Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

Jamaa katembea na mama mwenyenumba kimenuka ushauri

Mwambie aache uoga kwani kafumaniwa...awe na msimamo wa kukataa kwa sababu hakuna ushahidi wowote uliopo
Jamaa hajui jamaa anaushahidi wa namna gani, au anamtisha tu. inaonekana jamaa alikuw anajiachia sana na huyo wife mdogo wa mtu. jamaa anaweza asiwe na ushahidi wowote labda anamtisha tu. Jamaa akomae sio kweli.
Kutoa taarifa Polisi pia inaweza saidia au? Jamaa hawezi kukimbia mji manake anapiga kazi mjini na ofisini kwake kunajulikana.
 
Lazima kuna sehemu amekosea ,ila hilo sio kubwa kulitatua ,na yeye ashushe mkwala na atafute mguu wa kuku atembee nao ,ila asikubali kabisa kabisa akatae kwa nguvu zake zote .
 
Yani mtu unaambiwa usitembee na mke wa mtu lakini wewe hutaki, unajifanya wewe ndo kidume sana, handsome zaidi ya wengine, mjanja wa mjini n.k. Acha apigwe tu, manake hakuna namna nyingine sasa, na mimi nasema huyo contractor ampige tu manake tumechoka sasa
 
acha kuzungumzia nafsi ya tatu.. wewe ndio umefanya hivyo kubali tukushauri vyema...
 
Mke wa mtu ni sumu,usijaribu chombeza,yatakuja yakukute usiyoyategemea!
 
Umenena mkuu. Kuna madem kibao kitaa, kwa nini kum-do mke wa mtu?

kama huna sumu sogea kahumba pesa mbele unajichagulia,jamaa lazima atatue linda,muandalie KY tu
 
bora ukae mbali na hiyo nyumba kama anakaa kihonda mwambie aelekee njia ya mbeya kwa kuwa kaajiliwa, kama kajiajiri ahame mji....ukikaa hapo jamaa akirudi tena yupo kwake....atakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza analotaka.

kuna mjumbe kashauri ukatoe taarifa polisi, hivi unaenda kusemaje? wakikuu;liza kwa nini amekutishia kifo?
 
Mwambie jamaa amwambie huyo mke wa mwenye nyumba amwambie huyo mme wake(contractor) kwamba huyo jamaa mpenda wake za watu ni Afisa usalam..wa taif..
duh...!!! hiyo series ya kupeleka ujumbe mimi hoi..
 
Hiyo ndo hasara ya tamaa,ange2lia na mkewe hyo presure acngeipata.
 
mh huyo ajiandae tu mshauri aandike urithi wa mtoto wake huyo aliyeko tumboni kwa sababu atamwazha ivi ivi.
 
Napenda kutofautiana na washauri wote wa hapo juu!

Mambo ya kuripoti polisi wakati unajijua ushagonga mke wa mtu na mwenye mali ana ushahidi ni kukuza tatizo x 100000...unaweza ukamshinda mdai wako kwa mambo ya kipolisi, lakini kimtaamtaa ishu itakuwa na moto wa gesi, na akufuatilia kama vile anatrack nyayo za simba.

Binafsi ninachoona chaweza kufanyika kikasaidia ni jamaa awe mpole.
Ajikubalie moyoni kwamba ametenda hilo kosa na hawezi kujificha popote...U can run but you cant hide.!

Akishajikubali kuwa amekosa asisubiri jamaa arudi, aulizie huyo mhandisi yuko mkoa gani, na amfuate kiumeni hukohuko mkoa, afanye mbinu yoyote akutanishwe nae na aongee kwa maana ya kuomba Msamaha na kumsihi jamaa yaishe!
Zaidi ya hapo binafsi sioni njia yenye usalama!...

Ushauri wa eti ahame nyumba au akimbilie mkoa mwingine ndiyo kumrahisishia mhandisi kumnyofoa jamaa bandama kwa kutumia vijana au wazee wa kazi!

Mwambie jamaa afuate ushauri huu, hapa bana hakuna kujifanya mjanja, mke wa mtu ni kifo na asipofanya hivi nilivoshauri atarajie BIG RESULTS NOW.
Nawasilisha.
 
Kuna jamaa yangu amepata janga,
Amepigiwa simu na baba mwene nyumba wake akamtaarifu kwamba amepata taarifa zenye ushahidi kwamba yeye huyo mshkaji wangu anatembea na mke wake, na akirudi lazima amtoe maini . Huyo jamaa mwenye nyumba ni contractor kwa sasa yupo safarini.
Jamaa kweli amekiri alikuwa anatoka na huyo mama kwa muda kabla hata hajaoa. Jamaa anasema huyo mama ndiye aliyejilengesha kwake, jamaa kwa tamaa na kushindwa uzalendo akamkubali, Mama mwenyewe hata sio mzuri sana anamiaka kama 30 na amezaa na huyo mume wake watoto 2.
Jamaa yangu ameshaishi kwa huyo mama zaidi ya miaka 2 amerenew juzijuzi tu mkataba wake wa mwaka wa 3.

Huyo mama ni mke mdogo wa huyo mkandarasi ambaye amemjengea nyumba ya ukweli maeneo ya kihonda huku moro ambayo ina servant quarter kubwa kwa nyuma ambayo ndio amepangishiwa mshakji wangu.
Huyo mkandarasi anasafiri sana na ana mke mkubwa mwingine pia hivyo mara nyingi haji hapo kwa huyo bi mdogo, ila anamgharamia kila kitu na amempatia harrier ya kutembelea,
Kuna kipindi huyo jamaa yangu kabla hajanunua gari yake nilikuwa namuona na hiyo harrier ya huyo mama alikuwa anakuja nayo hata job na kushinda nayo kama yake ,huyo bi mdogo ni mama wa nyumbani hiyo gari haitumii sana, wala hapendi kuendesha, huyo mshkaji wangu alikuwa pia kama dreva wa huyo mama,mida ya jioni akitoka job au siku nyingine akiwa off alikuwa anampeleka huyo bi mdogo sokoni na saloon,

Mshakji ndio ameoa hivi karibuni miezi kama 3 imepita amemuoa aliyekuwa mchumba wake na anaujauzito wa miezi 7.
Huyo mke wa mshkaji naye amepata hizo taarifa na amekasirika sana amemwambia mshkaji ampe nauli arudi kwao songea.
Jamaa ni mtumishi ameajiriwa kwenye idara ya serikali.
Huyo jamaa yangu ameghafirika sana hajui jamaa anaushaidi gani na atarudi lini, na ana hofu ya maisha yake, ana mpango wa kukimbia ahame mkoa kwa kuogopa, huyo bi mdogo naye kamchunia sijui naye kapigwa mkwara na mume wake.
Tumemshauri atulie amuombe mke wake msamaha na atafute nyumba nyingine wahame hapo kwenye hiyo nyumba haraka na ikiwezekana aende kuripoti polisi. Akikimbia anaweza kufukuzwa kazi.
Ushauri wa ziada kwa huyu ndugu yetu manake anaogopa sana.

So mmeamua kumuweka contractor humu?ole wenu kama ni memba
 
Shigongo at work!! Hizi story zingine huwa sifiki hata mwisho!
Sioni ni kwa mantiki gani mnadhani huu ni utunzi!...mbona hii ni situation ya kawaida sana, na kila siku haya yanatokea mtaani, au mnapanic kwavile inahusisha Harrer?

Hiyo negligence yenu ina'derail mtiririko mzuri wa ushauri, na wengineo wenye mawazo ya kutembea na wake za watu wataona kama vile hii ishu ni ya kutunga na hivyo wataanguka tena kwenye kitanzi cha aina hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom