Jakaya Kikwete achaguliwa kuishinikiza Taliban kurudisha watoto wa kike shule

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289

Ndio maana mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau hii United Nations na mpaka kutishia kuacha kuchangia...

Sasa Kikwete masikini ya Mungu eti anatumwa aka negotiate na Taliban kurejesha watoto wa kike shule akiwa kama mwenyekiti wa Global Partnership for Education.

Mtu atakaepata mkanda wa mazungumzo ya Kikwete na Taliban atauza filamu ya comedy kali kuliko zote Afrika kama wasipom-behead mkutanoni.

Lakini lengo pana zaidi la GPE ni kupeleka fursa ya elimu bora kwa kila mtoto mnyonge duniani.

Huku nyumbani the Kikwetes of the third world wamefanya nini japo kujaribu kumpa mtoto mnyonge elimu wanayopata watoto wao binafsi? (Kumbuka hotuba ya JK kwenye mazishi ya JPM alivyoeleza bila aibu jinsi watoto wake wanavyosoma shule za academy).

Wanachaguliwa na UN kwa vigezo gani watu hawa hawa waliofeli katika mambo hayo hayo ya kuwapa nafuu wanyonge?
 
Huwa wanasema nabii hasifiki kwao je unataka kusema United Nations hawajawaona hao wewe uliowaona wanahekima na diplomasia ya juu kumzidi kikwete au unataka kutuaminisha kuwa huo ni uteuzi wa mchongo labda kama mimi na wewe tunamuelewa Kikwete katika nyanja tofauti ila He is the best sio kwa hilo tu lakini ni mwanadiplomasia bora na ni Tunu yetu hiyo
 
Naona mpigania legacy unaendeleza chuki zako kwa jk baada ya kushindwa kila kitu kuhusu yeye.

Hv wapigania legacy, kwanini mnamchukia sana the simple JK? Ndo mlivyoagizwa na mungu wenu?

Hilo ni jambo la kimataifa, mazungumzo yake yanaratibiwa vizuri kwa makubaliano ya pande mbili a wanapanga hadi wapi wakutane. Kusema watamla kichwa ni mawazo finyu ya Kiswahili uliyonayo kwa kudhani kuwa huko kuna kuchambana chambana tu km kwenu buza. JK amewatangulia mno, nyie endeleeni kujipanga!
 
Yaani kikwete una muona ana cheka cheka unahisi ni naive, weak na asiye na skills.

Tafuta profile yake utamjua vyema.

Ukion hadi Nyerere alimkubali those time tambua aliona kitu kwa huyu Jamaa. Mtu aliye pitia mafunzo ya kijeshi, hadi kufika vyeo kama Kanali tena jeshi lile la zamani, tambua humo kichwani na moyoni anavitu flani flani.
 
Usichokielewa ni kwamba , Taliban na JK wote wanamwabudu mtu mmoja , lzm watasikilizana , Taliban ni kivuli tu na sasa hv yanatengenezwa mapicha ili msishangae taifa X likianza kupeleka misaada Afghanstan ya Taliban , maisha ya dunian ni movie tupu , wenye akili ndo wanaelewa
 
Ndio maana mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau hii United Nations na mpaka kutishia kuacha kuchangia...

Sasa Kikwete masikini ya Mungu eti anatumwa aka negotiate na Taliban kurejesha watoto wa kike shule akiwa kama mwenyekiti wa Global Partnership for Education.

Mtu atakaepata mkanda wa mazungumzo ya Kikwete na Taliban atauza filamu ya comedy kali kuliko zote Afrika kama wasipom-behead mkutanoni.

Lakini lengo pana zaidi la GPE ni kupeleka fursa ya elimu bora kwa kila mtoto mnyonge duniani.

Huku nyumbani the Kikwetes of the third world wamefanya nini japo kujaribu kumpa mtoto mnyonge elimu wanayopata watoto wao binafsi? (Kumbuka hotuba ya JK kwenye mazishi ya JPM alivyoeleza bila aibu jinsi watoto wake wanavyosoma shule za academy).

Wanachaguliwa na UN kwa kigezo gani watu hawa hawa waliofeli katika maeneo hayo hayo ya kuleta maendeleo kwa watu masikini?

JK ni mwanadiplomasia mzuri sana....usimchukulie poa.
 
Back
Top Bottom