anasema safari hii, kwa kamati hii anayoiongoza, atawaomba wajumbe wake wakatae bahasha za "lunch" kwasababu bunge ndiyo litagharamia safari yao.

NB:

..sasa kwasababu bunge ndiyo linagharamia safari, je wajumbe wa kamati watapewa na bunge "lunch" ya shilingi ngapi?
 
yaani wanapeana rushwa wao kwa wao?????
 
Sasa nyie mnashangaa lunch? Mbona mambo mengi yako inflated? Kwani hamjui hata dizeli ya magari yao wanapewa Tshs 2500 kwa lita wakati bei elekezi iko chini ya hiyo?
 
Wakati huo huo Kamati ya Bunge inayoshughulikia Nishati na Madini imelazimika kuanza kazi mapema kutokana na makali ya mgao wa umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi za Bunge mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo January Makamba alisema lengo ni kubaini kwa haraka sababu za kukosekana kwa umeme nchini.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema kesho wajumbe wa kamati hiyo watakwenda Mtera kutizama hali halisi ya uzalishaji umeme kutoka kwenye chanzo hicho.

Akizungumzia safari hiyo alisema imegharamiwa na ofisi za Bunge ingawa awali ziara za namna hiyo zilikuwa zikigharamiwa na serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.

“Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch’ ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge,” alisema January.

Kwa habari kamili soma hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=23734

huyu january analazimisha umaarufu au uwaziri. anataka JK amuone mchapa kazi ili apewe uwaziri. mbona anasahau mapma?

1. huyu january alinufaika na rushwa kwenye malaria nomore
2. wahindi walimpa 600millioni kwenye kampeni yake
3. amepokea rushwa sana akiwa ikulu, leo anakuwa mother theresa?
4. dada yake mwamvitta kapokea 30% kibao toka vodacom ambazo alitumia kwenye kampeni inakuwaje leo ni msafi?

january asituchezee akili zetu.......kwa sababu ameona hela ndogo ndo maana anatuzingua? Arudishe za malaria no more, za ikulu, za wahindi na za vodacom... hanari ndo hiyo
 
This is good news!!! tunawaombea wabunge vijana muendelee kuibua maovu haya na ndio maana akina hamad rashid mohammed (political prostitute) wanang'ang'ania at the expense of poor tanzanians
 
huyu january analazimisha umaarufu au uwaziri. anataka JK amuone mchapa kazi ili apewe uwaziri. mbona anasahau mapma?

1. huyu january alinufaika na rushwa kwenye malaria nomore
2. wahindi walimpa 600millioni kwenye kampeni yake
3. amepokea rushwa sana akiwa ikulu, leo anakuwa mother theresa?
4. dada yake mwamvitta kapokea 30% kibao toka vodacom ambazo alitumia kwenye kampeni inakuwaje leo ni msafi?

january asituchezee akili zetu.......kwa sababu ameona hela ndogo ndo maana anatuzingua? Arudishe za malaria no more, za ikulu, za wahindi na za vodacom... hanari ndo hiyo
hakuna aliyesema yeye ni malaika na hakuna aliyekana kwamba hajanufaika na ufisadi.... tunachopongeza ni kitendo alichofanya... ulitaka azipokee kesho uendelee kupiga kelele??

Hivi ni lini tutajua kwamba penye jema ni vyema tuka -acknowledge? kama ambavyo tunashabikia mabaya ya mtu??

Je ni wangapi walikua wabaya leo wamebadilika na kuwa hata viongozi wa dini??

wewe ni dini gani?? maana niliposoma mimi kwenye vitabu ni kwamba wengi tu walikua wabaya na badae wakawa waalimu na watakatifu
 
Sasa nyie mnashangaa lunch? Mbona mambo mengi yako inflated? Kwani hamjui hata dizeli ya magari yao wanapewa Tshs 2500 kwa lita wakati bei elekezi iko chini ya hiyo?
Wow!!!

Halafu tunasema tuna PCCB inafanya kazi... au na wao wanalipana hivyohivyo?
 
January is not perfect, likewise me and you.

Nilisema mwanzo, he have a potential of becoming a great leader. This is one of many steps that he is suppose to take to become a great leader.
 
Sasa nyie mnashangaa lunch? Mbona mambo mengi yako inflated? Kwani hamjui hata dizeli ya magari yao wanapewa Tshs 2500 kwa lita wakati bei elekezi iko chini ya hiyo?

labda wanatumia disel tofauti na hii tunayotumia sisi walalahoi bin taabani
 
be careful ndugu yangu... tumpongeze lakini its too early kumhusudu, you never know!
kwani hamkumbuki mdingi wake huyu Yufuph alipokuwa RC dar Watu walimpenda sana.Leo mnamwonaje YUSUPH? Hivyo tuwe na subira tumpime kama ninguvu yake toka moyoni au ni ya soda.
 
Back
Top Bottom