Jamaa aomba kufungwa amkimbie mkewe

Jamaa aomba kufungwa amkimbie mkewe

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,712
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 katika jiji la Kansas nchini Marekani aliyepora bank kwa makusudi ili afungwe na kukaa mbali na mkewe, amepatikana na hatia na kuhukumiwa kukaa nyumbani miezi 6 na kuzuiwa kutoka bila ridhaa ya mkewe.

Lawrence John Ripple (kushoto) alivamia bank ya biashara ya Kansas na alipofika dirishani alimlazimisha tarishi (teller) ampe dola 2,924 akimtisha kwamba asipompa atampiga risasi. Alipopewa fedha hizo aliondoka, lakini baadae aljisalimisha polisi akiwa na kiasi chote cha pesa alichopora na kuwaambia polisi "mimi ndiye mtuhumiwa mnayemtafuta"
_
Kabla ya kufanya tukio hilo Lawrence alikuwa katika mzozo na mkewe na alimwambia mkewe kuwa ni bora akaishi jela kuliko kuendelea kuishi nae.

Wakili wa Jamhuri aliitaka mahakama kumuachia huru kwani kumfunga means mahakama itakua imekula njama za kumsaidia Lawrence kufanya jinai. Wakili huyo alisema taarifa ya daktari inaonesha Lawrence alipata msongo mkubwa wa mawazo kutokana na kitendo hicho, pia alikua amefanyiwa upasuaji wa moyo miezi michache iliyopita hivyo alihitaji kukaa na mkewe ili aweze kumuuguza.

Hata hivyo Wakili wa utetezi aliiomba mahakama imtendee haki mteja wake na kumfunga walau miezi kadhaa jela ili aweze kukaa mbali na mkewe.

Mahakama ilimpata Lawrence na hatia, lakini ilitupilia mbali maombi ya upande wa utetezi na kumhukumu Lawrence adhabu ya kukaa nyumbani miezi 6, na kuzuiwa kutoka bila ruhusa ya mkewe.!
FB_IMG_1561551904877.jpeg
 
Kuna nyakati kama mama anasema sana nyumbani unaweza kuiona nyumba chungu,that's the power of a woman,pamoja na miguvu yako yote lakini inafika mahali unakuwa mdogo kwake...
 
Kuna nyakati kama mama anasema sana nyumbani unaweza kuiona nyumba chungu,that's the power of a woman,pamoja na miguvu yako yote lakini inafika mahali unakuwa mdogo kwake...
Tuliopitia mkoleni tulifundishwa yote hayo. Usiwe na hivi, mume akikuudhi mwambie yaishe.
 
Asee ogopa sana hiki kiumbe mwananamke....anaweza kukufanyia visa ukaomba dunia ipasuke...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee mi ningekiuka saana halafu nione adhaby
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sasa akikiuka watamfanya nini?

Je watampleka gerezani? Au watamuongezea muda wa kukaa ndani?
 
Back
Top Bottom