Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa kibali cha Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Mtukula hadi Tanga lenye urefu wa km 1147.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James A. Mwainyekule amesema EWURA imetoa kibali cha Ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kwa EACOP.
Kibali hicho ni cha kujenga Bomba la mafuta ghafi kuanzia Mtukula Mkoni Kagera hadi Chongoleani Mkaoni Tanga.
James A. Mwainyekule, amesema Bomba hilo litapita katika Mikoa nane ambayo ni Kagera, Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Wanaozuia bomba la mafuta gafi lisijengwe ni Wanafiki. Kayasema hayo wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (#EWURA) ikitoa kibali cha ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Mtukula Mkoani Kagera hadi Chongoleani, Tanga lenye urefu wa KM 1147.
amesema “Kuna maneno mengi kuhusu bomba, wenzetu Ulaya wakidai halistahili kujengwa, hata Bunge la Ulaya limetoa Azimio ambalo ni maneno tu, wenzetu Nchi za Afrika na zinazoendelea kuna unafiki tena mkubwa sana, msingi wa maendeleo yao ilikuwa ni uvunaji wa rasilimali kama hizi mfano makaa ya mawe na gesi.”
Makamba amesema tahadhali zote za kimazingira zimechukuliwa kwani baada ya bomba kujengwa, juu yake tutapanda miti kiasi kwamba hutajua kama bomba limepita.
Bomba hilo litapita Mikoa 8 ambayo ni Kagera, Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.
Naye Omary Mgumba, Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa nane ambayo bomba limepita amesema hali ya Usalama ni nzuri. Wanaendela kufundisha wanavijiji ambapo bomba linapita ili walinde miundombinu kabla, wakati na baada ya mradi kumalizika.
Pia ameomba Serikali kuongeza Vituo vya Polisi kwenye Vituo sehemu bomba linapita.
Makamba: Juu ya bomba la mafuta kutapandwa miti
Kuna maneno kuwa linapita kwenye mbuga za Wanyama, vyanzo vya maji, watu wataathirika, hizo ni propaganda.
Kuna kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira, bomba litakapopita patapandwa miti juu yake kiasi kwamba itakuwa ngumu kujua kama kuna bomba limepita.
Watu 9,898 wataguswa na mradi na kati yao watu 390 tu ndio ambao ardhi yao itachukuliwa na wamepewa fursa kama wanataka kujengewa nyumba nyingine au kulipwa, hakuna vurugu wala nguvu iliyotumika.
85 wameamua kujengewa nyumba, tumelipa fidia Tsh. Bilioni 29 kwa wale ambao bomba litapita katika maeneo yao, kazi ya kulipa inaendelea.
Kuhusu haki za binadamu zimezingatiwa, NEMC walitoa maelekezo ya nini cha kufanya, mradi pia utatoa ajira na manufaa ya kiuchumi.
Makamba: Kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira na Haki za Bnadamu
Akizungumzia ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Kagera hadi Tanga amesema kuna kazi kubwa imefanyika kulinda mazingira sehemu ambapo litapita.
Amesema “Watu 9,898 wataguswa na mradi, kati yao Watu 390 ndio ambao ardhi yao itachukuliwa na wakapewa fursa kuchagua kujengewa nyumba nyingine au kulipwa, 85% wameamua kujengewa, pia tumelipa fidia Tsh. Bilioni 29 kwa ambao bomba litapita katika maeneo yao na zoezi la kulipa linaendelea.”
Aidha, amesema Haki za Binadamu zimezingatiwa kwa kuzingatia muongozo wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).