Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

Kama kusudio la ccm kupata katiba mpya ni hili basi hakuna maana tena ya kuwa n a katiba mpya. katiba ni mali ya wananchi wote watanzania na si ccm. itapoteza maana kama ccm wataendelea kuhujumu mchakato huu.
 
  • Thanks
Reactions: Ptz
Ingekuwa ni kukusanya maoni tu bila tafakuru hata wewe na Bulembo mngeweza kufanya hivyo. Ile kazi inahitaji weledi kama Warioba na wengine. Sasa wanapowapa somo lazima mkubali sababu Warioba hatumii kichwa kufugia nywele kama wewe.

Yeye anatumia kichwa kutafakari. Tunajua rasimu (sio mswada kama unavyoonyesha ukilaza wako hapa na si kweli ulipitishwa na wabunge wa CCM na CDM kama unavyochanganya hapo juu) imewashika pabaya maCCM na warioba kawashika sehemu mbaya mpaka mzae naye mwaka huu.

Tatizo la CCm wakizidiwa wanawatuma mburula waropoke kwani vilaza hawana nyuso za haya kama Bulembo. Wenye akili wanajua tu jamaa katumwa na CCM kule kwenye mkutano wa NEC
CCM inaelekea kubaya sana, hawa ndio watu wa propaganda! real. Nawakumbuka akina Paul Sozigwa, Msekwa n.k. halafu naangaalia kizazi cha Nape sina la kusema.

Mimi sina tatizo akibaki huko ICU-CCM, wasi wasi wangu anaweza kabisa kuwa miongoni mwa watu wenye maamuzi katika kundi au taifa letu.

- Kisheria Warioba hana haki zaidi yangu na wewe ni mwananchi tu wa kawaida ndio maana hana mamlaka ya kuamua Katiba mpya ni CCM yenye Wabunge wengi bungeni yenye hayo mamlaka,

Le Mutuz

Babu yangu William malecela, kuanzia sasa nakudharau kuliko kiasi. Nisamehe bure
 
  • Thanks
Reactions: Ptz
- Chama chenye majority kisingeweza kwenda kujiunga na Chama walichokiita cha Mashoga, tuliza boli mkuu umekurupukazzzz!!1

Le Mutuz

KWA AKILI yako ulitaka tuungane na nyie mafisadi? hamna jipya mmechuja sana mtajibaraguza bure kwa wananchi haswa sisi wakulima tushawachoka kabisa nyie wahuni na hatukusema ni mashoga ila itikadi yao inatetea hilo jambo elewa umepata shahada bure wewe mzee kachemka kupata mtoto boya Kama wewe kheri ungekuwa wa jinsia nyingine.
 
  • Thanks
Reactions: Ptz
Tatizo nchi hii kila mtoto wa mkubwa sasa anajiona anahaki ya kuropoka chochote mbele ya wapiga kura wa taifa hili. W.J Malecela huna cha kulidanganya taifa unahakika na kauli unazoleta hapa kwamba huo muswaada umepitishwa na wabunge wote maCCM na CDM? Nenda Mtera ukalime ZABIBU watanzania wa leo wameamka, upuuzi wenu sasa hivi parking yake ipo LUMUMBA na siyo ktk vichwa vya watanzania, kama unabisha subiri 2015, na lazima tuyaburuze magamba the HAGUE
 
  • Thanks
Reactions: Ptz
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

Una uelewa mdogo sana wa mambo dogo! Inaonekana wewe ndo mshauri mkubwa wa Burembo, tunawatamania sana nyinyi watoto wa maccm, ukweli ni kuwa kinachokuweka hapo ni nyota ya libaba lako, nyota ambayo mwisho wake umefika. Pole sana.
 
Sheria, kanuni na mazoea ni vitu vyenye ukaribu lkn sheria ni bosi wa vyote, warioba anaongea kisheria, bulembo anaongea kwa kanuni za chama na W.J Malecela unatumia uzoefu na mbaya unasafiria kivuli cha uzoefu wa baba yako. Sheria inamruhusu warioba kutoa elimu au ufafanuzi ktk kifungu chochote au utaratibu wowote ktk suala la katiba,

Bulembo yeye ni mwananchi wa kawaida alipaswa kuomba muongozo kwa mwenyekiti wa tume ya katiba km kuna kitu haelewi.
Pia msisahau rais hasubiri kusaini katiba bali muswada wa mabadiliko ya katiba, hapa mjue bado hatujapata rasimu ya pili ya katiba , na hiyo ni kazi ya warioba, na pia milango ya utoaji wa maoni kwa makundi maalum haijafungwa, ccm waende Ohio street wakatoe maoni na bulembo awe msemaji kama Nape yupo likizo. Kufanya kazi kwa mazoea bila shule ni tabia ya akina bulembo.
 
Mzee J.S yupo katika rekodi ya kutaka katiba ifanyiwe mabadiliko,tena iandikwe upya akiwa waziri mkuu. Sijui kwanini hajamsimulia mwanae kada wa chama sasa hivi.

Huyu bwana asiyejua tofauti ya rasimu na mswada wa sheria sijui ingekuwaje huko EAC, dah kuna hatari na majanga. Yote ni kazi ya mola kuwaepusha viumbe wake.

Huyu bwana anayeamini kuwa katiba inaandikwa na bunge ndiye angekuwa mjumbe wa NEC. Kazi ya mungu haina makosa.

Huyu bwana anayeamini katiba ya nchi inaandikwa na chama tawala ndiye anapita nchi nzima akitoa elimu kwa uma. Mungu wetu atukuzwe na sifa zote njema ni zako.

Huyu bwana anayeamini Warioba ametoa maoni kwasababu tu yanapingana na chama chake ndiye alikuwa awe mbunge wa EAC. Ahsante mungu kwa kutuonea huruma.

Ewe mwenyezi usituache viumbe wako, umasikini, maradhi na ujinga vimepiga kambi Tanzania. Hakuna dalili yoyote ya kuondoka kwani mizizi inatotokeza tena bila haya soni au aibu licha ya ujenzi wa shule za kata .

Basi nasi sote tunyanyue vichwa kwa unyenyekevu tukisema Amina.

Sheria, kanuni na mazoea ni vitu vyenye ukatibu lkn sheria ni bosi es vyote, warioba anaongea kisheria, bulembo anaongea kwa kanuni za chama na W.J Malecela unatumia uzoefu na mbaya unasafiria kivuli cha uzoefu wa baba yako. Sheria inamruhusu warioba kutoa elimu au ufafanuzi ktk kifungu chochote au utaratibu wowote ktk suala la katiba,

Bulembo yeye nini ni mwananchi wa kawaida alipaswa kuomba muongozo kwa mwenyekiti wa tume ya katiba km kuna kitu haelewi.
Pia msisahau rais hasubiri kusaini katiba bali muswada wa mabadiliko ya katiba, hapa mjue bado hatujapata rasimu ya pili ya katiba , na hiyo ni kazi ya warioba, na pia milango ya utoaji wa maoni kwa makundi maalum haijafungwa, ccm waende Ohio street wakatoe maoni na bulembo awe msemaji kama Nape yupo likizo. Kufanya kazi kwa mazoea bila shule ni tabia ya akina bulembo.
Sikubaliani nawe sehemu moja ya kivuli, maana kama angekuwa anasafiria kivuli cha baba yake asingesahau ugomvi wa baba yake na Nyerere ulikuwa juu ya nini.

Hoja zingine ulizosema masikini mwana wa Malecela hana habari nazo.
Yeye katumwa maneno basi anasema tu tena akiwa na kofia kama kithibitisho cha elimu.
Hajui mswada, hajui kazi za tume, hajui sheria iliyoanzisha tume, hajui rasimu yupo bize kumtukana Warioba.

'Napeh' ni kiboko, anaweza kumtuma mtu avue nguo na mtu akafanya hivyo. Nina mu admire sana 'Napeh' kwa kipaji.
Balozi anajuta! Katibu mkuuubwa anajuta! seuse 'mabolizozo'
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

jamani huu ni umbutika wa ajabu sana mdau williamu , mtoto wa malichela, hivi kweli rasimu iko bungeni?au ni muswada wa sheria ya mchakato wa kuapata katiba mpya?jamani kama haujui,vyema kuuliza wataalamu wa mambo; na hasa mwenendo wa mambo ya kibunge.hakuna rasimu iliyopelekwa bungeni mpaka sasa, na pia bado hata kuandikwa majumuisho ya maboresho ya mabaraza ya katiba , hatuna rasimu ya pili baada ya maboresho.hivyo hakuna rasimu iliyopelekwa bungeni.na kama ulitaka kumtetea bulembo tafuta namna nyingine na si kupotosha kuwa rasimu tayari inasubiriwa kusainiwa.huo ni umbutika wa kisheria
 
Malecela tafadhali elewa nauone mbali, kwa sasa tunayo rasimu chapa ya kwanza, tunasubiri chapa ya pill kisha bunge la katiba na mwisho kura ya maoni ya ndiyo, sasa kwa wasomi wapenda uzalendo tunasema, mchakato mbovu utaleta rasimu ya mwisho mbovu inaweza kukataliwa na wananchi na mahakama ya katiba, je unaweza kutafakari kwa haraka kama mchakato mzima utafeli itakuwa ni upotevu wa Billion ngapi, sasa haya yote yatakwenda vema km tume ya katiba itakuwa independent organ. Malecela nakuona una umri mkubwa kidogo lkn sijui ni kwanini elemu yako ni ya shule za kata. Ugomvi ulio ktk bunge kwa sasa si katiba noo ni muswada unaoruhusu kuwepo kipengele cha marekebisho ya katiba. Swali langu kwako tume ya warioba ikivunjwa na rasimu ya katiba haikupata kura za ndiyo je tutaunda tume nyingine maana ya warioba haipo na mwisho nani atafanya kampeni ya kura za ndiyo ni belembo au kinana? Katiba ni sheria ya nchi na sio ccm, chama cha siasa kitakachoundwa mwaka 2020 kitaongoza nchi kwa katiba hiyo. Hatuangalii kesho
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

basi mnaipeleka nchi pabaya! Eti #CCM ndio wanaamua katiba iweje! Upo serious Kiongozi?
 
Hata bulembo huwa anajisifu ujinga, hutoka ktk Mada anuai km wewe na hajui kitu, hii ni dalili huwa unatumika, sasa wewe umechaguliwa na mkutano mkuu,hao wakuu si akina Bulembo, hebu kanusha kwanza.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz
Haya maneno ni yako au yametoka kwa Baba yako? Only John ndiye anaweza kumwita Judge Warioba "Warioba",
 
sina uhakika na umri wako lakini we ni miongoni mwa vitu vinavyokera hapa duniani yaani huna tofauti kabisa na kinyesi cha binadamu

Ningeshauli lugha laini nyepesi inayoeleweka kwa watz wote make matusi na vjembe havjengi.Tujipange kwa nguvu za hoja tutafkia muafaka tu!!
 
Daima mwenyezi Mungu hawatupi walio wengi wamuombao kwa dhati na katika haki.

Ninaamini kuwa Taifa letu linaelekea ktk kupata mapinduzi ya kweli.Simaanishi mapinduzi ya chama bali mapinduzi ya viongozi wenye hekima,busala,hofu ya Mungu na uzalendo.

Ninachoshauli kwa sasa,tuwe makini sana kuwaangalia viongoz wetu hawa kwa jicho la pili ili ifkapo 2015 tuwe na maamuzi sahihi.

Hongera na pole zimfikie mzee Warioba na tume nzima kwa kazi ngumu,ninasmama nkimuomba Mwenyez Mungu azid kuwaongoza na kuwatia ujasili.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Hii kaz angepewa dingi yako, ungepiga kelele!!! Haaaa haaaa....... Mnatafunana mchana kweupeeee
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF

kaazi kwelikweli!
Watu kama Bulembo nahisi wanataka katiba mpya ipatikane kwa bloodshed. Tusivuruge wala kuhujumu utaratibu mzima wa kupata katiba mpya, madhara yake ni makubwa; mambo yanaweza haribika.
 
Mzee J.S yupo katika rekodi ya kutaka katiba ifanyiwe mabadiliko,tena iandikwe upya akiwa waziri mkuu. Sijui kwanini hajamsimulia mwanae kada wa chama sasa hivi.

Huyu bwana asiyejua tofauti ya rasimu na mswada wa sheria sijui ingekuwaje huko EAC, dah kuna hatari na majanga. Yote ni kazi ya mola kuwaepusha viumbe wake.

Huyu bwana anayeamini kuwa katiba inaandikwa na bunge ndiye angekuwa mjumbe wa NEC. Kazi ya mungu haina makosa.

Huyu bwana anayeamini katiba ya nchi inaandikwa na chama tawala ndiye anapita nchi nzima akitoa elimu kwa uma. Mungu wetu atukuzwe na sifa zote njema ni zako.

Huyu bwana anayeamini Warioba ametoa maoni kwasababu tu yanapingana na chama chake ndiye alikuwa awe mbunge wa EAC. Ahsante mungu kwa kutuonea huruma.

Ewe mwenyezi usituache viumbe wako, umasikini, maradhi na ujinga vimepiga kambi Tanzania. Hakuna dalili yoyote ya kuondoka kwani mizizi inatotokeza tena bila haya soni au aibu licha ya ujenzi wa shule za kata .

Basi nasi sote tunyanyue vichwa kwa unyenyekevu tukisema Amina.

Kwa level ya William Malecela nilidhani hili ni jambo dogo sana kuelewa na kuitofautisha. Hata hivyo, baada ya kusoma hii shule yako natuma atakuwa ameelewa. Ila sasa bado natafakari kama ndo angekuwa Mbunge wa Afrika Mashariki.
 
Back
Top Bottom