JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mapole, nale nahaya gheke! Yabiza kinehe mamunu ga ng’wenomo kalekorwa sana nene kuyumba na binge chiza? Lyanike lenge lyabizile na chuki leledoka chene🫢
Lyanike lenge tena 😳?
Thinking Waiting GIF by NoireSTEMinist.gif

Ambha, bahnu balena wivu sana!
 
Mwanaume, Usitabirike! Siri ya Kulinda Mvuto Wako Kwenye Mahusiano

Wanaume bado tupo pamoja tunabadilishana mawazo. Leo nataka kushea nanyi jambo moja muhimu sana ambalo wengi tunafeli, nalo linahusu Mvuto wako (Attraction) kwenye mahusiano.

Sikiliza kijana: Mwanaume usiwe unatabirika. Unapotabirika, unapoteza mvuto wako (mystery) kwa mwenza wako. Na unapokosa mvuto, automatically unakuwa unaboa!

Mwanamke akishajua wewe ni mtu wa namna gani, ratiba zako zote anazijua kichwani, na anajua ukasirishwapo unafanya nini au ukifurahi unafanya nini—basi unamfanya asiwe interested na wewe tena. Umeshamaliza utamu wote kwa sababu tayari anajua mwenendo wako mzima.

Je, Nini Cha Kufanya Ili Usitabirike?
Hapa ndio sehemu muhimu ambayo inabidi twende pamoja. Ili uwe mwanaume mwenye mvuto wa kudumu, lazima uwe mtu wa "amsha amsha" na mabadiliko ya kisaikolojia.

Badilika kulingana na mazingira: Siku nyingine unakuwa mpole sana na msikilizaji, siku nyingine unakuwa mcheshi na mchangamfu, na siku nyingine unakuwa serious na mwenye msimamo mkali (bila kufanya vurugu

Mshughulishe kiakili: Hali hii ya kutotabirika inamfanya mwenza wako ajiulize kila siku: "Huyu mtu mbona simuelewi vizuri leo?" Hapo unakuwa umeiteka akili yake na unakuwa sehemu ya mawazo yake kila saa. Hapo ndipo mvuto unapozaliwa.


Mifano Halisi ya Maisha (Kutabirika Vs Kutotabirika)

Mfano wa 1: Kisa cha Mchezaji Kaká na Mkewe wa Zamani
Wanawake hawapendi mwanaume aliyepoa sana na aliyenyooka kama rula. Huwa wanapenda "mishe mishe" na changamoto kidogo. Chukulia mfano wa mchezaji nyota wa zamani wa Brazil na Real Madrid/AC Milan, Kaká.
Pamoja na umaarufu wake wote, utajiri, tabia njema, na kumpa mkewe maisha ya kifahari, bado mkewe alikuja kuomba talaka. Sababu ilikuwa nini? Mkewe alisema wazi kuwa: "Kaká alikuwa mtu mkamili sana, amenyooka sana, hana makosa." Maana yake ni kwamba alikuwa anatabirika mno kiasi cha kuboa. Mahusiano yanahitaji amsha amsha na mabadiliko ili yasizobie!

Mfano wa 2: Ratiba na Kushtukiza (Surprises)
Mwanaume Anayetabirika: Kila siku ya Jumamosi saa 11 jioni anakuja nyumbani akiwa ameshika mfuko wa chipsi na kuku. Hakuna jipya, hakuna mabadiliko. Baada ya miezi sita, mwanamke hata akisikia mlango unafunguka anajua kabisa ni "chipsi kuku" imeingia. Hamasa inaisha.
Mwanaume Asiyetabirika: Jumamosi hii anarudi na matunda tu, Jumamosi ijayo hamwambii chochote anamwambia "vaa twende" kisha anampeleka sehemu mpya kabisa ambayo hawajawahi kwenda. Siku nyingine anachelewa kurudi kidogo akifanya dili zake bila kutoa maelezo ya kina ya kila sekunde. Hii inamfanya mwanamke awe na hamu ya kukutana naye kila siku.


Shukrani za Kipekee kwa Wadau!
Napenda kumalizia kwa kuwashukuru wadau wote ambao mnaendelea kupitia uzi huu na kusoma maandiko yetu ya nyuma kabisa.

Kuna wadau wanasoma na ku-like, na wanatupa feedback ya nguvu kwamba tupo pamoja. Mfano, kuna wadau mchana huu wamelike maandiko ambayo nilitupia mwezi kama huu mwaka jana, 2025! Unakuta notifications za vishindo (likes) zinapop kwenye screen yako ya simu.
Safi sana wakuu, mchango wenu tunauona. Tupo pamoja, tukutane kwenye uzi ujao!
 
Back
Top Bottom