🌿 Positive Affirmations kuhusu Kuepukana na Negative Energy
1. Nachagua amani yangu kuliko drama zisizo na maana.
2. Sitaruhusu maneno ya watu yaamue thamani yangu.
3. Nina haki ya kujitenga na mazingira yanayoninyang’anya amani.
4. Ninalinda akili yangu dhidi ya mawazo hasi na ushawishi usio na afya.
5. Nachagua kuwa karibu na watu wanaonijenga, kuniheshimu na kunitia moyo.
6. Si kila jambo linahitaji majibu yangu; wakati mwingine ukimya ni hekima.
7. Ninaachilia kile nisichoweza kudhibiti na kuelekeza nguvu zangu kwenye ninachoweza kubadilisha.
8. Moyo wangu hauhitaji kubeba chuki, hasira na mizigo ya wengine.
9. Ninajifunza kusema “hapana” bila kujisikia mwenye hatia.
10. Ninalinda mipaka yangu kwa sababu amani yangu ina thamani.
11. Sitaruhusu mtu mwenye huzuni ndani yake anifanye nipoteze furaha yangu.
12. Kila siku nachagua mawazo yanayonijenga badala ya yale yanayonivunja.
13. Ninaweza kuondoka mahali bila chuki, lakini kwa heshima ya nafsi yangu.
14. Ninastahili mazingira yenye amani, heshima na positivity.
15. Nina nguvu ya kuchagua kile ninachoruhusu kiingie moyoni mwangu.
🔥 Kauli ya leo
“Linda amani yako. Si kila mtu anayekuja kwenye maisha yako anapaswa kupewa nafasi ndani ya moyo wako.” 🌱
Kumbuka: Kuepuka negative energy si kuwachukia watu. Ni kujua ni nini unachoruhusu kikuchukue nguvu, muda na amani ya akili.