Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
How in the shag can a minister who is responsible for good governance and indirectly supervision of TISS utter such childish, nusery school responses?
How can our government be sound asleep when sensitive matters are at stake?
Inashangaza sana majibu ya Sophia Simba na Manumba kushangaa matokeo ya kuchunguzwa Chenge na SFO!
Inatia aibu kuwa wakati SFO walipokuja na kutoa rasmi tamko kuwa tunamchunguza Chenge, si Rais, Mawaziri, Polisi au Usalama walioshtuka na kuanza kazi kupeleleza inakuwaje aliyekuwa Mwanasheria Mkuu ambay ni Waziri katika Serikali na mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM anachunguzwa kwa tuhuma za Rushwa na Serikali ya Uingereza?
Can anyone with right mind respond to that?
This is what Simba stated as qouted by Tanzania Daima
Naye Manumba anatoa hoja kama hii, eti anasubiri amri kuzima moto..
This is crap, and Watanzania tumetukanwa na viongozi wetu!
How can our government be sound asleep when sensitive matters are at stake?
Inashangaza sana majibu ya Sophia Simba na Manumba kushangaa matokeo ya kuchunguzwa Chenge na SFO!
Inatia aibu kuwa wakati SFO walipokuja na kutoa rasmi tamko kuwa tunamchunguza Chenge, si Rais, Mawaziri, Polisi au Usalama walioshtuka na kuanza kazi kupeleleza inakuwaje aliyekuwa Mwanasheria Mkuu ambay ni Waziri katika Serikali na mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM anachunguzwa kwa tuhuma za Rushwa na Serikali ya Uingereza?
Can anyone with right mind respond to that?
This is what Simba stated as qouted by Tanzania Daima
Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Sophia Simba, alisema serikali ilikuwa bado haijaanza kumfanyia uchunguzi Chenge na kwamba suala hilo lilikuwa likishughulikiwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini Uingereza ya SFO.
Waziri Simba alisema maofisa wa SFO walifika hapa nchini na kuomba nyaraka na taarifa zote zinazomhusu Chenge na wakazichukua na kurudi kwao ambako wanaendelea na uchunguzi wao.
Aidha, waziri huyo alishindwa kueleza kama serikali ilikuwa imechukua hatua zozote kuchunguza iwapo waziri huyo aliyerejesha nchini juzi akitokea China alikuwa amewasilisha taarifa za kuwa na akaunti ya fedha katika Kisiwa cha Jersey katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi..
Waziri Simba, alieleza kuwa, kwa sasa serikali inajikita katika kuandaa utaratibu ambao utaiwezesha kupata fedha ambazo zilitozwa zaidi kuliko gharama halisi ya rada hiyo, iliyonunuliwa mwaka 2002.
Wale (SFO) ndio wamekuja kutaka mafaili na taarifa kuhusu Chenge na wakapewa halafu wameondoka kwenda kufanya uchunguzi wao, sasa sisi hatuna cha kufanya zaidi ya kusubiri matokeo, alisema Simba.
Alisema serikali haimtuhumu Chenge kwa kumiliki akaunti yenye fedha nyingi kiasi hicho, bali wale wenye kujua mambo hayo ndio watakaokuwa na jukumu la kufanya uchunguzi husika.
Alisema kifungu cha 6(i) cha Sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, kinabainisha wazi kuwa Kamishna wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi anayo mamlaka ya kuruhusu kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kiongozi wa umma.
Alisema kutokana na sheria hiyo, kamishna aliwaruhusu wataalamu wa SFO kuchukua taarifa kuhusu Waziri Chenge, jambo ambalo mtu yeyote anaweza kulifanya kama kamishna atakubaliana na sababu alizozitoa.
Waziri huyo ambaye hivi karibuni alikaririwa na gazeti moja akionyesha mshtuko wa wazi dhidi ya tuhuma hizo za Chenge hata kufikia hatua ya kuhoji pengine alizipata kwa kuuza ngombe wake, alisema taarifa za Chenge kumiliki kiasi kikubwa cha fedha wamezipata kupitia vyombo vya habari.
Sisi tuna taratibu za kufanya kazi na kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili watumishi wa umma. Hatuwezi kufanya uchunguzi wa kila taarifa inayotolewa na vyombo vya habari, alisema Simba.
Alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete alishaweka bayana msimamo wa Tanzania kuhusu suala la ununuzi wa rada ya kijeshi iliyonunuliwa kwa paundi za Uingereza milioni 28.
Alisema kama kuna tatizo lolote kwa mtumishi wa umma kuhusishwa katika tuhuma za rushwa, serikali itaangalia cha kufanya baada ya kupata taarifa za uhakika, baada ya uchunguzi kufanyika. Kama kuna ulazima wa kufanya uchunguzi kuhusu kiongozi wetu, tutaufanya, lakini si kwa shinikizo kutoka sehemu fulani au kwa sababu ya maneno ya watu, alisema Simba.
Naye Manumba anatoa hoja kama hii, eti anasubiri amri kuzima moto..
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alisema ofisi yake haijapokea taarifa yoyote rasmi ya maandishi kutoka ngazi za juu kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi Waziri Chenge.
Kwa kweli suala hili nimelisoma kwenye magazeti tu naomba tuwe na subira, alisema DCI Manumba katika mahojiano na gazeti hili jana.
Alisema kama ofisi yake ikipokea taarifa ya kumfanyia uchunguzi Chenge, haitasita kufanya hivyo kwa vile kazi yake kubwa ni kushughulikia matatizo kama hayo.
Tutafika hata huko anakodaiwa kuweka fedha hizo kuchunguza, kwa vile hivi sasa kuna njia nyingi za mawasiliano, alisema Manumba.
Hata hivyo, alisema kulingana na aina ya suala lenyewe, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndiyo yenye dhamana kubwa ya kuendesha uchunguzi.
DCI, ambaye hakutaka kuingia kiundani juu ya suala hilo, alisema taasisi nyingi za serikali zimegawana majukumu kwa mujibu wa sheria. Wenzetu wa TAKUKURU naamini hivi sasa wako katika nafasi nzuri zaidi ya kulizungumzia hili, mimi hapa nakupa tu hali ilivyo ya mgawanyiko wa majukumu yetu, alisema
This is crap, and Watanzania tumetukanwa na viongozi wetu!