JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

🫠🫠 Nimeangalia nyingi lakini hii ndio imebaki kwenye External mpaka Leo nikimiss kumuangalia mo palmo analia au ile royalty yake kwa general naweka 🤣🤣
Nikimiss Mugol na ohi kupigana na weka, nikimmiss Have mosu mwenyewe naweka hapa napata Hadi machozi wakati Prime minister ameorganize troops kwenda kummaliza.
General haek chi alikua royal sana kwa His majesty 🤣🤣🤣
Mimi Jumong ndio series niliyoirudia mara nyingi sana , haichokeshi kila nikirudia nahisi kama mpya .

Ile ya Haemosu alivyovamiwa na kuuwawa likuwa kikatili sana , ila niliEnjoy kipindi kile kifupi Jumong alivyokuwa akiishi na Haemosu ilikuwa so emotional.

Safari ya kutafuta chumvi milima katika milima huko Gosan na Ile vita ya kwanza dhidi ya Yimbom na Imdoon iliyosababisha Jumong kupotea , zile episode zilikuwa 🔥 🔥

Mwamba Jumong nakubali sana utulivu wake katika mipango na kufanya maamuzi.
 
secretarybird unapata ban kizembe mwanangu kwa kujaa kwenye mifumo ya wajinga mpaka mnatukanana hovyo.

Anyway, ban njema ukirudi njok usalimie huku

Cc : Mad Max
Dah, imeniuma sana. Atakua alijaa kwenye mfumo. Kuna watu ukigombana nao wanakimbilia polisi. Fastaa wanakureport unakula ban.

Mtu akikukera, unamuandikia matusi PM. Vya PM haviendi kwa Mods.
 
Dah, imeniuma sana. Atakua alijaa kwenye mfumo. Kuna watu ukigombana nao wanakimbilia polisi. Fastaa wanakureport unakula ban.

Mtu akikukera, unamuandikia matusi PM. Vya PM haviendi kwa Mods.
Nilikuwa namtania na kumsihi asile ban Jf inachangamka sana akiwepo .

Unakuta jitu linakukera makusudi linakutukana halafu yeye hata akila ban na ID upupu kama huyu ,yeye anakutukana kwa makusudi ujae kwenye mfumo akuripoti
IMG_20261011_210640.jpg
 
USIKU UNA MASWALI YAKE.

Mchana unaweza kucheka na watu, lakini usiku ukibaki peke yako ndipo mawazo yanapopata nafasi ya kuzungumza.

Kuna mambo huyasemi kwa mtu yeyote, si kwa sababu huna cha kusema, bali umejifunza kuwa si kila mtu ataelewa unachopitia.

Usiku mwema kwa wenye mawazo mengi na maneno machache.
 
Una punch lines Kali na maneno kuntu , nimejifunza kitu hapa
 
Watu wamezoea kukuhukumu kwa hali yako ya leo, wakasahau kuwa maisha hayajasimama hapo.

Punguza maneno, ficha mipango, jenga maisha yako. Siku matokeo yatakapoongea, hutahitaji kujitetea.

Usiku mwema kwa wanaojijenga kimya kimya.
 
Moja kitu nilichojifunza kwenye maisha tembea .

Ukiona mambo yako hayaendi eneo uliopa na una msongo wa mawazo hama nenda sehemu nyingine , hii Ina Faida sana kiakili , kisaikolojia na kiuchumi.

Ila angalizo Kabla ya kwenda mahali chunguza kwanza sehemu yenyewe , aina ya watu , fursa , mazingira nk
 
Back
Top Bottom