SEKTA MUHIMU: Mwanaume Mashine na Ustahimilivu wa Manhood
Wanaume, leo tunamalizia wiki yetu kwa kugusia swala zima la Mwanaume Mashine. Hapa ndio sekta muhimu zaidi linapokuja swala la manhood.
Nitagusia mambo machache ambayo kwa namna moja au nyingine yamekuwa yanatuathiri wengi wetu kisaikolojia na kimwili.
Ukweli Kuhusu "Kukosa" Nguvu za Kiume
Kwanza kabisa, hakuna mwanaume asiye na nguvu za kiume kabisa, bali wengi wetu tuna upungufu tu wa nguvu hizo.
Mwanaume asiye na nguvu kabisa ni yule aliyezaliwa na changamoto hiyo kibaolojia na hajawahi kusimamisha hata siku moja tangu azaliwe. Kama ulishawahi kusimamisha, wewe una uwezo, shida ni upungufu tu.
Vyanzo Vikuu Vya Upungufu wa Nguvu za Kiume
Matatizo ya Kisaikolojia (Hofu ya Kushindwa):
Hapa unajikuta unapata hofu ya kufanya vizuri just kwa sababu kuna siku ulikamia "kupiga show" kisha mashine ikagoma kusimama. Aibu au fedheha uliyopata siku hiyo inakaa kichwani, inakujengea hofu ya kutokewa na jambo hilo tena. Hofu hii isipodhibitiwa, inazaa tatizo kubwa la kisaikolojia.
Madhara ya Punyeto:
Kitendo cha kujichua kwa muda mrefu sana kinadhoofisha mishipa na misuli ya uume, na kuufanya uwe legelege. Mwisho wa siku mashine haisimami inavyotakiwa.
Adha ya Picha/Video za Ngono
(Pornography):
Ubongo wako unakuwa stimulated kupita kiasi. Matokeo yake, ukigusa tu mwanamke unamwaga mapema na gemu inaisha. Pili, kwa kuwa umezoea picha za ngono, unakosa hamu kabisa ukiwa na mwanamke live, kwa sababu ubongo wako umeshafanywa uamini kuwa ngono halisi ni ile ya kwenye video.
Mambo ya Kijinga Tunayoyaamini (Mitazamo Potofu)
Eti lazima uwe na dushe kubwa ili mwanamke aenjoy: Huu sio ukweli kabisa! Matokeo yake mnahangaika kunenepesha uume for nothing. Hata mwanaume mwenye nchi mbili (inch 2) anaweza kumfurahisha mwanamke vizuri sana akijua jinsi ya kutumia.
Eti mwanamke anapata kilele (kukojoa) kwa kupigiwa show ya masaa mengi: Hapa ndipo mnahangaika na Mkongo au mavumbi ya ajabu ajabu na kujichosha bure. Kiuhalisia, wastani wa mwanamke kufikia kilele ni ndani ya dakika 7 hadi 13, ikitegemeana na jinsi ulivyomuandaa (foreplay) na utayari wake.
Suluhisho la Uhakika:
Njia za Kurudisha Imara ya Mashine
Kumbuka: Hakuna dawa ya papo kwa hapo (instant) ya kutibu upungufu huu. Zilizopo (kama Viagra na vumbi) ni za muda mfupi tu; unameza sasa hivi, unapata nguvu, ukimaliza tendo tatizo liko pale pale. Unakuwa mtumwa wa dawa.
Nguvu za kiume zinategemea sana mzunguko sahihi wa damu kwenda kwenye uume. Ili kurekebisha mzunguko huo naturally, fanya haya:
Ufahamu pia kuna uhusiano mkubwa sana wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu mwilini,kwani damu ndio inayofanya uume usimame kwa kwenda kujaa sehemu ile na dushe kusimama,sasa remedy ya kwanza ni mazoezi,mazoezi humairahisha mzunguko wako wa damu na kuufanya uume wako uwe imara kabisa
Pili kuna mazoezi ya kegel ambayo unaweza kufanya hapo chumbani kwako,haya mazoezi ukifanya ndani ya miezi mitatu tu,utaona tofauti yake,uume unasimama vizur kabisa,na unachelewa kumaliza tendo, haya nimeyadhibitisha mimi binafsi,yani ni show show,hata kwa mtu ambaye gari linazimika ndani ya uke hapo shida hiyo imeisha kwakuwa yanaimarisha tatizo hilo,just go YouTube na ujifunze namna ya kufanya mazoezi hayo
Tatu,ufanisi wa afya ya uzazi inaenda sambamba na kula vizur,ule mlo kamili,matunda,mboga mboga,maziwa,mayai na yanayo shahabiana na hayo,mwili ukiwa unapata haki yake kwa virutubisho sahihi basi hata mashine nayo inakuwa vizuri.
Kwa shida ya kisaikolojia ambayo inakuletea hofu ya kushindwa tendo,jitahidi kuondoa hofu hiyo kwa kuamini kuwa unaweza kufanya vizur tu,mwambie mwenza wako shida yako ili akuwezeshe kuishinda hali hiyo,afahamu kwamba upo kwenye mchakato wa kupona kwahiyo avumilie pale unaposhindwa kuperfom,awe na subira akutie moyo na kadri utakavyoanza kuondoa hofu yako kichwani kwako basi kidogo kidogo utazidi kuimarika na kuwa fresh kabisa,nimepitia hayo najua yanawezekana kabisa.
Kumbuka kupona kunahitaji muda basi kikubwa kuwa na subira na endelea na jitihada za kuimarika siku hadi siku
Asante kwa kufuatilia wiki ya wanaume hapa usiku wa manane,na leo tumeimaliza rasmi.
Asante.