Jamani wabunge this is too much.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani wabunge this is too much....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuandamane, Jun 19, 2008.

 1. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Heshima mbele wana JF

  Nimekereka mpaka nimeona ni bora nije mbele yenu ile tujadili hili,

  Bahati nzuri nna kalikizo kadogo na kamenisaidia kuweza kupata muda wa kuangalia bunge moja kwa moja (live), Kinachonikera na wabunge wetu hasa wa CCM ni uzembe na upuuzi wa mambo, wabunge wamekuwa not attentive bungeni na zaidi ya yote naona wanazurura tuu nje ya bunge kana kwamba hawana la kufanya, labda kama kuna mwenye kujua kama hawa wabunge wana ssb za kufanya hivo kinyume na ninachokiona ni uzembe basi anisaidie

  Jana jioni wakati session ya pili imeanza namuona mama Six na J Kapuya wanapiga tuu stori nje.. kama wanataniana vile

  wabunge wengine wakiwa ndani wanapiga tu stori wengine wanasoma magazeti (bahati mbaya aliekuwa akisoma gazeti zikumjua ni nani, ingawa ni mwanaume) leo live MARY NAGU na WAZIRI MKUU... Just imagine WAZIRI MKUU PINDA wamegeukiana kabisa wanapiga michapo kana kwamba hawako bungeni

  J Komba ndo kabisa amekaa back Bench yeye ndo kabisa kageukiana na mwana mama gani anakula sijui nini,

  Mwengine ana soma sms

  Swali: hivi hawa wabunge wanajua walicho kifata hapo?? hili swali nataka alijibu PINDA

  nadhani ni dharau tuu maana hawawezi kuwa wanapuuzia hivi vikao wakati wanajua tuliowachagua tunawaona live

  Oni: Napendekeza uwekwe giant screen pale mbele ili wajione japo wabehave kidogo maana wanaonekana wamesha kuwa masugu

  These guys are not serious at all...........
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hili kweli linakera. Bahati nzuri wanasa video wanawanasa na kuwaonesha watanzania nini wanachofanya wabunge wao!

  Hii nami niliiangalia nikaona kweli wabunge hawako serious! Inasikitisha, Zitto wafahamishe wenzio hii imekaa vibaya!

  Yote haya mimi niliyaona nikabakia kucheka.

  Labda kuna baadhi ya wenzao wanajua hawana points ndo maana hawataki hata kuwasikiliza. Au ndio uwakilishi wenyewe.
  Hapo StarTv wasaidie tuone labda kama inaweza kusaidia.

  Nakuunga mkono katika hili pia. Lakini tusiandamane :)
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Jibu la kwa nini wabunge wengi hawakuweza kuishtukia bajeti feki.
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  LoL,

  You made my day m8!
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Labda Tuandamane tuchukue ushauri wako kuwa tuandamane!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Waturejeshee watu wetu nyumbani tuanze upya.
  Na wao unaweza kuta wamechoshwa na zecomedy...Ama pia labda ni kweli wameamua kutuona wabongo majuha.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mngesikiliza Bungeni leo au kwa wanaoona live natumaini wamejionea upuuuzi mwingine
  wabunge wa chama changu wanasimama na kumpongeza mkulo kwa uozo wa ufeki wa vitabu vya bajeti, halafu mbunge mmoja ndo katoa kali zaidi anamshauri mkulo asikose usingizi na akiweza aendelee kutengeneza watoto (wazembe) asisikilize kelele za wapinzani.

  Nakubaliana na signature ya mwanabodi mwenzetu kuwa IPO SIKU SHETANI ATASEMA ANAONEWA NA WATANZANIA WATAPIGA MAKOFI......

  Naunga mkono hoja ya tuandamane mia kwa mia (wanafiki wasema ndiooooooo)
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Hivi ni possible kwa kitu kama TAIFA KUROGWA?
  Jamani kama kuna mwenye knowledge ya hilo tufahamishane. Yani kama ni possible kwa Taifa kurogwa...Maana licha ya kwamba sijaona hizo video..Lakini maelezo hayo yananipa picha ambayo kwa kweli si vitendo vya kawaida kabisa...Unless ni some sort of SABOTAGE wanayowaonyesha wenzao wa CCM kuwa something has to happen before moving forward.
  Hizo ni option mbili...Kama hiyo ya kutoridhika na mwenendo wa chama si theory nzuri...Then wabunge hao nao hawafai hata kidogo na wananchi wasiwapigie tena kura.
   
 9. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wao wana shida gani na walalhoi? kama ni pesa wakimaliza kikao inaingia sijui ndo posho au mshahara? kama ni dili la epa au richmond tayari zimeshaingia kwenye akaunti. kama ni kukosa kura huo ni wongo kwa kuwa akimaliza tu kipindi chake hayo marupu rupu ataweza kununua wapiga kura kibao! hawa ndugu ni vema hilo jina mnalowaita waheshimiwa mliondoe ili wajisikie kuwa wao ni watu wa kawaida na kuwa jukumu lao ni kutetea watu wa kawaida.HILI JINA MHESHIMIWA LINANICHEFUA SANA, HUKO VIJINI UTASIKIA HATA MWENYEKITI WA KIJIJI ANAJIITA MHESHIMIWA, SIJU WANAHESHIMIWA KWA LIPI? KWA NJAA INAYOWAMALIZA WAPIGA KURA WAO?
   
 10. M

  Mabula Member

  #10
  Jun 19, 2008
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  our reps most of the time are not serious in the house!the story is different when it come to receiving their perdiums.ndiyo aina ya watu tulionao
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Naam, nimeiona hiyo mkuu. Ila nikukosoe kidogo, mbunge alisema Mkullo alale usingizi mnono asiwasikilize wapinzani na kelele zao ila spika akamkatisha akamwambia "Mheshimiwa akilala sana hatatengeneza watoto...". Kes kauli hiyo nilijikuta nabadili channel hapohapo!
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahahahaha hehehehe
  ah makubwa haya
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Ni wazi kuwa BUNGE LETU NI LA CCM na CCM IMEGAWANYIKA TAYARI KIMAKUNDI MAKUNDI.
  Tatizo ni mgawanyiko huo hautamnufaisha mwananchi huko bungeni na kwa hiyo waturudishie watu nyumbani tuanze upya. Huo ni ushauri wangu mwema.
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu Spika mawazo yake yote yapo kwenye hilo tendo tu.Nakumbuka hata Mama Kilango alishawahi kumpa kibomba kuhu kukosa sehemu ya kulala baada ya kusema atakuwa a staunch critic wa iuovu hata kama utatoka kwa mumewe.

  Freud would say he is dominated by ever present sexual desires in an attempt to use the most of a waning libido.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wanachonikera zaidi ni pale mtu anapopewa mda anaanza siju nampongeza.....sijui juzi....
  Mbaya zaidi utakuta wabunge zaidi ya watano wote wanaongea kile kile ktk opening remarks zao.
  Then at the end kapoint kamoja alafu pumba ili mradi tuu auze sula.Hopeless
  Mtu aliyeingia bungeni kisanii utamuona tuu.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pundit unachosema sikatai.
  Ila usisahau kuna mgawanyiko ama migawanyiko kede kede huko CCM.
  Kabla hawajaanza kuuana live live warudi nyumbani.
  Sitta..."Mzee wa Maji Taka" Ni mwanasiasa mkongwe mwenye vijembe.
  Hiyo ilikuwa ni kauli ya kijembe kwasababu ni wazi alimaanisha kuwa watu wasilale.
  Watoto inaweza kuwa MAJI TAKA TU.
  Ama pia kuwa wasilale...In any means hata kama kutengeneza watoto ndio sababu ya kuwafanya wawe macho.

  NCHI IKO NJIA PANDA HALAFU KUNA WANAOSEMA WATU WALALE?
  HAPA MIMI NAMASAPOTI SITTA KWANI HAO WABUNGE NI KWELI HUWA HAWALALI KWA NGONO!
  HALAFU MASLAHI YA TAIFA YAKIFIKA BASI WANAJIDAI KULALA...SOMETIMES HATA BUNGENI HUSINZIA KWA MUSHKELI WA USIKU ULIOPITA WA LIBENEKE.
   
 17. M

  Masaka JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mwenye uamuzi wa kurudisha watu nyumbani ni nani? na kama yupo ila hataki kurudisha watu nyumbani kabla ya 2010 je nini kitafanyika?
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hivi zile allowance waliongezewa vile?

  yote ulosema ni kweli tupu, unajua 'mtoto umleavyo ndivyo akuavyo', sasa imagine hapo kuna wengine wana majukumu ya kukemea nidhamu na utoro mashuleni, vyuoni, makazini nk... wakati huo huo wao wanashindwa kuonyesha hilo hapo bungeni!

  No wonder nidhamu makazini 'hairidhishi' iwapo mawaziri wenyewe ndio hivyo.
   
 19. J

  Jobo JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu Speaker akili yake naye huwa ni mbovu! Ana utani sana ndo maana hata anadiriki kusema kuna uchawi bungeni wakati sheria zetu hazitambui uchawi.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,597
  Likes Received: 1,998
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone kama Sitta ni mkweli.
  Kumbuka alisema tusubiri BUNGE kuhusu mambo ya ufisadi.
  Na hilo lilimshtua sana Chenge hadi akatamani BUNGE LISIWEPO ama kujaribu vitisho.
  Sitta alilonga hayo Huko jimboni Maiyore or something huko India.
  Pia ni kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na kina Zitto..Basi tusubiri tuone.
  Maana hata Rais mwenyewe anajua wananchi wengi wa kawaida wana hasira.
   
Loading...