Jamani wanaume wasomi mna nini?

Mi nafikiri hiyo dharau na majigambo haitokani na hiyo elimu ni tabia tu mtu anakuwa nayo sema huyo elimu ndo imekuwa fimbo ya kumchapia mkewe.
 
wakati wanatongozana huyo shemeji alikuwa akikupigia simu kulia lia na wanazohongana anakugawia?
 

Na wenye degree, dini moja, wameajiriwa, wengine kabila moja na hata wamekuwa mtaa mmoja wanaachana hawa unawaweka kundi gani???!!!
 
Tatizo huja hivi, kwanza rafiki yako kutokana na digrii yake alijiona mjuaji tangu awali. Alipokutana na huyo mumewe akaendeleza ujuaji japo jamaa bila shaka alikuwa akimsoma. Kwa kuwa hawakuwa wakiishi pamoja jamaa hakujua undani wa mwanamke. Walipooana ndio jamaa akaanza kumjua. Pengine alimvumilia awali lakini bado mwanamke alileta ujuaji. Wanawake wasomi wajuaji sana hata kama hawajui. Sasa naona jamaa kachoka ujinga wa mkewe na kumtolea uvivu.
 
Mi nafikiri hiyo dharau na majigambo haitokani na hiyo elimu ni tabia tu mtu anakuwa nayo sema huyo elimu ndo imekuwa fimbo ya kumchapia mkewe.

Na mke pia naweza sema kamuendekeza sana huyo "msomi" jibu lilikuwa tangu mwanzo ni "kama elimu ni kikwazo niendeleze na mimi" au "nimeolewa na wewe sio elimu yako tuheshimiane" au "wenye PhD pia bado wapo"

Ingawa wanasema ukimya ni busara kuna sehemu yaweza kuwa ukimya ndio tatizo!!!!
 

Kama kamchoka basi amuache tu ndio suluhisho la kudumu kama sio kumuendeleza naye apate elimu inayoitwa ya juu!!!!

Sio maneno na manyanyaso kwa dada wa watu, amteme akiwa bado anatazamika watu wajitoe muhanga kabla ya lala salama
 
Kama kamchoka basi amuache tu ndio suluhisho la kudumu kama sio kumuendeleza naye apate elimu inayoitwa ya juu!!!!

Sio maneno na manyanyaso kwa dada wa watu, amteme akiwa bado anatazamika watu wajitoe muhanga kabla ya lala salama
tatizo laweza kuwa huyo dada hajajua tatizo lake ambalo ni kujikweza. Sasa bahati mbaya alimpata mtu wa kumshusha, so kama hajajitambua na akienda kwa mwingine ni shida. Pia na jamaa nae aliyidisha chumvi
 
Hawa wanandoa wote malimbukeni wa elimu dunia kabisa. Elimu ya darasani haiusiani kabisa na ustaarabu na utashi wa mambo ya mapenzi. Sasa kutokana na ukilaza wao wa elimu dunia lazima hiyo ndoa iwe ya vurumai tu.

PhD+Masters+Bachelor w/out DISCPLINE= STUPIDITY. They need :help: these 2 fools...
 
Mmmm we sio bure ulikua haupendi huyo bibie kuish na mchizi wameishi miaka mitatu maugomvi yote hujaadithia sembuse hili we una ka conflict of interest.
 
Kwa maoni yangu mimi nadhani ni nitabia ya mtu, huyo unaemsema mwenye elimu ya juu angekuwa ameishia darasa la saba lakini ana hela za kufa mtu, kama ana damu ya dharau atakuwa na dharau tu.

Hii inasikitisha ndo maana unakuta mwanamke ana kila kitu kwa mwanaume wake (hela, usafiri, chakula, nguo urembo, kila kitu) lakini anakosa amani bila kusahau mgegedo. maana unaweza kuwa na hela na elimu ya juu lakini kitandani sifuri.

Pole sana dada
 

Kumbe BAKITA nao wamo humu.... safi sana.
 
Exactly.
 
 
Huyo elimu yake haijamsaidia...maana kuna kusoma na kuelimika...nadhanj hajaelimika.....ndo maana mda wote anajisikia na hiyo pHd...kikubwa pesa PHd kitu gani....by the way nina master tena ya abroad na undergraduate ya abroad
 
Kila kina na muogeleaji wake...

wakati mwenzako anakomaa kupata masters na ma-Phd wewe ulikuwa umelala??

Komaa na elimu na wewe uheshimike!

cc rafiki yako
 
Maswala ya elimu na familia hayaingiliani hata kidogo.

Ukiwa ofisini uwe mwanataaluma au onyesha PHD yako huko, ukirudi nyumbani unakuwa baba.

Inabidi tujue na tuweze kutofautisha baadhi ya maswala hasa ndoa, elimu na biashara kwa wakati mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…