Jakaya Kikwete: Rais Samia anaendesha nchi vizuri, tuendelee kumuunga mkono

Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.

Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.

My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.

----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2

Rais Mstaafu Kikwete amesema haya

"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote"

"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini"

====

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kwa uongozi imara katika kuhakikisha Huduma za Matibabu ya Dharura zinashushwa ngazi ya Hospitali za Wilaya.

Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pongezi hizo leo alipohudhuria hafla ya makabidhiano ya ramani katika eneo la ujenzi wa jengo la Huduma za Matibabu ya Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze- Msoga kwa Mkandarasi.

“Tulipokuwa na wazo la kujenga Hospitali yetu hii mpya tulizungumza na viongozi wa ABBOT pamoja na Dkt. Dorothy Gwajima wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, alisatusaidia sana”ameshukuru Mhe. Kikwete.

Hospitali ya Chalinze, Msoga inakuwa Hospitali ya kwanza ya Wilaya kuwa na Huduma za matibabu ya dharura nchini huku ikiwa kwenye eneo ambalo ni njia panda ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Kati ya nchi na Nyanda za Juu Kusini eneo ambali halina huduma za dharura kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa huduma za haraka hususani wale wanaopata ajali.
View attachment 1937945
Amsafishe na udhaifu unaouona wewe pekee au unamaanisha kuwa Rais Samiha ni dhaifu?
 
😁😁😁

0AIS-7z.jpg
 
Umeshapata uteuzi au bado ndio umeanza kujipendekeza
Wala sina haja ya uteuzi lakini ukweli lazima tuseme. Ndani ya hii miezi sita tumaini limeonekana. Sisi wadaiwa wa bodi ya mikopo na watumishi, wakulima tunaelewa nini Hangaya anafanya na lazima tuappreciate. Huu utamaduni wa kuponda kila kitu ulitugharimu huko nyuma.
Najua hawezi kumaliza kero zote ndani ya nusu mwaka, Ila anaonyesha matumaini.
 
Hata mimi ningekuwa nanufaika na utawala wake iwe halali au haramu pia ningesema hivyo hivyo. Mafuta ya kula lita 20 sh. 89,000/= sukari kilo 2,900/= tozo za miamala ya simu, tozo za mita za nyumba, ugaidi wa kusingiziana!!! Mhh kweli alieshiba hamjui mwenye njaa.
Mafuta na sukari vimeanza kupanda baada ya Samia kuingia madarakani?
 
Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.

Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.

My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.

----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2

Rais Mstaafu Kikwete amesema haya

"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote"

"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini"

====

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kwa uongozi imara katika kuhakikisha Huduma za Matibabu ya Dharura zinashushwa ngazi ya Hospitali za Wilaya.

Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pongezi hizo leo alipohudhuria hafla ya makabidhiano ya ramani katika eneo la ujenzi wa jengo la Huduma za Matibabu ya Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze- Msoga kwa Mkandarasi.

“Tulipokuwa na wazo la kujenga Hospitali yetu hii mpya tulizungumza na viongozi wa ABBOT pamoja na Dkt. Dorothy Gwajima wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, alisatusaidia sana”ameshukuru Mhe. Kikwete.

Hospitali ya Chalinze, Msoga inakuwa Hospitali ya kwanza ya Wilaya kuwa na Huduma za matibabu ya dharura nchini huku ikiwa kwenye eneo ambalo ni njia panda ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Kati ya nchi na Nyanda za Juu Kusini eneo ambali halina huduma za dharura kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa huduma za haraka hususani wale wanaopata ajali.
View attachment 1937945
Akili za kuambiwa Changanya na zako

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Umepagawa nini wewe hukuona kura ya Mungu iliompa Samia urasi ? Weka kwenye akili yako na uzingatie Mungu huwa anamuondoa mtu ili mwingine achukue nafasi.
Weka hapa uthibitisho hiyo kura ilipigwa lini? Acha pang'ang'a mingi

By the way CCM hua mnaamini kwenye kura au mnakuwa na matokeo yenu tayari hata kabla ya zoezi??

Jinsi mlivyonyanyasa mawakala wa vyama pinzani especially CHADEMA na ACT ni Mungu gani huyo mnayemzungumzia wapi au mungu wa chato?
 
Piga kazi mama Kuna watu tuna imani utatuvusha, nilichogundua nchi hii hata tukiongozwa na malaika bado maneno hayatakosekana. Walioko nje ya system lazima watataka kuaminisha watu kuwa huwezi ili wapate nafasi
 
Weka hapa uthibitisho hiyo kura ilipigwa lini?

By the way CCM hua mnaamini kwenye kura au mnakuwa na matokeo yenu tayai hata kabla ya zoezi?...

Kwa watu wenye imani ya Mungu huamin kua Mungu huumpa ufalme amtakaye na humnyima ufalme amtakaye wewe uwe na majeshi na kura zote ziwe zako kama Mungu hakuandika wewe kua Mfalme katu haiwi atakufanyia chochote kile ili usikae pale na unaweza kua kapuku kama tulivyo mimi na wewe kama Mungu alituandikia kuwa Wafalme iko siku unashitukia umekua Mfalme bila hata mwenyewe kujua hivi kwa akili yako iliwahi kupita kichwani mwako kua ikosiku Mgufuli angekua Raisi wa nchi hii? ukimtizama alikua na uzito upi ktk Chama CCM?

Na weka akilinimwako Mungu huliadhibu taifa fulani kwa uovu wao kwa kuwapa kiongozi MUOVU pia huwa hulipa nafuu taifa fulani kwa kuwapa kiongozi Mwema
 
Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya
Muda wake uliisha huyu Mzee kimya, hatuhitaji kusikia lolote toka kwake, kwani sisi hatuwezi ku-assess utendaji wa Kiongozi?
 
Back
Top Bottom