Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

...Dr Anatoa mihadhara Universities huko Marekani. JK anakumbatiwa na kupewa PhD za kumwaga huko mMarekani kama shukrani za dhahabu wanazobeba Tz.

- Hapa haihusu sio mahali pake hapa ni mjadala wa katiba na Warioba.

Le Mutuz
 
Kuna watu wengine wanataka kutulazimisha kufanya vyama vyao kuwa Tanzania.

Kama kuna mtu anaamini warioba kaleta mawazo yake na siyo ya wananchi si ataje ni mawazo yepi?

Je si unajua kuwa kuna kura ya maoni?

Kwa nini usielimishe wananchi ili wayakatae mawazo hayo kuliko kupotosha?

Watanzania ndio wanaojua katiba wanayoitaka si chama chochote cha siasa.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

wewe na bulembo ni moja ya wavuta bangi maarufu sana pale ccm...Mngekuwa na staha,hekima na busara msingesita kumuita warioba chemba ili kupata muafaka juu ya madai mlioropoka kule TANGA.msiwafanye watz washindwe kumwaamini RAIS wa tz kwani ndiye aliyemchagua WARIOBA.KWANINI MNATAKA KUMFANYA RAIS KIKWETE AONEKANE DHAIFU???

Tatizo kubwa la viongozi wabishi,wafu kwenye fikra,wanaoongozwa kwa nguvu za giza,wanaotumia majini kama miungu yao huwa hawadumu.

Msipojirekebisha uongeaji WENU,
msipobadilika kimtazamo,
msipotenda haki,
msipoonyesha uwajibikaji kwa wachache wanaowaamini,
msipoacha kumdhalilisha RAIS kwa kuwa ndo mteuzi wa WARIOBA,
msipoweka hekima na busara kama dira ya nafasi mlizo nazo kwenye jamii hamtadumu kwenye siasa za tz kwa kipindi kifupi sana.MSHIKE SANA ELIMU USIMWACHE AENDE ZAKE.
 
Hivi Malecela unatumiaga Cigar kubwa au una-comment wakati ukiwa nyingi kichwani?Maana wewe hata ukielekezwa mara ngapi bado hutaelewa.Nahisi hao walimu waliokufundisha walipata shida sana na wewe.Mtu una bichwa kubwa kama nyumbu lakini zito kuelewa.
Tunarudia tena yale mapendekezo yaliyomo katika Rasimu sio mapendekezo binafsi ya Jaji Warioba kama unavyofikiri,Yale na maoni ya Watanzania wote.Alichofanya yeye ni kuzichukua zile hoja zilizotokana na kundi kubwa zaidi la watoa maoni na kuziingiza katika Rasimu.Kwahiyo kilichomo katika hiyo Rasimu kinatokana na Watanzania wengi zaidi.Si unajua tena sisi Wananchi ndio wamiliki halali wa hii Katiba na siyo nyinyi Wanasiasa.Tunachokifanya hapa ni kuwaandikia Mkataba mpya ili tukiwapa Nchi mfanye yale tutakayowaandikia katika huu Mkataba sasa sielewi kwanini tena nyinyi waajiriwa hamuutaki Mkataba tunaouandaa sisi Waajiri wenu badala yake mnataka mtuandikie Mkataba nyinyi,Mliona wapi hiyo?

- Kaka pole sana bad timing ya chama chako Chadema, mmekosea ombeni kwa CCM tuahirishe mambo ya Katiba mpya maana time is not on your side, hilo lichama lenu mmejaza washauri vilaza sana nenda usome historia ya kubadilisha katiba Duniani uje hapa uniambie ni wapi Duniani iliwahi kutokea chama Minority na Waziri Mkuu wa zamani waliwahi kubadili katiba mpya ya taifa hakuna mkuu, poleni sana ndio tatizo lenu la kulilia lilia mambo msiyoyajua sasa limewapoasukia, poleni sana!!

Le Mutuz
 
wewe na bulembo ni moja ya wavuta bangi maarufu sana pale ccm...Mngekuwa na staha,hekima na busara msingesita kumuita warioba chemba ili kupata muafaka juu ya madai mlioropoka kule TANGA.msiwafanye watz washindwe kumwaamini RAIS wa tz kwani ndiye aliyemchagua WARIOBA.KWANINI MNATAKA KUMFANYA RAIS KIKWETE AONEKANE DHAIFU???

Tatizo kubwa la viongozi wabishi,wafu kwenye fikra,wanaoongozwa kwa nguvu za giza,wanaotumia majini kama miungu yao huwa hawadumu.

Msipojirekebisha uongeaji,
msipobadilika kimtazamo,
msipotenda haki,
msipoonyesha uwajibikaji kwa wachache wanaowaamini,
msipoweka hekima na busara kama dira ya nafasi mlizo nazo kwenye jamii hamtadumu kwenye siasa za tz kwa kipindi kifupi sana.MSHIKE SANA ELIMU USIMWACHE AENDE ZAKE.

- ha! ha! ha! ha! ha! imenivunja mbavu sana fungua thread ya wavuta bangi CCM, lakini hapa umeingia mahali sio pako, Sheria ya jamhuri ipo wazi kwamba Warioba na Chadema pamoja na CUF hamna nguvu ya kubadili katiba ni CCM tu yenye wabunge 280 ndio wenye haki kwa sababu inawakilisha wananchi wengi sana wa Taifa hili sio Chadema wala Warioba.

Le Mutuz
 
1. ndio maana kuna Tume ilisema Wananchi wa Tanzania 80% hawataki vyama vingi vya siasa, lakini Serikali ya CCM ikaapuuza na kuruhusu Wapinzani.

2. MWalimu alipokuwepo sikuwahi kusikia Warioba anataka Serikali tatu, sasa leo ameibukia wapi na hizi habari za Serikali tatu?

1. Hizo zilkuwa busara za Baba wa Taifa, na wananchi wote wanalijua hilo.

2. Suala la serikali tatu si la Warioba, ni sisi wananchi ndiyo tunataka mfumo huo; yeye anatimiza wajibu wake aliopewa na Rais wa nchi, mbona mnamuingia kwenye kazi yake?.
 
- Ni maneno ya mtaani hayana anything to do na political reality ya bongo sasa hivi, Warioba na Chadema hawana nguvu kisheria ya kuandika Katiba mpya ila ni CCM tu yenye nguvu kisheria ya kuandika katiba mpya, Warioba na Chadema wanatakiwa kuomba huruma ya CCM ili katiba mpya labda iwe na mambo yao, lakini Sheria ya jamhuri ya Tanzania ipo wazi kwamba ni CCM tu wenye majority ndio wenye haki ya kuamua namna katiba mpya iwe!

- Pole sana mkuu, huu ndio ukweli wa mambo wacha kujaza maneno ya mtaani haya tunajadili the future of this nation sio mambo ya kijinga jinga ya mtaani, soma tema katiba utajua inasema wazi kwamba kwenye hili la katiba mpya ni CCM tu ndio wenye the final desicion on katiba mpya. Kama una tatizo na mimi na maisha yangu fungua thread yake, hii sio! ha! ha!

Le Mutuz
Kuwa mtoto wa kiongozi si kujua kila kitu au kuharibu kazi za wenzako.Tena vijana kama nyie
mgekuwa wapole kwelikweli katika hatua muhimu za mabadiliko ya watu wote kimfumo.

Kwa mwenye akili nyingi na timamu moja kwa moja atakuona wewe kama ni mtu fulani
uliyetumwa kuharibu kazi za wenzako kwa kujifanya mkeleketwa wa chama tawala ili hapo
baadae uweze kuteuliwa katika nafasi fulani.Anyway unaweza kuteuliwa/kuchaguliwa kupitia
mgongo wa familia yenu,lakini hiyo haijalishi sana kwani si kila mtu atakuwa kiongozi.

Wana CCM kuendelea kumchokonoa Mzee Warioba na tume yake ni sawa na kuendesha
kampeni za kupunguza kura 2014-2015.

Kama ni majority ndio wenye uamuzi kwanini msiache taratibu na kanuni zilizowekwa na tume
zimalizike? Si vema kumdakiadakia mtu kabla hajamaliza kuongea.
 
Kwani Warioba akiwa mwenyekiti wa tume hiyo inamuondolea haki yake ya uraia katika kutoa maoni yake?!

Au ndio ule msemo '' Simple minds discuss.........................''
 
quote_icon.png
By W. J. Malecela
- Mbona Mwenyekiti wako Chadema ana elimu ndogo sana, toa boriti kwako kwanza mkuu!!, halafu PhD ya Dr. Slaa ni ya wapi eti? ha1 ha! h!

Le Mutuz

...Dr Anatoa mihadhara Universities huko Marekani. JK anakumbatiwa na kupewa PhD za kumwaga huko mMarekani kama shukrani za dhahabu wanazobeba Tz.

quote_icon.png
By W. J. Malecela
-- Hapa haihusu sio mahali pake hapa ni mjadala wa katiba na Warioba.

Le Mutuz

..... kumbe ukifundishwa unaelewa? Nashukuru umejigundua mwenyewe.
 
Kwani Warioba akiwa mwenyekiti wa tume hiyo inamuondolea haki yake ya uraia katika kutoa maoni yake?!

Au ndio ule msemo '' Simple minds discuss.........................''

- Sawa sawa hana haki ya kusema maoni yake akiwa kwenye tume, akitaka ajivue kwanza kuwepo kwenye tume ndio atoe maoni yake kama sisi wengine wote, hiyo ni sheria wala sio maneno ya mtaani na yeye Warioba anajua sana, poleni sana!1

Le Mutuz
 
1. Hizo zilkuwa busara za Baba wa Taifa, na wananchi wote wanalijua hilo.

2. Suala la serikali tatu si la Warioba, ni sisi wananchi ndiyo tunataka mfumo huo; yeye anatimiza wajibu wake aliopewa na Rais wa nchi, mbona mnamuingia kwenye kazi yake?.

- Rais hakumpa wajibu wa kuwafokea wananchi kwamba Serikali Tatu lazima zitakuwepo, na hakumpa wajibu wa kupiga piga kelele majukwaani alichotakiwa ni kukusanya maoni tu ya kuyafikisha kwa aliyemtuma sio kuanza kuamua maoni yawe vipi.

- Eti unaposema sisi wananchi unawaongelea wananchi gani waliokupa dhamana ya kuwaongelea? Sema wewe unataka Serikali tatu sio sisi

Le Mutuz
 
Kwa hali ya kawaida, hata kama Warioba kaandaa rasimu, bado ana haki msingi ya kuchangia mawazo.

Anayesema warioba haruhusiwi kusema chochote kuhusu rasimu haeleweki.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF

Acha watafunane wenyewe kwa wenyewe, bahati mbaya sisiemu imegawanyika makundi mawili kundi moja ni lile linaloshikilia imani na itikadi ya uanzishwaji wa sisiemu itikadi ya mwanzo kabisa. hawa ni wale wenye msimamo kama wa baba wa taifa wanaojali maslahi ya wananchi walio wengi (kama kina Warioba) kundi la pili ni wale ambao wanaona wamechelewa sana kuzitumia fursa hapo awali na sasa wameamua kutafuna kila kinachokaribia machoni pao wanatafuta umaarufu na fedha hawajali tena maslahi ya wananchi hawa ndio kama kina Bulembo na viongozi wengine wengi walioko madarakani
CHONDE CHONDE RAISI KIKWETE ULIOWATEUA WANAKUPIGA CHANGA LA MACHO,WANATOA RIPOTI NZURI LAKINI UHALISIA WAKE SIO. HASA KATIKA ELIMU, AFYA, ARDHI, UCHUMI,MAJI NK. HALI YA WANANCHI SI SHWARI. HUSHANGAI HALI ILIVYO SASA KITU KIDOGO TU WANANCHI WAMEPIGA MTU AU WAMEGOMA AU WAMETUKANA .TUNAELEKEA SHIMONI USIPOANGALIA KWA UMAKINI TUNAINGIA KWENYE KINA KIREFU SIJUI TUTATOKAJE HUKO
 
- Sawa sawa hana haki ya kusema maoni yake akiwa kwenye tume, akitaka ajivue kwanza kuwepo kwenye tume ndio atoe maoni yake kama sisi wengine wote, hiyo ni sheria wala sio maneno ya mtaani na yeye Warioba anajua sana, poleni sana!1

Le Mutuz

Well, Le Mutuz ninafahamu hilo, kwani ina maana kila Warioba anachoongea tangu awe mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya inachukuliwa kuwa ni maoni ya mwenyekiti?!

Tatizo lipo pale Bulembo anapoona mawazo yote ya Warioba ni mawazo ya mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya huku Warioba naye akiona Bulembo anaongea kwa niaba ya CCM.

Warioba na Bulembo wote wana haki ya kuzungumza kwangu tatizo ni pale wanapozungumza kwa mamlaka ya ofisi zao...
 
- Warioba anauliza kama Bulembo ametumwa na CCM, lakini yeye hajasema kama anatumwa na Tume nzima kwa kila alilokwisha lisema toka awe kwenye tume hiyo ndicho kinachochekesha sana hapa, otherwise Bulembo kama Kiongozi wa CCM tena mjumbe wa Kamati kuu ana haki ya kumkumbusha Warioba kwamba hana mamlaka ya kuamua katiba mpya, anayo mamlaka ya kukusanya maoni tu!!

Le Mutuz
 
Kwa hali ya kawaida, hata kama Warioba kaandaa rasimu, bado ana haki msingi ya kuchangia mawazo.

Anayesema warioba haruhusiwi kusema chochote kuhusu rasimu haeleweki.

- Mmezoea sana kutawaliwa kwa maneno ya hali ya kawaida badala ya Sheria, pole sana mkuu Sheria inasema Warioba akitaka kutoa maoni yake binafsi ajitoe kwenye tume kwanza!!

Le Mutuz
 
- Mmezoea sana kutawaliwa kwa maneno ya hali ya kawaida badala ya Sheria, pole sana mkuu Sheria inasema Warioba akitaka kutoa maoni yake binafsi ajitoe kwenye tume kwanza!!

Le Mutuz

una hangover ya viroba!
 
Ukiangalia Vyombo vya habari vinavyoripoti habari za bwana warioba ni rahisi kupata majibu
 
Ukiangalia Vyombo vya habari vinavyoripoti habari za bwana warioba ni rahisi kupata majibu

- Kwamba nayo mengi yamenunuliwa kwenye kujaribu kutafuta njia ya mkato kubadili katiba, upo right sana ila tupo wananchi wengi tu ambao tutaendelea kusema wazi bila kuogopa wala kutishika, kwamba Sheria ya Tanzania sasa hivi ipo wazi kwamba ni Majority bungeni yaani CCM ndio wenye haki ya kubadili katiba watakavyo lakini sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Kumbe wewe na Bulembo mnazo akili zinazofanana..ni kama sasa Chama kinaanza kupoteza credibility kutokana na matamshi ya wajinga wachache..Nenda kwenye shria iliyounda hii tume ya Mabadiliko ya Katiba utakutana na kipengele kinachompa mamlaka ya kukusanya maoni pamoja na kutoa elimu ya katiba mpya..tena ilisisitizwa kuwa ni TUME ndio yenye mamlaka katika kufanikisha...

Tufanyage utafiti kabla ya kulaumu.
 
Back
Top Bottom