Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

evangelical

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
5,984
Reaction score
9,938
Kuna jamaa yangu amepata janga,
Amepigiwa simu na baba mwene nyumba wake akamtaarifu kwamba amepata taarifa zenye ushahidi kwamba yeye huyo mshkaji wangu anatembea na mke wake, na akirudi lazima amtoe maini . Huyo jamaa mwenye nyumba ni contractor kwa sasa yupo safarini.
Jamaa kweli amekiri alikuwa anatoka na huyo mama kwa muda kabla hata hajaoa. Jamaa anasema huyo mama ndiye aliyejilengesha kwake, jamaa kwa tamaa na kushindwa uzalendo akamkubali, Mama mwenyewe hata sio mzuri sana anamiaka kama 30 na amezaa na huyo mume wake watoto 2.
Jamaa yangu ameshaishi kwa huyo mama zaidi ya miaka 2 amerenew juzijuzi tu mkataba wake wa mwaka wa 3.

Huyo mama ni mke mdogo wa huyo mkandarasi ambaye amemjengea nyumba ya ukweli maeneo ya kihonda huku moro ambayo ina servant quarter kubwa kwa nyuma ambayo ndio amepangishiwa mshakji wangu.
Huyo mkandarasi anasafiri sana na ana mke mkubwa mwingine pia hivyo mara nyingi haji hapo kwa huyo bi mdogo, ila anamgharamia kila kitu na amempatia harrier ya kutembelea,
Kuna kipindi huyo jamaa yangu kabla hajanunua gari yake nilikuwa namuona na hiyo harrier ya huyo mama alikuwa anakuja nayo hata job na kushinda nayo kama yake ,huyo bi mdogo ni mama wa nyumbani hiyo gari haitumii sana, wala hapendi kuendesha, huyo mshkaji wangu alikuwa pia kama dreva wa huyo mama,mida ya jioni akitoka job au siku nyingine akiwa off alikuwa anampeleka huyo bi mdogo sokoni na saloon,

Mshakji ndio ameoa hivi karibuni miezi kama 3 imepita amemuoa aliyekuwa mchumba wake na anaujauzito wa miezi 7.
Huyo mke wa mshkaji naye amepata hizo taarifa na amekasirika sana amemwambia mshkaji ampe nauli arudi kwao songea.
Jamaa ni mtumishi ameajiriwa kwenye idara ya serikali.
Huyo jamaa yangu ameghafirika sana hajui jamaa anaushaidi gani na atarudi lini, na ana hofu ya maisha yake, ana mpango wa kukimbia ahame mkoa kwa kuogopa, huyo bi mdogo naye kamchunia sijui naye kapigwa mkwara na mume wake.
Tumemshauri atulie amuombe mke wake msamaha na atafute nyumba nyingine wahame hapo kwenye hiyo nyumba haraka na ikiwezekana aende kuripoti polisi. Akikimbia anaweza kufukuzwa kazi.
Ushauri wa ziada kwa huyu ndugu yetu manake anaogopa sana.
 
Mke wa mtu sumu,mume wa mtu maziwa,uzinzi ni mbaya sana
 
Ndo inavyokuwa ukila vya watu maisha maish huwa ya wasi wasi ila hajitambui huwezi ukawa unakula mke wa mwenye nyumba na wewe unaishi hapohapo hizo siyo akili hata kidogo ndo akome anaghafirika nin alipokuwa anatembelea harrier hakujua kuwa yatamkuta?
 
Mwache aendelee kusubiri hapo hapo aje kuharibiwa heshima ya makalio yake...
 
huyo jamaa ni mpuuzi sana na ni haki yake kupigwa shaba.
 
Mwambie ahame mji, atakiona cha moto, mke wa mtu sumu na haikingwi na hata maziwa.
 
mh,hii imemkalia pabaya...jamaa yako alipitiliza yaani hadi kutumia gari alonunuliwa na mmewe? He will pay the price....hapo ni kukimbia tu kwanza kama anaweza,ila kama anaroho ngumu amface mwenye mali as if hajatoka na mamwenyenyumba maana hamna ushahidi hajakamatwa red handed
 
Watu wana ujasiri wa ajabu. Mwambie afanye mpango ahame mji maana hapo akisamehewa basi tigo inavunjwa.
 
