Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.
Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.
Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.
Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.
Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!
Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.