WIKI YA WANAUME ,Epuka Mtego wa "Yes King": Kupoteza Akili Kisa Unapenda
Bado tunaendelea na Wiki ya WANAUME hapa JamiiForums, ndani ya kiota chetu cha usiku wa manane. Kuchika kukicha, na leo nataka tuguse jeraha ambalo wengi wetu tunalilea kimyakimya.
Hommies, leo tuzungumzie huu ugonjwa wa kukubali kila kitu (Yes-Man) ili mradi tu kumfurahisha mwenza wako.
Hili ni kosa la kijinga sana ambalo wanaume wengi tunalifanya. Eti kwa kuwa mwanamke unampenda, basi hata akiongea pumba au upuuzi uliopitiliza, wewe unaitikia tu kichwa kama mjusi wa ukutani—yote hayo in the name of love. Ukiulizwa kwa nini unafanya hivyo, huna hata majibu ya kueleweka. Unajichekesha tu!
Kumpenda Mtu Kusikufanye Uwe "Chizi"
Listen guys, kumpenda mtu haimaanishi upoteze uwezo wako wa kufikiri (reasoning capacity). Haimanishi uweke akili yako mfukoni na kutanguliza hisia mbele.
Mambo ya kuendeshwa na hisia 100% waachie wenye nazo—ambao ni wanawake. Mwanaume umeumbwa utumie hisia kidogo sana, na AKILI NYINGI MNO. Au hamjasikia maandiko yakisisitiza: "Ishi nao kwa akili"?
Mfano wa Kwanza:
Mwanamke wako anakuja na wazo la kijinga kabisa la kibiashara. Anakwambia, "Baby, kuna mtindo mpya wa kupaka kucha mjini, nataka nikope laki tano nianze biashara hiyo kesho." Wewe unajua kabisa kucha sio kipaumbele cha eneo lenu na hiyo hela itapotea, lakini kwa sababu tu hutaki anunenepe mdomo, unajibu: "Sawa baby, wazo zuri sana, ngoja nikupe mimi hiyo hela."
Huko ni kupoteza akili!
Wanawake Wanatutega (Na Wanajua Ukweli)
Pale ambapo mwanamke wako kachochola (kaboronga), muweke sawa kistaarabu. Pale anapoleta hoja mbovu, weka mambo sawa kwa misingi ya ukweli. Mwisho wa siku, atakuheshimu na kukupenda zaidi.
Hivi umeshawahi kujiuliza; mwanamke anajua kabisa hapa nimeongea upuuzi au nimefanya ujinga, halafu wewe mwanaume unakuja kumsifia na kumuunga mkono. Hivi unadhani anakuchukuliaje? Haoni kama kapata mwanaume, anaona kapata "shabiki" au "fala" wa kumuendesha.
Mfano wa Pili:
Mmetoka wote out, akafanya fujo au kumfokea mhudumu wa mgahawa kisa tu kamcheleweshea kinywaji kijinga. Mnaingia kwenye gari anakwambia, "Umeona nilivyomkomesha yule muhudumu? Amenikera sana!" Wewe badala ya kumwambia ukweli, unajibu, "Eeh baby, safi sana, ulifanya vizuri kumnyoosha."
Bro, hapo anakudharau kimyakimya. Anajua huna msimamo na huwezi kuwa kiongozi wake.
Acha Hofu ya Kuachwa
Listen, acha hofu ya kijinga eti “nikimkosoa atajisikia vibaya” au “atapata picha kwamba namuona hana maana, ataniacha.”
Kama ukimrekebisha kwa hoja za msingi, kwa sauti ya kiume na kwa ustaarabu bila kufoka, trust me, utaonekana mwanaume wa maana sana kwake. Wanawake wanavutiwa na wanaume wenye msimamo (frame), sio wanaume bendera hufuata upepo.
Mwanaume ni Kiongozi. Na kiongozi anyoosha pale mambo yanapoenda mrama, hajidhihirishi kuwa mnyonge kisa anasaka mapenzi.
Kama vipi, tukutane kesho katika muendelezo wa Wiki ya Wanaume, hapa hapa jukwaani, kwenye uzi wetu pendwa wa Usiku wa Manane.