JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.
I like your courage SM....I believe we need to take some legal action against ccm. Keep it up!



Mkuu P;

Tuko ukurasa moja Mkuu.

CCM can fool some people all the time; but they cannot fool the people all the time . . . . now we see the light . . . . we'll stand up for our rights . . . . Get up, Stand up, stand up for your right, dont give up the fight . . . .

Mambo ya Bob hayo. Cheers!

Peace & Love.

Respect.
 
Last edited by a moderator:
wakitaka kujiunga wajiunge........wasipotaka watuachie jf yetu....
 
Hii spidi ni kubwa kuliko in less than 20 min tayari umepata maadvocates mmekubaliana terms? mwanzo ulisema inategemea JF admini wakiafiki tayari wameshaafiki, that is great.

Mkuu Quinine;

Heshima mbele Kamanda!

You can chhose to Trust; Dunia ni kama kijiji with Communication Technology. Jana walikuwa walikuwa wameomba kuipitia Press Release kwanza na baada ya hapo watatushauri. Kwa wanasheria Wazalendo hawahitaji Fees kwenye kesi kama hizi sana sana gharama za mahakama yenyewe ambazo si za kutisha katika kufungua kesi.

Niliwasiliana na Maxence pia juu ya hili.

Any way I hope by jioni tutakuwa tumepata jibu.

Respect.
 
Madai ya CCM si ya kupuuzwa kuna jambo la msingi hapa katika Forum ambalo kwa hakika linahitaji kutazamwa kwa jicho la tatu:
1. kuwa critical thinkers haimaanishi kukosoa kila jambo, nimewahi kulisema hili katika moja ya thread zangu baada ya kupokea changamoto ambazo kwa kweli ukipima huoni msingi wa hoja ulikuwa wapi zaidi ya ushabiki.

2. Kuna mabadiliko makubwa katika mwenendo wa uchangiaji katika forum, nimelitazama hili kwa muda sasa mpaka wakati mwingine nasita kuomba fikara za watanzania kwa kuwa utaishia kupokea michango iliyojaa matusi na kejeli isiyotoa hoja za kitaalam na zilizotafitiwa. Ushahidi mzuri soma thread zote za wiki hii uchuje mwenyewe.

3. Kinadharia na mlengo wa Hoja nyingi ambazo hazitoi mizani sawa katika uchambuzi zinaweza kujenga hoja ya nguvu kwa madai ya CCM.

4. Inawezekana wapo wanajamii wenye mlengo wa wastani na wahafidhina ambao kamwe mawazo yao ni sahihi kuliko ya wengine.

5. Hii ni forum yenye heshma na msaada mkubwa katika jamii, tutumie taaluma na hoja zenye kuleta mabadiliko ya kweli katika kuleta ustawi wa maisha ya Mtanzania. Nilipendezwa sana na Hoja ya Mwanakijiji last week kuhusu hoja ya CHADEMA na ukosoaji wa Utawala. Ilijaa mantiki na yenye kutoa taswira sahihi ya Upinzani na mabadiliko.

6. Haya ni mawazo binafsi na si msimamo wa Taasisi yoyote wala kipindi chochote katika chombo chochote cha habari.

Yahya M

From Fikra Pevu - Political Paranoia? Tanzania's Ruling Party threatens online social media | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

The following is the statement issued earlier today by JamiiForums - the most prominent Tanzanian online social gathering. The popular political forum played a crucial role in a lead up to the General Elections in October 2010 by being the most authoritative source of politica news, discussion and debate. However, few days ago JamiiForums came under a well calculated and targeted attack by the ruling party - Chama cha Mapinduzi - which accused the forum for being "anti-CCM" and "anti-government".


The statement was distributed to a variety of media outlets in the country and abroad as well as to a number of interested parties.
 
Yaani wee acha tu! Sijawahi kuona potential lawsuit ikiwa discussed na potential plaintiffs publicly namna hii. I am going to go out on a limb and say this 'potential lawsuit' being spearheaded by Superman will not see the light of day. Quote me!!

Haaaa haaaa;

Mkuu; kufungua kesi kuna tabu gani kama facts zote zipo?

People has done it and it never sounds as u think!

Respect.
 
h.sep7.gif
Jamii Forum yaijibu CCM


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
MTANDAO wa Jamii Forums umesema madai ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Tanzania Bara), Pius Msekwa, kuuhusisha mtandao huo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ya kubuni na yana lengo la kuwatisha Watanzania kutoa maoni yao kwa uhuru kupitia mitandao mbalimbali.
Mtandao huo ulianzishwa mwaka 2006 na madai hayo kwamba mtandao huo unafanya kazi hatarishi dhidi ya CCM na serikali yana lengo la kuuchafua na kuuvunjia hadhi ambayo imejijengea kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu.
"…Ni jaribio dhaifu la Chama cha Mapinduzi kubebesha lawama mitandao ya intaneti kwa mapungufu na migongano iliyojitokeza ndani ya chama chao katika miaka michache iliyopita na siku za karibuni," ilisema taarifa hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mtandao huo unaotembelewa na wastani wa watu 20,000 kwa siku umekanusha madai hayo kwa maelezo kuwa hayana msingi wala ukweli.
"Tunapinga vikali madai yasiyo na msingi ya Chama cha Mapinduzi kuhusu umiliki, malengo na nafasi ya JF (Jamii Forums) katika medani ya vyombo vya habari nchini na mchango wake katika mijadala ya kisiasa nchini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Ilisema kwa mara ya kwanza waliyasoma madai hayo yakiwa yameripotiwa kwenye magazeti mawili ya kila siku.
Kwa mujibu wa mtandao huo hawajawahi kufadhiliwa na CHADEMA lakini wanaamini kuwa wamelengwa na CCM kwa sababu katika miaka mitano iliyopita mtandao wao umekuwa ukishiriki vilivyo kufichua kashfa mbalimbali ambazo zimelindima nchini hatimaye kusababisha chama tawala kuamua kujivua gamba.
Mtandao huo umesema madai hayo yamesomwa na kusikiwa na watu wengi nchini hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa. Yamesababisha wasiwasi usio wa lazima kwa wanachama 40,000 ambao wametawanyika pote nchini na katika kila kona ya dunia.
Madai hayo ya CCM yalitolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Msekwa wakati wa kutambulisha uongozi mpya wa chama hicho.

Good Start!

Cheers Matola!
 
Mwanakijiji, inasikitisha kuona hata vijana wa leo fikra zao zimekuwa za uoga kupindukia. Usishangae hayo ya kuogopa CCM, mfano mdogo wa jinsi CCM ilivyoharibu psych ya watanzania ni pale unapoenda benki na kuona tellers na services mbaya kupindukia na hakuna hata mmoja anayethubutu kumconfront manager au kufunga account kuwalazimisha watambue uzito wao. Watanzania utawasikia wakilalamika huku wakiwa wamekaa kwenye foleni ndefu na ATMs hazifanyi kazi. Mpaka hapo tutakapotambua umuhimu wa kupigania hazi zetu ndio tutabadilika. Press release kama hii ni mojawapo ya njia za kusafisha damage done over many years.

Mkuu Gogomoka;

Tuko Ukurasa moja.

Peace & Love.

Respect.
 
Kama nilivyosema awali ni vyema kupitia vielelezo vilivyopo na kufanya maamuzi sahihi. Kwenda mahakamani ni haki ya kila ambaye anaona haki yake imekanyagwa na mwingine bila kujali unyonge wake wala ubabe wa aliyeikanyaga. Katika hili muda unahitajika angalau kujiridhisha kama JF watakuwa na kesi dhidi ya CCM au la. Ni jambo la kisheria ambalo halipaswi kusukumwa na hisia.

Katika hili kuna walalamikaji zaidi ya mmoja, YouTube, Twitter, Facebook na CHADEMA. Wote waliotajwa ni tishio wanaweza kulalamika. Chadema wanaonekana wamesingiziwa kumiliki mtandao ambao sio wao. Huo unasemekana ni uongo. JF wanasemekana kumilikiwa na Chadema wakati si kweli. Je kumiliki au kumilikiwa katika hali hii kuna athari kisheria? Kwa maneno hayo JF/Chadema wamepoteza sifa mbele ya jamii? Huu ni mfano tu nimeutoa. Yote yanawezekana ila ni lazima kuangalia hili suala kwa mapana yake na si hisia.

Wakati hayo yanaendelea hakuna kinachotuzuia kuendelea kuwa JF. Mijadala ndiyo inayotufanya tuwe JF hivyo tuendelee kujadili.

Mkuu MA;

Asante sana kwa taarifa ya awali. Ni vema nawe pia ukaipitia zaidi na kutujulisha kama: Je; kwa kusema uongo dhidi ya JF na kutupakja matope, sheria inasemaje? Usituulize sisi wana JF bali wewe kama Mwanasheria ndiyo utpatie maoni na Pro and cons!

Peace & Love.

Respect.
 
Melo na mwenzake Mushi walishawai kamatwa na kuhojiwa na police. Tundu lisu chadema ndio mwanasheria wao. Utakataaje kama si mtandao wa chama. Mijadala iwe ya busara si matusi wala uchochezi ulivyo sasa. Hakuna uhuru bila mipaka.

Oooh My . . . !

JF zaidi ya uijuavyo! What is the connection hiyo Mkuu?

So, Mwanasheria angekuwa Lamwai JF ingekuwa ya CCM?

Respect.
 
mwanakijiji,

kuna tuhuma nzito zinafufuka huku tuliko kwamba umenunuliwa na chadema baada ya pesa yako ya dhamana kwenye kesi yako kuishi marekani bila visa.

chadema kupitia mbowe na slaa na wafuasi wa mengi walilipia dola 5000.

kwa sisi wengine huo ni mgongano wa maslahi. ghafla umeanza kuwa nape wa chadema.

tuthibitishie ni chadema wamelipa udhamini wako.

imekuwaje mtu unajifanya mtetea ufuataji wa sheria unaishi nchi za watu ukivunja sheria.
 
Yaani Mkuu Max hapa ndio mmewamaliza kabisa

"Tulitarajia kuwa badala ya kulaumiwa kuwa tunafanya kazi "hatarishi" kwa CCM na serikali yake, chama hicho kingetoa tuzo kwa mtandao huu kwa ujasiri dhidi ya ufisadi kwani ni kutokana na kazi yetu hiyo tumeweza hata kuonyesha kuwa kulikuwa na gamba lisilotakiwa ndani ya chama hicho kikongwe
"

Kwa sababu kama kweli wamedhamiria kupambana na mafisadi ndani ya chama, hawana budi kupongeza kila anawesaidia kuwafahamu na kuwafichua mafisadi hao........hapa ndipo nia yao inapopimwa na kujua kama kweli wamedhamiria au wanatania
 
I swear upon my forefathers, that I will continue to act irregularly to the most uncouth party in Tanzania called CCM . I am ant and will continue to be ant -CCM .. MAGAMBA for the rest of my life.

Pius Msekwa is just a mzee who needs to rest . I wonder if he knows how to browse JAMIIFORUMS.com
 
mwanakijiji,

kuna tuhuma nzito zinafufuka huku tuliko kwamba umenunuliwa na chadema baada ya pesa yako ya dhamana kwenye kesi yako kuishi marekani bila visa.

chadema kupitia mbowe na slaa na wafuasi wa mengi walilipia dola 5000.

kwa sisi wengine huo ni mgongano wa maslahi. ghafla umeanza kuwa nape wa chadema.

tuthibitishie ni chadema wamelipa udhamini wako.

imekuwaje mtu unajifanya mtetea ufuataji wa sheria unaishi nchi za watu ukivunja sheria.


Naomba fuatilia kwa makini ushauri niliokupa kwenye post yako ya jana kabla mambo hayajakuharibikia...umesikia Sophia Simba
 
Dawa ya moto sio maji, ni moto. CCM waache unazi. Kama walikuwa na MAGAMBA, wangeshindaje kwa kishindo. Wavue magamba (wawe makini wasijejikuta bila kivazi) watoe na sumu walizozipanda hao MAGAMBA.

Msekwa alipokuwa spika hakuwa GAMBA kama sasa.

Keep it up JF.

Wengine walikuwa hawana ila kwasasa yanaota!
 
Hawa ccm kama hawataki kusemwa si waondoe mfumo wa fikra huru na mawazo binafsi ili wafikirie badala yetu? Kama ni kiongozi mzuri na genuine kwanini uogope kukosolewa?
 
Kuna wakati mwingine ni vizuri tu kuweka rekodi straight. CCM na taasisi zake wanajipanga vilivyo tu kuhakikisha kuwa nguvu za mitandao hii zinakuwa muted.

Kuna hatua kadhaa ambazo zinapikwa ambazo zinalengo la kusababisha mabadiliko makubwa ya mambo haya ya mawasiliano ili kuweza kuhakikisha kuwa serikali inakuwa na upper hand katika kudhibiti "vurugu, uchochezi n.k". Hili lililofanywa na kina Msekwa ni utangulizi tu wa yale yaliyomo.
Mzee Mwanakijiji, hili lina ukweli ndio maana ile miswada miwili ya huduma za habari (Media Services bill 2007 ) na haki ya kupata habari, (The Right to Information Bill, 2007)kwanza ilikuwa miwili, sasa itaunganishwa na kuwa mswada mmoja tuu Media Bill, ulishapita hatua zote mpaka baraza la mawaziri, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
 
katika mapambano kati ya fikra zenye tija na itikadi za ushabiki wa ccm mambo kama haya ni ya kawaida kutokea. kama wanaona wana-jf ni CDM wajisajili walete hoja hapa sio kuwadanganya wa-tz ambao wengi wao hata kama sio members wamekuwa wakisoma comments zetu na mambo mbalimbali tunayoibua humu.

naungana na member aliyesema kuwa hizi sio zama za zidumu fikra za m/kiti.

waende zao na chama chao cha magamba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom