Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,649
- 140,207
Hiyo ni mwaka jana hiyo
Ninafahamiana sana Angel toka 2020 hivi kwa nyakati tofauti nimekuwa ninafanya naye kazi. Kusema kweli Angel ni mzuri, ana umbo na kalio la maana, ogopa sana dada mwembamba mwenye kalio, anakuwa na shape tamu balaa.
Wakati fulani nilikuwa namtamani sana, wakati fulani nilimweleza kweli, asingekuwa mke wa mtu nisingemuacha salama. Basi aliishia kucheka tu.
Mwaka mmoja tukajikuta wote tunasoma chuo kimoja lakini ni Blended(online). Sasa mwaka jana nikawa natakiwa kufika Campus, ikatokea coincidence na yeye akawa na changamoto kama yangu. Hivyo akaomba tusafiri pamoja.
Siku ya safari akanielekeza karibu na kwake nimpitie, atakuwa na mumewe. Nikaonana na jamaa akaniachia mke wake nisafiri naye.
Sijui kama uzungu au kumuamini sana, jamaa alinikabidhi mke wake akiwa kwenye nguo ya kubana mwili (tight). Wote mnajua mwanamke mwenye figure halafu avae tight anakuwaje. Mbaya zaidi tulikuwa tunatumia usafiri binafsi.
Badala ya kusema fisi kakabidhiwa kondoo nikajisemea inabidi kumuheshimisha huyu jamaa.
Tulivyofika campus tukakuta kuna uhaba wa guest houses zenye hadhi yetu. Nyingi zilikuwa zimejaa. Baada ya kuhangaika sana tukapata chumba kimoja. Muda ukiwa umeenda sana karibu saa 6 usiku Angel akaniambia brother tumezunguka sana tutumie tu chumba hiki wote.
Nikajiuliza peke yangu nitaweza kweli kulala bila kumgusa huyu, nikamkumbuka jamaa akinikabidhi mke wake bila kusema chochote. Nikaingiwa imani na kusema HAPANA hiki kikombe kiniepuke. Nikamwambia Angel pamoja na yote wewe lala tu, mimi nitalala kwenye gari, masaa 7 sio mengi. Akanisihi nijiamini tu, nisiwe na shaka kwani tunaheshimiana. Bado msimamo wangu ulibaki vilevile, nikamwambia mimi najijua tukilala humu wote nitakusumbua na tutavunjiana heshima.
Angel hakuelewa akaingia bafuni akabadilisha nguo, akavaa dela akapanda kitandani akavuta shuka akalala miguuni. Akaniambia nakuachia huko mbele 😊😊😊
Nikaingiwa ujasiri, nikamwambia njoo ufunge mlango mimi nalala kwenye gari. Nikiwa kwenye gari ananitumia sana sms ananiambia hakujua kama mimi ni dhaifu hivyo, ananibembeleza nisilale kwenye gari. Nikampotezea mazima, nikawa sijibu sms zake
Mwisho wa siku ikawa asubuhi, tukaenda chuo na mchana tukaanza safari ya kurudi.
My Take
Wanaume tukiamua kutokulombeana wake inawezekana.