JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

hata sikumuelewa maana anao ujuaji mwingi mi nilipitia jana asubuhi nikasema mbona haviingiliani hata kidogo then nikatoka sijarudi tena,, vipi kuna mpya nika chungulie tena Seran
 
haya kafute ile link kwanza😂😂😂😂
Siifuti!
1782543600008.gif
 

Wanaume na Usafi







Ni dhahiri kabisa, wanaume wengi bado tunasuasua kwenye swala zima la unadhifu. Unakuta geto la mwamba halijulikani kama anakaa binadamu au ni stoo ya mkaa!


Hata kama unakaa kwenye chumba kimoja, mpangilio wa nafasi yako unazungumza kwa sauti kubwa kuhusu wewe ni nani. Ukipanga vitu vyako vizuri, chumba kinakuwa smart, na hata kufagia au kupiga deki inakuwa rahisi sana. Lakini wengi wetu hatupo hivyo—ukiona siku hiyo mwamba anasafisha chumba chake, basi jua kuna shori anakuja kutembelea.



1. Usafi wa Mwili na Mavazi


Utamsikia mtu anajitetea: "Nioge ya nini wakati nalala peke yangu?"


Guys, kwani usafi wako unategemea uwepo wa mwanamke geto? Je, hujui kuwa huu ni kwa faida ya afya yako mwenyewe? Usafi huanza na wewe, kwa ajili yako.



2. Janga la Nguo za Ndani (Boxers)


Hapa sasa ndio kuna balaa kubwa. Utamkuta mwamba ana boxer mbili tu! Kwa namna hii usafi utatoka wapi? Mtu anavaa boxer moja siku nne hadi tano mfululizo—kama sio uchafu huu ni nini?


Ushauri wa Bure: Atleast kwa kiwango cha chini, mwanaume uwe na pair saba (7) za boxer. Walau baada ya siku mbili unabadilisha. Kweli hadi usafi wa nguo za ndani uhitaji kusukumwa au kuambiwa?


3. Nukia Vizuri, Jenga Confidence


Kama unavyopenda mwanamke au mke wako awe smart na mwenye kuvutia kwa ajili yako, basi jua hata wao wanafurahi sana kukuona na wewe uko nadhifu.


Mwanaume piga manukato (perfume) na unukie vizuri!



  • Kwanza, inakufanya ujisikie vizuri mwenyewe (you feel good about yourself).
  • Pili, inakujengea heshima na mvuto mbele ya watu wengine.

Binafsi, napenda sana kunukia vizuri—inanipa confidence ya hatari kila ninapokatiza.



Tusiwe smart kichwani tu, bali tuwe smart na nadhifu kwenye kila nyanja ya maisha yetu. Usafi ni utambulisho wako.


Kesho tutamalizia Wiki ya Wanaume kutoka hapa Usiku wa Manane.


Alamsiki!
 
Back
Top Bottom