Mwambie aache uoga kwani kafumaniwa...awe na msimamo wa kukataa kwa sababu hakuna ushahidi wowote uliopo
 
Kuna jamaa yangu amepata janga,
Amepigiwa simu na baba mwene nyumba wake akamtaarifu kwamba amepata taarifa zenye ushahidi kwamba yeye huyo mshkaji wangu anatembea na mke wake, na akirudi lazima amtoe maini (jamaa ana mguu wa kuku). Huyo jamaa ni contractor kwa sasa yupo safarini.
Jamaa kweli amekiri alikuwa anatoka na huyo mama kwa muda kabla hata hajaoa.
Jamaa yangu ameshaishi kwa huyo mama zaidi ya miaka 2 amerenew juzijuzi tu mkataba wake wa mwaka wa 3.

Huyo mama ni mke mdogo wa huyo mkandarasi ambaye amemjengea nyumba ya ukweli maeneo ya kihonda huku moro ambayo ina servant quarter kubwa kwa nyuma ambayo ndio amepangishiwa mshakji wangu.
Huyo mkandarasi anasafiri sana na ana mke mkubwa mwingine pia hivyo mara nyingi haji hapo kwa huyo bi mdogo, ila anamgharamia kila kitu na amempatia harrier ya kutembelea,
Kuna kipindi huyo jamaa yangu kabla hajanunua gari yake nilikuwa namuona na hiyo harrier ya huyo mama alikuwa anakuja nayo hata job na kushinda nayo kama yake ,huyo bi mdogo ni mama wa nyumbani hiyo gari haitumii sana, wala hapendi kuendesha, huyo mshkaji wangu alikuwa pia kama dreva wa huyo mama,mida ya jioni akitoka job au siku nyingine akiwa off alikuwa anampeleka huyo bi mdogo sokoni na saloon,

Mshakji ndio ameoa hivi karibuni miezi kama 3 imepita amemuoa aliyekuwa mchumba wake na anaujauzito wa miezi 7.
Huyo mke wa mshkaji naye amepata hizo taarifa na amekasirika sana amemwambia mshkaji ampe nauli arudi kwao songea.
Jamaa ni mtumishi ameajiriwa kwenye idara ya serikali.
Huyo jamaa yangu ameghafirika sana hajui jamaa anaushaidi gani na atarudi lini, na ana hofu ya maisha yake, ana mpango wa kukimbia ahame mkoa kwa kuogopa, huyo bi mdogo naye kamchunia sijui naye kapigwa mkwara na mume wake.
Tumemshauri atulie amuombe mke wake msamaha na atafute nyumba nyingine wahame hapo kwenye hiyo nyumba haraka na ikiwezekana aende kuripoti polisi.
Ushauri wa ziada kwa huyu ndugu yetu manake anaogopa sana.

Kwakua mwili hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe na tamaa ikikomaa huzaa dhambi na dhambi ikikomaa huzaa mauti hivyo hajashinda tamaa imezaa dhambi na dhambi hii imekomaa itazaa mauti ASUBIRI MAUTI MJINGA HUYO ATATEMBEAJE NA MKE WA MTU ILI HALI ALIKUWA NA MCHUMBA?
 
Mwambie jamaa amwambie huyo mke wa mwenye nyumba amwambie huyo mme wake(contractor) kwamba huyo jamaa mpenda wake za watu ni Afisa usalam..wa taif..
 
Apigwe tu kwanza ni mshenzi sana
Mke wa mtu sumu sana.
 
Yaani umewaanika hujawabakiza! Kama contractor ni memba humu huu ni ushahidi tosha.
Ahame kwanza hapo asap,wakati anatafakari atoke vipi kwenye hilo sakata aliloliingia.
Pole kwa mkewe
 
Hapo si pa kukaa,pili ajipeleke mwenyewe polisi akaripoti ametishiwa maisha ili jamaa aitwe awekwe kama ushaihidi kwa lolote baya litakalotokea then asimsogelee kabisa huyo hayawani(malaya mke wa mtu)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom