Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Mzee warioba kujibishana na mtu mdogo sana kama Bulembo ( ambaye hapo alipo amepachikwa kama boya ) ni kujivunjia heshima bure , wewe ni mtu mkubwa mno , bulembo hata Mungu akiwa Abdalah hawezi kufika hata robo ya ulipofika .
 
Samahani naomba CV ya bulembo na ya w.j. Malecela kwa mnaozijua
 
- hatuwezi kuongelea rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema bulembo ni sawa sawa kwamba warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, warioba kama mwananchi wa tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- narudia tena warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu katiba, hatuwezi kujadili rasimu sasa maana tayari rasimu ipo bungeni inasubiri saini ya rais twende kwa mbele.

le mutuz

hapo pekundu, inatia shaka sana kama uelewa wa viongozi wa ccm kama wewe huu ndo uelewa wenu, basi tusitegemee chochote chanya
 
- Katiba mpya mmeitaka wenyewe mkjiua wazi kwamba hamuwezi kubadili anything kwa sababu hamna wabunge wa kutosha, sasa mnalilia nini na mnamlilia nani hasa?

Le Mutuz
huku umepotea bana.leo bado sojaona post ya mbebs yeyote kule fb kumbe uko huku!pls funga mjadala hapa rudi kule fb mabs wako wanakisubiri bana.hapa wapo watu wanaojadili hatma ya nchi yetu aka sirias people.pls wahi kule fb fans wako wanakusubiri
 
Namshauri warioba afanye kazi yake aache mdomo haitamsaidia zaidi atajizalilisha tu.
 
William ni mmoja wa Watanzania waliobahatika kuona sehemu tofauti na Tanzania ingawa sina uhakika kama exposure hiyo inamsaidia.

Ni mtoto wa Mzee Malecela aliyeshika nyadhifa nyingi serikalini ikiwa ni pamoja na uwaziri wa mambo ya nje,uwaziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais na mgombea mtarajiwa wa Urais CCM mara mbili

Nashawishika kusema William ana mtukana mzee wake kwa sababu za kuthibitika kutokana na maandishi yake

Si kawaida kumjibu kwa kutambua ufinyu na maono yake, ninachotaka kufanya ni jamvi kumuelewa na kuelewa upotoshaji na matusi kwa wazee akiwemo baba yake.

Hoja ya serikali 3 ilianza siku nyingi na kundi la G55 liliifikisha bungeni.
Kundi hili lilikuwa na wabunge 55 wa chama tawala CCM kilichokuwa na wabunge zaidi ya 200.
Kiongozi wa serikali bungeni alikuwa baba yake william mzee J.S.Malecela.

Hoja ya G55 ilikataliwa na Nyerere kwasababu kuu mbili, kwanza haikuwa sera ya CCM na haiwezi kufanyika bila wananchi kuulizwa. Nyerere alitambua kuwa kubadili katiba ilihitaji ridhaa ya wananchi na si CCM.
Nyerere alimtuhumu Malecala kwa kumshauri rais vibaya.

William anaposema sera ya CCM ni serikali 2, wakati baba yake ambaye ni mwanzilishi wa CCM alitaka serikali 3 Kupitia idadi ya wabunge 55 kama ambavyo wapo 47 wa upinzani sasa ni kutoelewa anaongelea nini.
Hapa William hamtukani Warioba anamtukana baba yake mzazi. Hii kama si laana sijui ni nini.

William na kofia ya degree na kuishi nje ya nchi hajui kuwa katiba si ya chama ni ya wananchi.
Hatambui kuwa katiba haina chama kwasababu vyama vinapita katiba inabaki.
KANU na UNIP hazipo tena lakini Kenya na Zambia zipo.
Sasa kuaminisha kuwa CCM ndio wanaandika katiba, inasikitisha sana!!

Aasema wabunge wa CCM wana haki ya kuandika katiba. Hilo tu linaonyesha jinsi asivyojua katiba ni kitu gani. Lakini pia hajui hata sera za chama chake.

CCM haina sera wala haikuwa na ilani ya kuandika katiba.Hakuna kikao chochote kiwe cha NEC, CC au kamati ya wabunge kilichojadili suala la katiba.'Haki ya kuandika katiba'' wanaipata wapi?

Willy, CCM kupitia tume ya Jaji Nyalali, Kisanga na Warioba zimeshawahi kuleta maoni ya serikali 3.
Hakuna mahali katika rekodi CCM imewakemea kwa hilo. Warioba kama baba yako Malecela ndio wenye chama na wanaijua nchi kabla hujazaliwa. Kuwatukana wakiwemo akina Kisanga, Nyalali n.k. ni laana, ungama sasa hivi.

Willy, anasema kazi ya tume ya Warioba ni kukusanya maoni. Tume ya Warioba si makarani ni watu wenye weledi wa kueleza watu nini maana ya katiba ili watoe mawazo kulingana na hadidu za rejea.
Hadidu za rejea wamepewa na JK ambaye ni mwenyekiti wa CCM, kumtukana Warioba ni kumtukana JK, laana hiyo!

Willy anasema Warioba asiandike katiba aachie wananchi. Wakati huo huo haelezi wapi Warioba amelazimisha mawazo yake. Amesahau kuwa mawazo ya wananchi aliyokusanya Warioba ndiyo yale ya G55 ambayo baba yake alisimama Kidete kutetea akiwa na CCM ya wabunge 55.
Vipi amtukane baba yake kupitia Warioba kama si laana.

Williama na Bulembo hawaelezi wapi Warioba na tume yake wamelazimisha mawazo yao.
Wanasema wananchi wamekataa maoni ya Warioba, hawaelezi ni kigezo gani kimetumika kusema wananchi 'wamekataa' hata kabla ya kura ya maoni achilia mbali bunge la katiba.

Willy anasema kazi ya Warioba imekwisha kilichofikishwa bungeni mswada.
Mungu wangu! huyu ni kiongozi ambaye hajui kuwa kilichofikishwa si mswada wa rasimu ni marekebisho ya mswada ambao ulianzisha tume ya Warioba. Hajui kipi kimeanza kipi kinafuta na kitamalizika kipi. jamani!

Anasema wabunge wa CCM wanapaswa kuandika katiba, aibu kubwa!
wabunge wapi kwasababu hiyo si kazi ya chama na hata hao wabunge hawajui ni kitu gani kwasababu haipo katika ilani yao wala sera, sijui kama Willya anajua anachoandika.

Nia si kumjibu kwasababu hana hoja, ninachotaka Wanajamvi wafahamu ni kuwa huyu ipo siku utamsikia ni mjumbe wa NEC au CC. Unaweza kumsikia ni waziri, balozi wetu nchi za nje au mwenyekiti wa bodi ilimradi tu anaweza kuwa sehemu ya maamuzi yanayowahusu Watanzania.

Kwa mtu asiyejua kwanini Tanzania ni masikini basi ajiulize tena.

Mkuu hapo mwisho umemaliza,mabogus aina ya William wamejaa ktk utawala wa nchi,na hii ni moja ya sababu kubwa majirani zetu wameanza kututenga kama kutustua kwamba mnatawaliwa na watu wajinga ambao hawana uwezo wa kuongoza taifa tajiri kwa rasilimali,lakini wananchi wengi masikini!
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais,

kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.
weye sio mzima kabisaaaaaaa; upelekwe milembe sasa hiv, la sivyo utasabbisha majanga kwa wanainch.
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz

Hivi kwanini mtu ukiwa ccm hata ungekuwa na akili zako zinakuwa hazifanyi kazi? Nyinyi ni karaha na aibu ya nchi hii.
 
- Una maana failure ya Chadema kushindwa kushika madaraka au? ha! ha!

Le Mutuz

Mkuu inasemekana ile miaka nne uliokuwa kule Kwiro Secondary School ilipotea bure ukatoka na kibuyu hivi ni ya kweli hayo?Binafsi siamini kwasababu inasemekana watu wenye ndonga (vichwa) kubwa kama yako huwa wana akili sana.
 
huku umepotea bana.leo bado sojaona post ya mbebs yeyote kule fb kumbe uko huku!pls funga mjadala hapa rudi kule fb mabs wako wanakisubiri bana.hapa wapo watu wanaojadili hatma ya nchi yetu aka sirias people.pls wahi kule fb fans wako wanakusubiri



Sweet girl

Umemjibu vizuri sana huyo boya W J Malechela sio kosa lake ila ni mfumo anaoutumikia akili yake bado iko enzi za miaka 47 mumsamehe tu

Ni jadi yao jiulize kwa nini Mwalimu alimuita baba yake kwamba ni Muhuni? Ni kawaida yao kuanzia mzee mwenyewe Malechela,akaja Lusinde,kuna huyu W J Malechela na Job Ndugai sasa unakuta kwamba Mkoa wa Dodoma ndio kati ya Mkoa unatoa watu machizi ambao ni omnipotent na wana inferior complex hivyo ni wa kuhurumiwa muda mwingine hawajui cha kufanya
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

tatizo lenu maccm ndilo hilo mara zote mnapenda kujadili watu badala ya hoja iliyoko mezani udhaifu huu umeanzia bungeni, sehemu ambayo badala hoja wao hujadili watu hususani chadema

leo akina Bulembo badala ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya katiba mpya, anatumia pesa nyingi kuandaa mikutano ya kuwasema watu - personal attack

hata wewe tunayeamini labda umeelimika kumbe ni walewale
 
Le Mutuz sikutarajia kuwa utakuwa na uelewa finyu kiasi hicho; alichosema jaji Warioba, ni watu wajadili rasimu iliyotolewa na tume na si wajumbe wake! Sasa kwa uelewa wako; ni bunge lipi la katiba lililojadili rasimu na ilitolewa na tume ipi? Hivi mpaka leo huwezi kutofautisha kati ya rasimu ya katiba na mswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba?
 
- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz
Ulevi huu wa madaraka ndio utakaosababisha damu kumwagika. Ndio maana mliamua kutoa ule mwongozo wenu kwenye Mabaraza ya Katiba ili mchakachue Katiba? Chama chenye wanachama wasiozidi milioni 3 kitaamua hatma ya wananchi milioni 44? Hakuna Chama chenye hatimiliki na nchi hii, sio CCM wala Chadema. Vyama vitakufa kama tutakavyokufa mimi na wewe ila Tanzania itadumu daima dawamu. Mnakera sana nyie CCM
 
maccm wote Mungu amewanyima burasa sishangai huyo mjinga kumpinga warioba akili za kuku hizo.
 
maccm wote Mungu amewanyima busara sishangai huyo mjinga kumpinga warioba akili za kuku hizo.
 
Wewe na Bulembo ni waganga njaa. Haujisikii vibaya kuongozwa na Bulembo ambaye mara kadhaa kabwagwa chini uchaguzi wa udiwani Kijitonyama; Kiboko yake ni Juma Ulole Ulole, Bulembo ni darasa la VII halafu CCM mnampa madaraka mtu mwenye shule ndogo

'Makamu wa Rais' wa Slaa katika uchaguz wa 2010 hakuwa na walau Cheti cha Pre Form One! Ina maana kama Babu angeupata Ukikwete halafu akadanja kabla ya 2015 tungeongozwa na Binadamu asiejuwa walau Definition yA Definishen ya ' URAIS'!
 
Back
Top Bottom