DOKEZO Responded Mpimbwe, Katavi: Inakuwaje DMO anayechunguzwa kwa ufisadi na matumizi mabaya ya nafasi, anahamishwa kimyakimya?

DOKEZO Responded Mpimbwe, Katavi: Inakuwaje DMO anayechunguzwa kwa ufisadi na matumizi mabaya ya nafasi, anahamishwa kimyakimya?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hali ya sintofahamu imezidi kutanda ndani ya Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi baada ya aliyekuwa DMO kutajwa kuhamishwa ghafla kutoka Halmashauri ya Mpimbwe kufuatia tuhuma nzito za ukusanyaji wa fedha za vituo vya kutolea huduma za afya zinazodaiwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 60, ambapo fedha hizo alidai ameagizwa na Mkurugenzi kwa ajili ya matumizi ya ujio wa Mwenge tarehe 27/09/2025, jambo ambalo si kweli.

Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka miongoni mwa watumishi wa halmashauri hiyo, fedha hizo zinadaiwa kukusanywa kwa utaratibu wenye utata.

Kila incharge wa kituo ambacho kina mapato makubwa alipewa maelekezo ya kutoa pesa mbichi nje ya mfumo, huku kazi ya ukusanyaji akipewa mtumishi mwingine ambaye fedha hizo zinadaiwa kuwekwa kwenye akaunti binafsi inayohusishwa na mke wa mtumishi huyo.

Kinachozua maswali makubwa kwa watumishi ni hatua ya mamlaka kuishia kumhamisha mtuhumiwa mkuu wakati uchunguzi wa vyombo mbalimbali, ukiwemo wa TAKUKURU, ulidaiwa kuanza kufanyika kabla ya hatua hiyo ya uhamisho.

TAKUKURU walishafika na kuhoji watumishi wote waliohusika katika kupokea maelekezo ya kutoa pesa hizo, na kuna watumishi walikiri kuingiziwa pesa na kuombwa zirudishwe na DMO huyo.

Watumishi wengi sasa wanahoji:
1. Je, kuhamishwa ndio adhabu mpya ya matumizi mabaya ya fedha za umma?

Wengine wanaamini kuwa uhamisho huo wa haraka unaweza kuwa njia ya kuzima mjadala huku ukweli wa tuhuma hizo ukiachwa gizani bila majibu rasmi.

Chanzo kimoja kutoka ndani ya halmashauri, ambacho hakikutaka kutajwa jina kwa sababu za kiusalama, kilidai kuwa timu mbalimbali zilifika kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo wa fedha hizo, jambo linaloongeza uzito wa tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo wa zamani wa afya wilayani humo.

Pamoja na hayo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kueleza:
1. Nani anawajibika kati ya DMO au mtumishi aliyeagizwa na DMO?

2. Kwa nini akaunti binafsi ya mke wa mtumishi ilitumika?

3. Na kama uchunguzi ulikuwa unaendelea, kwa nini mtuhumiwa ahamishwe kabla ya kesi kukamilika?

Suala hili linaendelea kuzua mjadala mkubwa huku macho yakielekezwa kwa mamlaka za uchunguzi kuona kama haki itatendeka au sakata hilo litamalizwa kimya kimya kwa uhamisho wa kawaida.

Pia soma:

1. DOKEZO - Inawezekanaje Mganga Mkuu wa Halmashauri Mpimbwe Mwenye Tuhuma za Wizi wa Fedha Ahamishwe Kabla Uchunguzi Kukamilika, Au Ni Njia ya Kumlinda?

2. KERO - Halmashauri ya Mpimbwe inawatesa Wazabuni kwa kutolipa madeni

UPDATE: :
 
A

Anonymous

Guest
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imemhamisha aliyekua Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe kwenda halmashauri ya Mji Nanyamba huku akiwa na tuhuma za wizi wa fedha za serikali.

TAKUKURU wilaya walikuwa tayari wameanza uchunguzi kuhusu tuhuma hizo, lakini cha kushangaza mtuhumiwa amehamishwa kabla uchunguzi haujakamilika.

Suala hilo limeendelea kuibua mjadala kuhusu uwajibikaji, uwazi katika utumishi wa umma, na namna taasisi za serikali zinavyoshughulikia tuhuma zinazohusu matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Kwa hivyo gentleman,
ulitaka achunguzwa akiwepo right?🐒
 
Back
Top Bottom