Jamani mnalikumbuka hili!.

Yegomasika

JF-Expert Member
Mar 21, 2009
13,164
61,249
Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
Nakwambia ilikuwa shughuli haswa, mwenye kukumbuka vinginvyo aongezee.
 
Dah mkuu kweli umenikumbusha mbali enzi za vipindi km jioni njema, ila kinachonikuna ni kile cha michezo mbili kasoro bana home kwetu ilikuwa msosi wa jioni twala au unapakuliwa kuanzia mbili kamili basi mmetoka zenu wazee kucheza mpira ile njaa inauma mmekaa sebuleni ikifika mbili kasoro ikianza kale ka mziki basi mioyo inainuka mnajua sasa time imewadia. kuna mazungumzo baada ya habari, jpili kipindi cha salamu kwa wagonjwa, mama na mwana, habari na muziki, tehe kweli tumetoka mbali
 
Mama na mwana, kwa ambao kipindi tulikuwa watoto.
Michezo ya kuigiza pwagu na pwaguza, mzee jongo na bi nyakomba.:lol:
 
Chei Chei Shangazi

"Kitendawili, tega".

Kijaruba, hahaaaa Abdallah Mlawa aka mr Kijaluba.

From me to you.....hapo unasikia soul music si mchezo.

Siku ya Idd, wanapiga "Mpenzi wangu ninakupa, mkno wa Idd - by Sallum Abdallah".

Zilipendwa. Mhhhh, mchezo wa redio. Mie niliishia ule wa wale watoto walienda kutafuta maji ya uzima ili baba yao apone.
 
Chei Chei Shangazi

"Kitendawili, tega".

Kijaruba, hahaaaa Abdallah Mlawa aka mr Kijaluba.

From me to you.....hapo unasikia soul music si mchezo.

Siku ya Idd, wanapiga "Mpenzi wangu ninakupa, mkno wa Idd - by Sallum Abdallah".

Zilipendwa. Mhhhh, mchezo wa redio. Mie niliishia ule wa wale watoto walienda kutafuta maji ya uzima ili baba yao apone.
Du unakumbuka bado majina ya michezo ya radio, from me to you ilikuwa inarushwa na External service, hivi jamani hii station bado ipo?.
 
Huu wimbo kama sikosei ulikuwa ukipigwa kwenye kipindi cha TUMWABUDU MUNGU. Nilihangaika sana kuupata maana sikufahamu nani mtunzi. Siku moja niliangalia film moja inayohusu Dr mmoja huko Congo wakati wa vita ya II ya dunia. Jamaa alikuwa Mgeruman na maadamu walipigwa, basi na yeye alifukuzwa. Kabla ya kuondoka, walionyesha amekaa kwenye kinanda na anapiga huu wimbo/mziki wa Johann Sebastian Bach.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=0SVuHV7suhQ[/ame]
 
Bila kusahau tumbuizo asilia....captain wake akiwa uncle J nyaisanga.

Utamsikia akisema haooo mwanakuja sasa waluguru...anaachia ngoma
yao kidogo then utamsikia akisema aahh waluguru acheni hasira njooni pole pole
then anaachia ngoma sasa.


hahahahhahh...
 
Kulikua na kipindi cha Mkulima wa kisasa na ule wimbo wake wa kuanzia kipindi, mkoa kwa mkoa, na kile kipindi cha asubuhi ikiwa ndio inafunguliwa saa kumi na moja alfajiri cha Inueni Mioyo, Mgeni wetu na kipindi cha michezo na ule wimbo wake
 
kulikuwa na kipindi cha matukio ambacho kilikuwa siku ya jumapili na jumatatu shule nilikuwa sikipendi kipindi hiki kwani kilikuwa chanikumbusha kesho shule. Uncle J. Nyaisanga na kipindi cha misakato humo kulikuwa kunapigwa nyimbo mpya za DDC mlimani park, tomatoma, Uda jazz, Juwata Jazz, Orchestra makasy na nyingine nyingi huku akikutajia wanamuziki husika katika bendi. marehemu Michael Katembo alikuwa na vichekesho katika kipindi hicho, kipindi cha mikingamo wakati wa uhujumu uchumi nilikuja kusikia kuwa kilitumika kubigana majungu, halafu kulikuwa na kipindi kilicho kuwa kinaendeshwa na mkurugenzi Mzee David Wakati. halafu kulikua na external service huko ndo kulikuwa na nyimbo za kizungu na kilikuwa chaendeshwa kwa ung'eng'e. na nikikumbuka watangazaji kama akina Sekioni Kitojo, Ahmed Jongo, Charles Hilary, Abisai Steven Ben Kiko (huyu alivuma sana wakati wa vita vya uganda na taarifa za vita watu walikukwa wakikusanyika redioni kusikilliza anatoa habari gani) Mambo ya zamani wakati mwingine yanaleta burudani kwa kweli. Si vibaya tukikumbuka katuni za chakubanga na company yake ya akina chupaki.
 
Ndugu, kuna kipindi cha KOMBORA alfajiri saa kumi na moja. E bwana ee nilikuwa nikisikia tu kipindi hiki moyo unaanza kwenda mbio. Maana naogopa kibaridi cha kule kwetu na wakati huo kipindi kinanikumbusha kuwa kumekucha inabidi niamke kwenda shule. Ukifikiria baridi iliyopo na mwalimu wa zamu ni mkali si mchezo . Henzi hizo waalimu wanapitia JKT ni wachungu mno. DU! ee BWANA EE. Si mchezo.
 
Na zile saa za taarifa ya habari midundo ya ngooma kabla habari haijasomwa
na matangazo ya vifo na kimlio chake
 
Bila kusahau tumbuizo asilia....captain wake akiwa uncle J nyaisanga.

Utamsikia akisema haooo mwanakuja sasa waluguru...anaachia ngoma
yao kidogo then utamsikia akisema aahh waluguru acheni hasira njooni pole pole
then anaachia ngoma sasa.


hahahahhahh...

Mkuu hicho mwenyewe alikua Michael Katembo,ila baadae alikua anasema Katembo usijesema ni mdogo kihivyo bali ni jitembo haswa,...haaa
Kwa wale tulosoma mikoani ukitoka shule ile mida ya sita unusu kuwahi msosi m kisha urudi kwa shule unafika home unakutana na MALENGA wetu,.dah njaa inauma zaidi ,...lol
 
daaaa....mkuu umenikumbusha enzi hizo nipo kijijini kwetu na Redio yangu ya minga. Mimi nilipenda vipindi vya Tuimbe sote enzi ya komba akiwa kijana. tumbuizo asilia, wapi MARIMA NDELEMA? Yupo kweli!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom