Waziri wa Afya wa Kenya Aden Duale, ameamuru kusitishwa mara moja kwa ujenzi wa kituo cha karantini ya ugonjwa wa Ebola kinachofadhiliwa na Marekani katika kambi moja ya jeshi Nanyuki iliyopo county ya Laikipia ambako kumeshuhudiwa maandamano makubwa yaliyosababisha vifo kupinga mpango huo.
Hatua hii imekuja baada ya waziri huyo kupatikana na hatia ya kuidharau mahakama kwa kutofuata amri ya kusitisha ujenzi huo. Amri iliyotolewa Mei, 2026
Hata hivyo, Juni 22, 2026, jaji alitoa uamuzi kuwa Duale alipuuza amri hiyo na kuruhusu mradi huo uendelee. Leo Juni 23, 2026, Waziri wa Afya Aden Duale alifika Mahakamani akikabiliwa na kesi ya kuidharau amri ya mahakama ambapo Mawakili wa upande uliofungua kesi hiyo dhidi ya Duale walikuwa wamemwomba jaji kumpa waziri huyo kifungo cha miezi 15 jela.
Duale alikiri kufanya kosa na kuomba Mahakama imsamehe na kuthibitisha kuwa serikali imesitisha mpango huo uliokuwa umependekezwa. Jaji wa Mahakama Kuu, Patricia Nyaundi, alikubali ombi la msamaha la Duale na kusema kuwa waziri huyo "amesamehewa lakini amepewa onyo kali."
Akizungumzia hatua zinazofuata, Duale alisema kuwa serikali za Kenya na Marekani zimekubaliana kusitisha ushirikiano uliokusudiwa kuhusu kituo hicho cha Ebola kufuatia amri hiyo ya mahakama. Maombi ya kutaka afungwe jela yametupiliwa mbali.
Source: BBC