January Makamba akataa bahasha za milioni moja za "Lunch"

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Wakati huo huo Kamati ya Bunge inayoshughulikia Nishati na Madini imelazimika kuanza kazi mapema kutokana na makali ya mgao wa umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi za Bunge mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo January Makamba alisema lengo ni kubaini kwa haraka sababu za kukosekana kwa umeme nchini.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema kesho wajumbe wa kamati hiyo watakwenda Mtera kutizama hali halisi ya uzalishaji umeme kutoka kwenye chanzo hicho.

Akizungumzia safari hiyo alisema imegharamiwa na ofisi za Bunge ingawa awali ziara za namna hiyo zilikuwa zikigharamiwa na serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.

"Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch' ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge," alisema January.

Kwa habari kamili soma hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=23734
 
Mnyonge munyonge lakini haki yake umpe, kufikia sasa mh.January Makamba kwa maoni yangu ni mbunge pekee aliyejipambanua kuwa na vipau mbele vinavyogusa mambo ya msingi kwa wakati tulio nao,kwa hilo nazidi kumpongeza. Pamoja na hayo hili suala la wajumbe wa kanati iliyopita kupewa lunchi ya shs1 milioni ni rushwa, TAKUKURU inapashwa ifuatilie suala hilo na wananchi tujulishwe.:msela:
 
Takukuru iwahoji waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo wasisubiri mpk tuandamane plz hosea usiendelee kutuudhi , hawa tumewachagua waende kutuwakisha bungeni si kusanya posho mbili hii ni rushwa ya wazi huwezi kulipwa 2 times kwa same activity
 
Hizo bahasha zinatoka bajeti gani?

Tanzania zaid ya tuijuavyo, Kweli Lunch ya million moja!!!!

January hivi kuzuia hizo hela ni kuwaomba wabunge wazikatae???
 
Duh, milioni moja per day? then watu wamecheleweshewa mishahara hamna hela?:coffee::coffee:
 
Mnyonge munyonge lakini haki yake umpe, kufikia sasa mh.January Makamba kwa maoni yangu ni mbunge pekee aliyejipambanua kuwa na vipau mbele vinavyogusa mambo ya msingi kwa wakati tulio nao,kwa hilo nazidi kumpongeza. Pamoja na hayo hili suala la wajumbe wa kanati iliyopita kupewa lunchi ya shs1 milioni ni rushwa, TAKUKURU inapashwa ifuatilie suala hilo na wananchi tujulishwe.:msela:
Tangu siku alipomuandikia barua Waziri wa Nishati na Madini aelezee mambo yanayohusu umeme,ununuzi wa mitambo,uajiri wa wanasheria.Nilimuona huyu Mh. kama mpiganaji kijana ndani ya mdomo wa Mamba
 
6 alishawahi kukemea wabunge kupokea posho 2x! But, 1m 'lunch' sio double posho, ni bonge la HONGO 100% aisee!
 
I have escorted these big sana waheshimiwa and they are not given any red cent, unless they bring a formal, signed and authorised request.......I have moved from generation consultancy to transmission so I will miss this visit and I will miss to pick their brains...

No red cent from TANESCO whilst CAG is watchin
 
Milioni ya lunch?Lunch ya milioni ikoje kwanza??Kwa style hii maendeleo yatabaki kua hadithi Tanzania!
 
safi kwa kijana huyu kuonyesha mfano, lakini ingependeza zaidi kama atagombea next time akiwa nje ya chama cha mafisadi
 
Kumbe serikali yenyewe ndo wanao endekeza rushwa, ndo maana Rashidi wa KAF anang'ang'ana kuwemo kwenye kamati! Ingekuwa yeye angepita nazo!
 
Du dau kubwa sana hivi nyuma ya huu mgawo kuna nani? ni AJABU KM HATA HAPO BUNGENI WAPO wauaji wa TANESCO
nashukuru kwa kutujuza na TAKUKURU hebu fuatilieni huko isije ikawa km Richmond kwa msaada zaidi link nzuri kwa Gazeti hilo ni
Tanzania Daima - Sauti ya Watu samahani Ng'wanza Madaso nimeirekebisha link yako ili ipatikane vizuri hasa kwa wanaotumia Mozilla Fire Fox
 
Mnyonge munyonge lakini haki yake umpe, kufikia sasa mh.January Makamba kwa maoni yangu ni mbunge pekee aliyejipambanua kuwa na vipau mbele vinavyogusa mambo ya msingi kwa wakati tulio nao,kwa hilo nazidi kumpongeza. Pamoja na hayo hili suala la wajumbe wa kanati iliyopita kupewa lunchi ya shs1 milioni ni rushwa, TAKUKURU inapashwa ifuatilie suala hilo na wananchi tujulishwe.:msela:

In the group clouded with all sorts of unwanted things, he must single out himself as not one of those that think everyday its business as usual. Kwa kuanza sio mbaya....nampa muda kujua it would be how long!
 
safi kwa kijana huyu kuonyesha mfano, lakini ingependeza zaidi kama atagombea next time akiwa nje ya chama cha mafisadi

Ukimsifia January huenda hujaelewa siasa za Tanzania. Kama angekuwa kwenye timu ya ukombozi asingeingia kwenye kinyanganyiro cha kumtoa Shelukindo kwa pesa za Rostam. Kama mnahitaji ukombozi wa kweli acheni kughilibiwa, jitahidi kutofautisha kati ya mchele na pumba
 
Nina mashaka na haya aliyoyasema huyu kijana January... Tusiamini sana ndugu zangu, huyu jamaa anatafuta huruma na umaarufu kutoka kwa wananchi!!! Aondoe kwanza boriti kwenye jicho lake ndio ahangaike na kibanzi jicho la mwenzake.
 
Back
Top Bottom