Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Serikali yababaika
TUHUMA DHIDI YA CHENGE
na Salehe Mohamed, Dodoma na Kulwa Karedia Da
TUHUMA zinazomkabili Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, anayedaiwa kukutwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja katika akaunti zinazochunguzwa iwapo zina uhusiano wowote na ununuzi wa rada nchini Uingereza mwaka 2002, zinaonekana kuilemea serikali.
Siku moja tu baada ya Chenge mwenyewe kutoa kauli akieleza kushtushwa na tuhuma hizo ambazo aliziita za kuumbiwa na zinazotokana na chuki binafsi, viongozi serikalini wenye dhamana ya masuala ya utawala bora, usalama na uhalifu wameanza kutoa taarifa zinazokinzana.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Sophia Simba, alisema serikali ilikuwa bado haijaanza kumfanyia uchunguzi Chenge na kwamba suala hilo lilikuwa likishughulikiwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini Uingereza ya SFO.
Waziri Simba alisema maofisa wa SFO walifika hapa nchini na kuomba nyaraka na taarifa zote zinazomhusu Chenge na wakazichukua na kurudi kwao ambako wanaendelea na uchunguzi wao.
Aidha, waziri huyo alishindwa kueleza kama serikali ilikuwa imechukua hatua zozote kuchunguza iwapo waziri huyo aliyerejesha nchini juzi akitokea China alikuwa amewasilisha taarifa za kuwa na akaunti ya fedha katika Kisiwa cha Jersey katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi..
Waziri Simba, alieleza kuwa, kwa sasa serikali inajikita katika kuandaa utaratibu ambao utaiwezesha kupata fedha ambazo zilitozwa zaidi kuliko gharama halisi ya rada hiyo, iliyonunuliwa mwaka 2002.
Wale (SFO) ndio wamekuja kutaka mafaili na taarifa kuhusu Chenge na wakapewa halafu wameondoka kwenda kufanya uchunguzi wao, sasa sisi hatuna cha kufanya zaidi ya kusubiri matokeo, alisema Simba.
Alisema serikali haimtuhumu Chenge kwa kumiliki akaunti yenye fedha nyingi kiasi hicho, bali wale wenye kujua mambo hayo ndio watakaokuwa na jukumu la kufanya uchunguzi husika.
Alisema kifungu cha 6(i) cha Sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, kinabainisha wazi kuwa Kamishna wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi anayo mamlaka ya kuruhusu kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kiongozi wa umma.
Alisema kutokana na sheria hiyo, kamishna aliwaruhusu wataalamu wa SFO kuchukua taarifa kuhusu Waziri Chenge, jambo ambalo mtu yeyote anaweza kulifanya kama kamishna atakubaliana na sababu alizozitoa.
Waziri huyo ambaye hivi karibuni alikaririwa na gazeti moja akionyesha mshtuko wa wazi dhidi ya tuhuma hizo za Chenge hata kufikia hatua ya kuhoji pengine alizipata kwa kuuza ngombe wake, alisema taarifa za Chenge kumiliki kiasi kikubwa cha fedha wamezipata kupitia vyombo vya habari.
Sisi tuna taratibu za kufanya kazi na kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili watumishi wa umma. Hatuwezi kufanya uchunguzi wa kila taarifa inayotolewa na vyombo vya habari, alisema Simba.
Alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete alishaweka bayana msimamo wa Tanzania kuhusu suala la ununuzi wa rada ya kijeshi iliyonunuliwa kwa paundi za Uingereza milioni 28.
Alisema kama kuna tatizo lolote kwa mtumishi wa umma kuhusishwa katika tuhuma za rushwa, serikali itaangalia cha kufanya baada ya kupata taarifa za uhakika, baada ya uchunguzi kufanyika.
Kama kuna ulazima wa kufanya uchunguzi kuhusu kiongozi wetu, tutaufanya, lakini si kwa shinikizo kutoka sehemu fulani au kwa sababu ya maneno ya watu, alisema Simba.
Wakati Waziri Simba akitoa majibu hayo, Jeshi la Polisi limebainisha kuwa, haliwezi kufanya uchunguzi hivi sasa dhidi ya waziri huyo kwa sababu hadi hivi sasa halijapokea taarifa zozote kutoka serikalini, zinazolitaka kumchunguza.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alisema ofisi yake haijapokea taarifa yoyote rasmi ya maandishi kutoka ngazi za juu kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi Waziri Chenge.
Kwa kweli suala hili nimelisoma kwenye magazeti tu naomba tuwe na subira, alisema DCI Manumba katika mahojiano na gazeti hili jana.
Alisema kama ofisi yake ikipokea taarifa ya kumfanyia uchunguzi Chenge, haitasita kufanya hivyo kwa vile kazi yake kubwa ni kushughulikia matatizo kama hayo.
Tutafika hata huko anakodaiwa kuweka fedha hizo kuchunguza, kwa vile hivi sasa kuna njia nyingi za mawasiliano, alisema Manumba.
Hata hivyo, alisema kulingana na aina ya suala lenyewe, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndiyo yenye dhamana kubwa ya kuendesha uchunguzi.
DCI, ambaye hakutaka kuingia kiundani juu ya suala hilo, alisema taasisi nyingi za serikali zimegawana majukumu kwa mujibu wa sheria.
Wenzetu wa TAKUKURU naamini hivi sasa wako katika nafasi nzuri zaidi ya kulizungumzia hili, mimi hapa nakupa tu hali ilivyo ya mgawanyiko wa majukumu yetu, alisema.
Tanzania Daima haikuweza kuwasiliana na TAKUKURU kutokana na ukweli kwamba, iwapo ingekiri kumchunguza waziri huyo basi sheria ingelizuia gazeti hili kuandika taarifa hizo.
Jumamosi ya wiki iliyopita, gazeti linaloheshimika nchini Uingereza, la The Guardian liliandika kuwa katika uchunguzi huo wa SFO iligundulika akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja katika akaunti moja, katika Kisiwa cha Jersey.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, SFO inamchukulia Chenge kuwa mtu anayeweza akawa shahidi muhimu katika uchunguzi mzima wa zabuni ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE ya nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, SFO inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28, ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, inaaminika kwamba, uchunguzi huo wa SFO unatarajiwa kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.
Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Waziri Chenge zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey zina uhusiano wowote na zile zilizotoka katika Kampuni ya BAE System inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada hiyo kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.
The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, linaripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo, alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.
Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa, alisema mwanasheria huyo wa Chenge.
Hata hivyo, gazeti hilo liliandika kuwa uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa.
Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.
Akizungumza baada ya kurejea nchini juzi, Waziri Chenge aliwataka wananchi kuwa na subira kuhusu uchunguzi huo na kile alichokiita vijisenti ambavyo vinatakiwa kujulikana vilipatikanaje.
Alikiri kwamba tuhuma hizo dhidi yake ni nzito na zilizomshtua, na akakataa kuelezea chochote kwa undani kuhusu kuwa na fedha hizo au njia alizozipata, na iwapo kulikuwa na uhusiano wowote kati ya tuhuma hizo na kashfa ya ununuzi wa rada ya kijeshi.
Hata hivyo alisema amekuwa kiongozi serikalini kwa muda mrefu, akishika nyadhifa tofauti, akiwa ameshika nafasi ya Uanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka 10, hivyo fedha alizokuwa akilipwa zilikuwa halali.
Tuhuma za ufisadi dhidi yangu ni nzito mno inabidi nipate muda wa kukaa na kutafakari kwanza, na ukweli wa mambo utajulikana baada ya vyombo vya dola vilivyopewa kazi ya kunichunguza kumaliza kazi yake na hapo nitakuwa na muda wa kujibu, alisema Chenge juzi.
Source: Tanzania Daima
aliyo guku oyaga gete ituja ya ntuzu!ulindoshi sana guku!i bariadi a banhu balilya milenda na bugali ubebe bilion moja ulihaya vijisenti aliyo ulindoshi sana!