Jamani mnalikumbuka hili!.

Kumekucha (Kumekucha jamaa kumekucha, hata majogoo vijijini yana wikaaa na jua mbinguni limetoa (hapa kidogo nahisi kama nimichapia) na majembe mabegani tukafanye kazi sasaaa oh oh sasaaa tusonge mbele... (malizia).

Inueni moyo: (Tumshukuruuu mungu weeetu aliyetujlia imani hii siku za kale na siku hizi...)

Malenga wetu: (hapa ni mashairi kwa kwenda mbele).

Out and About (external service) Kipindi kilikuwa kinaanza saa sita mchana.

Mikingamo (mikingamo ni sauti ya umma kwa hiyo tuambie wako wapi na ni kina nani na wanafanya nini kuendelea rushwa magendo kuaharibu mali za umma, na kikingamo kitasema wazi...)

Club raha Leo ( kilitumika kualika wafanyakazi kwenda studio na kupigiwa muziki live (sometimes)

Wakati wa Kazi (watangazaji walikuwa wakitembelea viwanda na maofisi mbali mbali na kuwahoji wafanyakazi na kuwapatia nafasi za kutuma salam na kuchagua nyimbo)

Kipindi cha wagonjwa (watangazaji walikuwa wakitembelea wagonjwa mahospitalini kuwajulia hali na kuwapatia nafasi za kutuma salam na kuchagua nyimbo).

Lala salama (kipindi cha salamu za usiku na nyimbo laini)

Hadithi na Nyimbo
(Kipindi cha muziki lakini kwa mtindo wa hadithi na simulizi)

Lakini enzi hizo ilikuwa safi sana, vipindi vilikuwa vinaelimisha kwa njia moja au nyingine. Sina uhakika kama siku hizi ile michezo ya redio na zile hadithi za watoto kama bado zinaendelezwa au ndio zisha zikwa...!
 
1.kahawa ni mali
2.ugua pole
3.karibu mgeni
4.misakato
5.mambo mpwito mpwito

Naam,Mambo ya watu wazima haya.
 
wakuu mnakumbuka maigizo ya Mzee Jangala usiku saa tatu???, never miss.
enzi hizo kwanza mwasikiliza wadhamini CHIBUKU!!, ..chibuku oyeee, chibukuuu hongera hongeraa hongeraaa...!, duh.
 
Bila kusahau ANA KWA ANA na kile kipindi cha mashairi!!
From me to you ..hiki kipindi kilikuwa kinatayarishwa na Maria Ulimwengu kama sijakosea!!
 
Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
5. .................na Chuo cha uongozi wa maendeleo Mzumbe
 
Kuna kipindi kilikuwa kinaanza na wimbo wa ..tujengeee tujengeee tujenge na mwananchi engneering contractor..watu shule wakawa wanaimba tujenge na mwananchi chini ya likomtata
 
Kuna kipindi kilikuwa kinaanza na wimbo wa ..tujengeee tujengeee tujenge na mwananchi engneering contractor..watu shule wakawa wanaimba tujenge na mwananchi chini ya likomtata

Mdogo wangu na mtoto wa Sister walikuwa Arusha. Na waliporudi huku Sikonge wakawa wanaimba "Kijenge Kijenge cha kokwaa..." Tukawa tunafahamu kuwa ni wimbo waliokuwa wakiimba wakati wako Arusha na kwa kufahamu kuwa Arusha kuna Kijenge.

Siku moja ikabidi tuende kumuuliza mama maana ya wimbo. Nilicheka kuja kufahamu kuwa walikuwa wakiimba kivyao, ila wimbo hasa ni "Tujenge, tujenge, tujenge pamoja.... Siasa za ujamaa/Mwalimu kasema...". Asante mkuu kwa kunikumbusha tena.
 
Aaah mi ile instrument ya kipindi cha michezo ilikuwa inaniacha hoi sana,na kipindi cha pole kwa kazi!!
 
mazungumzo baada ya habari sijui ilianza mwaka gani. . .
Nadhani kilianza wakati ule TANU bado ipo madarakani na mara nyingi yale masimulizi yalikuwa kwenye vitabu vilivyokuwa vikijulikana kwa jina la DARUBINI. (mambo ya ujamaa) Kama bado nakumbuka vizuri.
 
Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
Nakwambia ilikuwa shughuli haswa, mwenye kukumbuka vinginvyo aongezee.

Hii niliirushaga michizi blog sometimes 2008 watu wakilumbuka mbali sana
(link hii hapa kwa comments jamaa walizotoa http://issamichuzi.blogspot.com/2008/11/vipindi-vya-rtd-unavikumbuka.html)

Vipindi Vya RTD Unavikumbuka??
Wadau leo nimeona nije na hii nyingine, nimekumbuka sana ile miaka ya nyuma kidogo wakati tulikuwa hatuna radio stations nyingi kama zilivyo sasa, wakati huo station ilikuwa ni Radio Tanzania tu na ile idhaa yake ya kiingereza (External).
Fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.
"Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.
"Starehe na BP " - Uncle J. (Julius Nyaisanga) alikuwa anakimudu vyema kabisa""Kahawa ni Mali" - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.
"Jifunze Kiswahili Fasaha" - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..
"TTCL Simu kwa Maendeleo" kipindi cha "Serikali za Mitaa", " Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba na kundi lake wakati ule.
Ukija vipindi vya week ends kama "Club Raha leo Show", bila kusahau kipindi cha "Mama na Mwana" namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k wadau ongezeeni hapo kumbukumbu zenu.
Japokuwa kilikuwa ni kipindi cha watoto lakini nakumbuka watu wazima walikuwa wanazifuatilia kwa umakini sana zile hadithi bila kukosa sehemu hata moja juma moja baada ya lingine.
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.

Je, wewe mdau unakumbuka nini miaka hiyo hapo kunako Radio Tanzania (RTD)???
Mdau yule yule wa Dodoma,
Natanguliza shukrani Bro Michu

© Michuzi | Friday, November 14, 2008 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |


Maoni: 92


Tarehe Fri Nov 14, 02:32:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hapo mdau kasahau asubuhi tunaamka na MAJIRA. tunapata habari toka kwa wawakilishi mikoani. Kuna kipindi nilikuwa nakichukia sana kwa sababu kikianza tu nasikia njaa MALENGA WETU. Vipindi vingine kama JENGA NA MECCO,TAIRI GENERAL na marehemu bati kombwa, Kipindi cha Michezo saa mbili kasorobo. YOTE TISA KUNA KIPINDI NAKIMISI SANA. 'MUZIKI NA HISIA' Kipindi hiki kilinivutia sana. Wadau lete vipindi vingine

Tarehe Fri Nov 14, 03:24:00 AM, Mtoa Maoni: Mkazi Wa Makojo, Mara

Ilikuwa myeyusho tu, sisi kwetu tulikuwa tunapata mawimbi ya sauti ya Kenya kuliko RTD na kipindi alichokipenda sana mama yangu ni 'JE HUU NI UUNGWANA?'NA MAMBO MBOTELA!

Tarehe Fri Nov 14, 03:30:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Mie naukumbuka ule wimbo wa mzee Makongoro akiwaonya madereva wasinywe kileo kama gongo na kuendesha. 'Ati dereva kalewa gongo ah! sawa hiyo?!' Halafu wengine wanabwakiza 'haata hiyo si sawa dereva acha vitukoo!!. Wimbo huu ulitungwa kufuatia hotuba ya mwalimu Nyerere akiwaonya madereva kuwa wastaarabu barabarani. Hiyo ndiyo ilikuwa miaka ya chama kimoja chenye uongozi thabiti wa Taifa.

Tarehe Fri Nov 14, 03:31:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Duu hapo umasahau kulikuwa na mchana mwema, wahenga wetu,wakati wa kazi, mazungumzo baada habari, mambo mpwitompwito,pwagu na pwaguzi,kumakucha jamani kumekucha,from me to you, dial a disc,majira na zengine kibao nipe muda nitakulretea.

Tarehe Fri Nov 14, 03:51:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Mdau kuna na hivi vifuatavyo:
Kijaluba, Kipindi cha Mashairi
Pwagu na Pwaguzi.
Bila kusahau kipindi ambacho kwa sasa hivi kingekuwa na kazi ya ziada cha Mikingamo. "Ndugu fulani wa jiji fulani akishirikiana na fulani walikwiba pesa za umma na kuzificha kwenye kisiwa fulani!"

Tarehe Fri Nov 14, 04:02:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Duuuuh mdau wa dodoma umenikumbusha mbali sana na kipindi cha hadithi ''KISA CHA MFALME JUHA'' kwani nilikuwa sikikosi hata kidogo zile hadithi nakumbuka niliachwa na treni kwenda Dodoma kwa kumalizia kipindi ikabidi nisafiri siku nyingine. Kweli ya kale Matamu

Tarehe Fri Nov 14, 04:14:00 AM, Mtoa Maoni: Halikuniki

Mdau kipindi cha mama na mwana hapo zamani kilikuwa kinaendeshwa na DEBORAH MWENDA!Wakati huo hadithi ya Binti chura na Ua jekundu zinatukusanya pembeni mwa redio kuanzia saa 8 mchana.

Any way.. kila mtu na zamani yake, hata mtoto wa mwaka mmoja nae ana zamani yake!


Binafsi nakumbuka kipindi cha Mzee jangala cha usiku, kilikuwa kinadhaminiwa na "CHIBUKU"

Zaidi ya yote kipindi cha jumapili salamu za wagonjwa hospitalini. Kiashiria ni wimbo wenye ujumbe mzito " ..Ajue bwana mungu wa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama..."

Mwisho sikisahau kipindi cha majira asubuhi saa 12.30 kilikuwa kinanikera sana sababu ndo mida ya kuwahi namba shuleni (shule ya msingi Tandale Dar.), viranja wanoko na mwaalimu wa zamu balaa ukichelewa namba. Huku nimebeba dumu la maji ya kumwagilia bustani za shule, huku ufagio wakufagilia, huku kifuu cha kupikia uji wa shule, huku nimebeba madaftar, huku michongoma sijui yakueka kwenye uzio, huku kikombe cha uji..dah kama askari anaenda vitani!

Ah imebaki historia wala haijirudii tena...!

Tarehe Fri Nov 14, 04:17:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

(Ugua poe )JUMAPILI.wakati umewadia wasalamu kwawagonjwa hosipitalini leo tunawapa pole.....
Mikingamo.Asiria salam.Malenga wetu,Jumanne kibao.Tumbu
 
Idhaa ya biashara ilikuwa na kajingo...PHILIPS ndiyo yenyewe! Sauti safi sauti kubwa!
Umenikumbusha tangazo moja la Benki ya Biashara enzi hizo ilikuwa sauti ya mwanamke akilalamika ameibiwa:

Jamaniiii weziii... weziii haooo....Haoooo wamekimbiaaa... Wameniibia kila kitu pamoja na kasha langu la pesa ah! Epukana na hasara ya namna hii kwa kuweka pesa zako kwenye benki ya biashara... (Hii kipande ya mwisho sina uhakika sana)
 
Huu wimbo kama sikosei ulikuwa ukipigwa kwenye kipindi cha TUMWABUDU MUNGU. Nilihangaika sana kuupata maana sikufahamu nani mtunzi. Siku moja niliangalia film moja inayohusu Dr mmoja huko Congo wakati wa vita ya II ya dunia. Jamaa alikuwa Mgeruman na maadamu walipigwa, basi na yeye alifukuzwa. Kabla ya kuondoka, walionyesha amekaa kwenye kinanda na anapiga huu wimbo/mziki wa Johann Sebastian Bach.

http://www.youtube.com/watch?v=0SVuHV7suhQ

Mkuu nashukuru sana kwa kutatua kitendawili changu cha siku nyingi.
Hii ala mimi pia naipenda sana na huwa inakumbusha mbali sana kwani
nilikuwa nasikiliza sana hichi kipindi kutokana na ule muda wake (saa nane /saa tisa alasiri) mara nyingi nilikuwa nakuwa nimepumzika nikiwa nimeshatoka kanisani na nimemaliza tu kupata lunch najinyoosha nikisikiliza kipindi hiki siku ya Jpili.

Mkuu kuna ule mwingine pia wa kipindi ambacho huwa kinafuatana na hiki nafikiri huwa kinaitwa BIBLIA YATWAMBIA NINI kama sikosei ama NYIMBO ZA INJILI huwa nacho ni saa nane na nusu ama saa tisa alasiri.

Nilishaga zitafuta sana mpaka nikasema nitakuja piga simu TBC1 niwaulize siku moja lakini sikuwahi fanya hivyo.

Thanks mkuu post na ule mwingine pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom