Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

Ndiyo maana unaambiwa hapa duniani huwezi kusikia baba mwenye gari kuna BABA MWENYE NYUMBA TU. Sasa km wewe unajifanya mkware ishi kwenye gari yako tuone.
 
mkuu akiamua kukimbia naomba aniachie nafasio yake ya kazi huku mtaani kugumu,mwambie akimbie tuu aokoe maisha yake bwana ila hiyo kazi plz nijulisheni akiwa wazi.
 
Hii imekaa vibaya kwa huyu jamaa. Lakini anachoweza kufanya kwa sasa ni kwenda polisi amfungulie kesi huyo jamaa na ajitahidi polisi wamkamate akiwa hajarudi Morogoro. Hii itamfanya jamaa aogope kuua lakini ajihadhari sana.
 
Huyo jamaa atauawa. Mwambie ahame nyumba. Ama sivyo jamaa atalisuka mabaunsa watamla 0713.. Halafu wanaume hatujali kabisa hisia za mademu, yaani huyo jamaa ambaye dem wake analiwa hata hafikirii kwamba huyo mwanamke na yeye huwa anashikwa na nye-ge kipindi chote ambacho yeye anakuwa kwa mkewe?

Kweli kabisa hata huyo mke simlaumu kama kitanda, chakula, mavazi, nyumba,nk hata kwao vipo. Tatizo la wanaume wenye uwezo kiuchumi ni maskini wa kufikiri. Utashangaa anasema "huyu mwanamke nimemjengea nyumba,nimemnunulia gari na kila kitu ninampa,sijui nimfanyie nini aridhike" Hatambui kuwa kila kitu ni pamoja na yeye mwenyewe.
 
Kuna jamaa yangu amepata janga,
Amepigiwa simu na baba mwene nyumba wake akamtaarifu kwamba amepata taarifa zenye ushahidi kwamba yeye huyo mshkaji wangu anatembea na mke wake, na akirudi lazima amtoe maini . Huyo jamaa mwenye nyumba ni contractor kwa sasa yupo safarini.
Jamaa kweli amekiri alikuwa anatoka na huyo mama kwa muda kabla hata hajaoa. Jamaa anasema huyo mama ndiye aliyejilengesha kwake, jamaa kwa tamaa na kushindwa uzalendo akamkubali, Mama mwenyewe hata sio mzuri sana anamiaka kama 30 na amezaa na huyo mume wake watoto 2.
Jamaa yangu ameshaishi kwa huyo mama zaidi ya miaka 2 amerenew juzijuzi tu mkataba wake wa mwaka wa 3.

Huyo mama ni mke mdogo wa huyo mkandarasi ambaye amemjengea nyumba ya ukweli maeneo ya kihonda huku moro ambayo ina servant quarter kubwa kwa nyuma ambayo ndio amepangishiwa mshakji wangu.
Huyo mkandarasi anasafiri sana na ana mke mkubwa mwingine pia hivyo mara nyingi haji hapo kwa huyo bi mdogo, ila anamgharamia kila kitu na amempatia harrier ya kutembelea,
Kuna kipindi huyo jamaa yangu kabla hajanunua gari yake nilikuwa namuona na hiyo harrier ya huyo mama alikuwa anakuja nayo hata job na kushinda nayo kama yake ,huyo bi mdogo ni mama wa nyumbani hiyo gari haitumii sana, wala hapendi kuendesha, huyo mshkaji wangu alikuwa pia kama dreva wa huyo mama,mida ya jioni akitoka job au siku nyingine akiwa off alikuwa anampeleka huyo bi mdogo sokoni na saloon,

Mshakji ndio ameoa hivi karibuni miezi kama 3 imepita amemuoa aliyekuwa mchumba wake na anaujauzito wa miezi 7.
Huyo mke wa mshkaji naye amepata hizo taarifa na amekasirika sana amemwambia mshkaji ampe nauli arudi kwao songea.
Jamaa ni mtumishi ameajiriwa kwenye idara ya serikali.
Huyo jamaa yangu ameghafirika sana hajui jamaa anaushaidi gani na atarudi lini, na ana hofu ya maisha yake, ana mpango wa kukimbia ahame mkoa kwa kuogopa, huyo bi mdogo naye kamchunia sijui naye kapigwa mkwara na mume wake.
Tumemshauri atulie amuombe mke wake msamaha na atafute nyumba nyingine wahame hapo kwenye hiyo nyumba haraka na ikiwezekana aende kuripoti polisi. Akikimbia anaweza kufukuzwa kazi.
Ushauri wa ziada kwa huyu ndugu yetu manake anaogopa sana.

Hasira za nini wee bwanaaa, wewe una wako nyumbani nami ninawangu nyumbani chuki ya nini kati yangu mimi nawewe nasema sina makosa weee bwanaaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom