Jamaanii kuku kamaliza debe la mahindi,karanga

Huyo kuku aweza kuwa na mafua ya ndege mwache mkuu,bora ufuge ngamia kwani kuhalalishwa mwenyewe akubali kwa maombi bila shari,ukimla kinguvu lazima akudhuru
sasa mkuu we fikili kaisha kula debe la mahindi,debe la karanga na sasa la mtama limefikia nusu.
Washauri mbengu zangu zipoteee hivi hivi sibora ningesipanda kwingine.?
 
Kuku huyu mayai bado ajataga iweje wenzangu wale mayai?
Cha ajabu kuku huyu mwanzo aliruka banda lao na kutua kwenye banda langu mwenye
kama aliruka banda lao na kutua kwenye banda lako, sasa kipi kikushangazacho? ATARUKA PIA KWAKO NA KUTUA KWA WENZAKO VILE VILE! pole lakini!
 
Jamani kuku kamaliza debe la mahindi,Niliaaza taratibu kumlushia mbegu za mahindi nilishutuka debe limekwisha ,hivyo hivyo kamaliza debe la karanga.Kuku huyu sasa kanenepa sana kapendeza sana na anavutikia kila kona anakopita.Kuku huyu kila inapofika siku ya kuliwa au kuchinjwa,utasikia kuku anaumwa tumbo,kuku ameshikwa na ungonjwa wa mafua.mala kuku anaendesha kila saaa.Kuku huyu utasikia akisema nipo mwezini, sikukuu hikifika hili aliwe kuku amekuwa anaruka kwa sababu ya mabawa yake.
Sasa waungwana na debe la mtama limefika nusu bado kuku ataki kuliwa,Tatito kubwa la kuku huyu kila asubuhi anapoamuka utasikia analalamika kuomba nimrushie mtama au nimpunguzie mtama.
Kuku huyu siku zinafika kuliwa kitoeo na kila zana zakumchinja zimeandaliwa,maji ya moto ya kumnyonyolea pia na grovis lakini kuku huyu anapotea mtaaa ataonekana jioni kuja kulala bandani kwake.?
Sasa kuku huyu ataliwa kubudu siku ikifika/

Huyo kuku ni wanyama au wamayai?
 
mtoa mada naomba nisichangie....! naomba kutoa pongezi binafsi kwako na kwa JF.!
Lugha nzuri ambayo watoto wetu wa darasa la sita labda wawe wamekaa na "mwalimu wa twisheni" ndio angalau wafunguke macho/japo kuna mitoto imeshatuzidi umri.
lugha hizi huweza kufanya JF ikawa mtandao salama pindi umkutapo mwanao anatembelea na kuwashauri wanafunzi watembelee majukwaa mbalimbali. kwa ajilinya kupata elimu maridhawa.....HONGERA
 
Labda kuku kaona hakuna jiko la mkaa la kumchomea. Anaogopa baridi ya kwenye freezer? Washa mkaa umeremete sawia, uone kama kuku hajaulizia kisu akakuletea uchinje mwenyewe,lol
 
kuku wako, manati ya nini? ukiona unahitaji manati basi ujue huyo si wako.pole kwa kuwafugia walaji wengine.yaani....kufuga ufuge wewe, kula wale wengine! inauma.


Hakuna siku nimeburudika kama leo hasa niliposoma huu uzi! Big up Mzee
 
Mtupie mtama karibu na mtego akisogea tu anaswe na kuliwa, hakikisha zana zote zipo tayari la sivyo atachoropoka
 
Usikute huyo kuku anakuwaga bize na jogoo lingine ila weye ni wakumpatia mtama na hiyo mikaranga....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom