Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

Yaani wewe kuzaliwa ni kwamba Mama yako ametoa tu Maradhi tumboni! sijui asingekuzaa angekuwaje?!

Halafu wewe MISS BANTU mbona huwa unapenda sana kupost ujinga kwenye mambo ya msingi?
Au kukaa kwako huko kwa wazungu kumekufanya upungukiwe na ufahamu.isije kuwa jamaa walikuchezea makalio ndio ufahamu ukakutoka?? Nadaut sana!
 
Wewe na Bulembo ni waganga njaa. Haujisikii vibaya kuongozwa na Bulembo ambaye mara kadhaa kabwagwa chini uchaguzi wa udiwani Kijitonyama; Kiboko yake ni Juma Ulole Ulole, Bulembo ni darasa la VII halafu CCM mnampa madaraka mtu mwenye shule ndogo

'Makamu wa Rais' wa Slaa katika uchaguz wa 2010 hakuwa na walau Cheti cha Pre Form One! Ina maana kama Babu angeupata Ukikwete halafu akadanja kabla ya 2015 tungeongozwa na Binadamu asiejuwa walau Definition yA Definishen ya ' URAIS'!
 
dah! Kiukweli, wananchi wote wenye uelewa na uzalendo wa kweli, tutahitaji serikali tatu. Ningependa ile kanuni/sheria ya america ya watu fulani kupiga kura za maamuzi iingie hapa kwetu pia, kwani maamuzi ya wengi nayo ni tatizo kwetu. Wengi wanamezeshwa ujinga. Wazanzibar naamini mtatusaidia kufanikisha hili.
 
Kama uelewa wa viongozi wetu ndiyo huu, tumekwisha. Kwamba mpaka muda huu kuna Viongozi hawajui tofauti ya rasimu ya Katiba na Sheria ya mabadiliko ya Katiba. Kama William mpaka hii page ya 14 hajastuka namna anavyojivua nguo kwa uelewa mdogo juu ya jambo kama hili tunategemea nini kwa Mwenyekiti wake Bulembo!

Halafu CCM hawana Watu wakuweka mambo sawa hata kwa njia ya simu pale Viongozi wao wanapojichanganya mtandaoni. Kwamba Nape Nnauye umeshindwa hata kumpigia simu William ili asiaibike. Ama hamjui aibu ya mtu kama huyu (Mtoto wa Waziri mkuu na Makamu mwenyekiti wa Ccm) inavyokiharibu Chama chenu?

Kama hawa ndiyo Watu tunaowapa dhamana ya kulinda Taifa letu tujue tulishapigika kitambo!
nguruvi 3 @ngw'amapalala na wengineo huu ni "msiba" kwa Taifa.

So dissapointed
 
lemutuz shirikisha ubongo wako be4 you post, katiba inayoundwa si kwa ajili ya ccm wala cdm.ni ya watz wote, lakin ccm kwa kutumia uwingi wa uwakilish wenu bungeni mnataka kutuletea katiba ya ccm na sio ya wa tz. Hatuko tayari kuona hilo
 
Mimi napenda nimtetee Malecela Jnr kama binadamu lakini sizitetei hoja zake kuhusiana na mchakato wa katiba kwa sababu hazina hoja, hazina ukweli na ni garbage in, garbage out.

Mimi naona watu wanaomuhusisha baba yake malecela Jnr kwenye hii kadhia nao wanakosa werevu na hekima. Hawa ni watu wawili wazima tofauti. Mawazo, fikra na utendaji wao katika jamii na hasa kisiasa ni vitu viwili tofauti.

Utendaji wa baba yake hauwezi ukahusishwa na utendaji wa mwanae kwenye mambo ya kimaisha na kisiasa. Makosa ya malecela Snr hayawezi kuwa binded together na kuwa pia ni makosa ya Malecela Jnr na pia kinyume chake ni sawa.

Kumshushia maneno ya dharau na kejeli Mzee Malecela siyo busara hata kidogo hasa kama unajitambua. Ukubwa wa jina la Malecela usiwe ni sumu kwa wanae na vituko vya Malecela Jnr isiwe ni tiketi ya kumshushia heshima Mzee Malecela.

It's sad, siasa zinatufanya mpaka tunaanza kukosa ubinadamu ambao ni naturally given na tunachagua hate.

Siasa tulizikuta, na siasa tutaziacha. Kwa nini tusijadili mambo ya kisiasa kwa maelewano tukiongozwa na misingi ya kukubali kutokubaliana?.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz
Icho chuo kilichokutunuku shahada walikupa bure au ulisomea kweli maana unachofafanua ata hakieleweki.Rasimu ya katiba imepelekwa katika bunge lipi wakati bunge la katiba bado.Warioba yupo sahihi sheria iliyounda tume yake inampa mamlaka ya kuelimisha wananchi juu mambo yote ya katiba,sasa ulitaka asiwaambie wananchi maana ya katiba ili wajadili nini?au wamjadili warioba binafsi kama mnavyotaka makada wa CCM iliyopoteza mwelekeo.Nakushauri mtumie vizuri mzee Malecela kukujenga kisiasa,iyo ni fursa adhimu ambayo wengine hawana.Baba yako anaheshimika na watanzania wote kwa sababu ya uwezo wake wa kujenga hoja.Waingereza wana msemo usemao"Creative mind discusses issues while simple mind discusses individuals",wewe ni msomi tafakari na uchukue hatua.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Le Mutuz kulikuwa na haja gani kumpa Bulembo huo ujumbe ili amwambie wariomba while u can do it on ur own brother?

You have the courage mkuu why unamtumia Bulembo? Haya maneno yaliyosemwa jana ulianza kuyapigia chapuo humu mapema sana na jana yametamkwa na mwenyekiti wako, sasa umefurahia kuwa ujumbe umefika?

Unayajua majukumu ya jaji wariomba ndani ya tume hii?

Maoni yaliyotolewa na wananchi tanzania bara na visiwani umeyaona naukayasoma?

Kwa nini mnadhani wariomba katunga mambo yake mpk kufikia hatua ya kusema kuwa anawasemea watanzania?

Mkiambiwa mmeutaka mswaada huu mtakataa? Mnajitia kitanzani sana kwa kauli zenu nyeupe kaa muvi za adui yenu bila kujua watanzania wanawacheck tu
 
afu we lemutuz OLE WAKO KESHO UENDELEE NA PUMBA ZAKO, IVI HAUNA MSHAURI? Jamaa UNAJIVUA NGUO MBELE ZA WATOTO, MODS WATU KAMA HAWA UNAPIGA BAN WAJIFUNZE. Haiwezekani ad page ya 14 MTU ANAANDIKA PUMBA ,WATU WANAMWELEWESHA LAKINI HAELEWI! We mgogo gani wewe LEMUTUZ?
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

magamba hayataki katiba mpya ndio maana yanapiga siasa za maji taka ktk jambo hili mwenyeketi wenu amteue nyie mumshambulie majanga upogo
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Je, CCM ina haki ya kuwasemea Watanganyika au Wazanzibari? Mbona hamtaki kuwapa serikali wazitakazo?
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF

Suala la katiba mpya siyo sera ya CCM ndio maana wameshavuruga na wanaendelea kuvuruga mchakato wa katiba mpya
 
Jamani mna uhakika huyu le mituz hayupo na chupa ya whisky pembeni. Hizi dharau anazoeleekeza kwa warioba si bure. Anaongea km mhuni tu wa kijiweni. Warioba anahatarisha vitumbua vyenue! Lakini ndugu Willy si vema kuposti kwenye mitandao ukiwa mlevi. Ni aibu!
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

Unajua Job descriptions za tume ama ndo siasa tu na mambo ya kusikia?
 
dah! Kiukweli, wananchi wote wenye uelewa na uzalendo wa kweli, tutahitaji serikali tatu. Ningependa ile kanuni/sheria ya america ya watu fulani kupiga kura za maamuzi iingie hapa kwetu pia, kwani maamuzi ya wengi nayo ni tatizo kwetu. Wengi wanamezeshwa ujinga. Wazanzibar naamini mtatusaidia kufanikisha hili.

kweli wamekunywa maji ya green ni unazi wa vyama na itikadi hakunaga utaifa majanga
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

Hili jamaa linaongea nini? Unajiabisha hapa ndugu, kümbe ndio unavyoelewa hivi. Khaaaa!
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada,....

Wakati tulipokuambia hapa jamvini kuwa hufai hata kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ulidhani tuliokosea?

Hata kama hiyo rasimu ndiyo imekuwa mswada, nani amekuambia kuwa mswada hauongelewi?

- tunaishi kwa Sheria sio kanuni,

C.r.a.p from an aspiring legislator! Unapoendesha gari barabarani unatakiwa kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.

Kama tunaishi kwa sheria tuu na siyo kanuni, basi kusingekuwa na kanuni za usalama barabarani.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz
Ingekuwa ni kukusanya maoni tu bila tafakuru hata wewe na Bulembo mngeweza kufanya hivyo. Ile kazi inahitaji weledi kama Warioba na wengine. Sasa wanapowapa somo lazima mkubali sababu Warioba hatumii kichwa kufugia nywele kama wewe. Yeye anatumia kichwa kutafakari. Tunajua rasimu (sio mswada kama unavyoonyesha ukilaza wako hapa na si kweli ulipitishwa na wabunge wa CCM na CDM kama unavyochanganya hapo juu) imewashika pabaya maCCM na warioba kawashika sehemu mbaya mpaka mzae naye mwaka huu. Tatizo la CCm wakizidiwa wanawatuma mburula waropoke kwani vilaza hawana nyuso za haya kama Bulembo. Wenye akili wanajua tu jamaa katumwa na CCM kule kwenye mkutano wa NEC
 
Wakati tulipokuambia hapa jamvini kuwa hufai hata kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ulidhani tuliokosea?Hata kama hiyo rasimu ndiyo imekuwa mswada, nani amekuambia kuwa mswada hauongelewi?
Ndiye alikuwa atuwakilishe EAC!!! Lahaula!
Huyu asiyekumbuka kuwa mzee wake alikuwa champion wa katiba tena kwa utaratibu wa 'ukumbini'

Lakini EMT kwa nchi yetu bado hatujapona. Ipo siku utasikia ni balozi, waziri au mkuu wa mkoa kama si wilaya. Tatizo tu 'mzee alitibuana' na mtandao. Hata hivyo kuna kusameheana hasa tukielekea 2015.

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom