Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

Mkuu asungwilemwaifunga ndugu yangu MADORO kajitahidi kwa kadri ya uwezo wake katoa mifano ya majaji waliosoma na Jaji Mkuu,katoa angalizo zuri sana kwamba mtu anaweza kuanza darasa la kwanza na miaka minne zingatia hiyo ilikuwa mwaka 1956 !.Mengine ata wewe unaweza kusaidia si kukosoa taarifa muhimu.

Chanzo cha taarifa ya Jaji huyo hakiwezi kuwa Chuo kikuu peke yake, hata shule ya msingi alikosoma zipo, shule ya sekondari, High school kote unaweza kupata taarifa hizo. Mtoa uzi kama angekuwa makini asingeishia chuo kikuu kitivo cha sheria peke yake.
 
Last edited by a moderator:
Chanzo cha taarifa ya Jaji huyo hakiwezi kuwa Chuo kikuu peke yake, hata shule ya msingi alikosoma zipo, shule ya sekondari, High school kote unaweza kupata taarifa hizo. Mtoa uzi kama angekuwa makini asingeishia chuo kikuu kitivo cha sheria peke yake.

Yeye kwa uwezo wake amefika chuo kikuu, kama unaweza kufuatilia shule ya msingi, sekondari na a level itakuwa vizuri kuliko kumtwisha lawama zisizo na msingi wowote.
 
Suala la mtoto mdogo wa miaka 4 kuanza darasa la kwanza kidogo linawezekana miaka hii,ila kwa miaka ya nyuma hilo jambo lilikuwa gumu kweli kweli.
Hivi,uadilifu wetu kama taifa u wapi?
Kama mtendaji mkuu wa idara ya kutoa haki kisheria anadanganya umri,our destiny is at stake.
 
Inawezekana ikawa kweli ukizingatia wale walioachwa waliambiwa raisi ameangalia umri na afya na si uzoefu. Walipochunguza wakagundua afya ya chande ni mgogoro tupu, then wakashikilia la umri. Yaleyale ya spika ili wamteuwe wanayemtaka.
 
Mtoa mada, kwa nini umeamua kufuatilia suala hili mkuu!
 
Post hapa zinapotea ukiwa humu humu jamvini. Ngoja nilog out kabla hawajanikaribia zaidi!
.
 
Kama wangekuwa wanaangalia suala la Afya ya Majaji. Rais anatuhumiwa kuwateua wagonjwa kuwa majaji ili wapate fursa ya kwenda kutibiwa India. Ugonjwa ni sababu ya mtu kupumzishwa au kustaafishwa, lakini kwa JK limekuwa ni suala la kuongezea watu. Hebu Majaji pamoja na kuwa suala hili linawagusa, jitokezeni semeni uteuzi wa jaji Kulwa Masaba na jaji Madina Muro walioteuliwa wakiwa wagonjwa baadaye wakafariki. Au Jaji Mwendwa Malecela tangu ateuliwe mwaka 2006 ni mgonjwa anapata favour ya kwenda India kuhudhuria matibabu na hadi sasa hajawahi kusikiliza hata kesi moja. Ikumbukwe kuwa jaji Mwalusanya kwa mazingira yanayofanana mwaka 1994 alipata stroke, ila alipelekewa karatasi ili asaini kuwa anajiuzulu Ujaji. moderators imekuwaje mbona kama tulisoma kuwa Jaji Mkuu Othmani Chande ni ndugu wa damu wa Rashid Othman Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa taifa, lakini muda mfupi hatuoni maneno hayo?. Muhimili wa Mahakama nao sasa tutautilia shaka
 
Yeye kwa uwezo wake amefika chuo kikuu, kama unaweza kufuatilia shule ya msingi, sekondari na a level itakuwa vizuri kuliko kumtwisha lawama zisizo na msingi wowote.
. Uzi sio wangu na sipendi na sina kawaida ya kudandia kazi ya mtu. Kama ameamua kutoa taarifa anapaswa kutoa taarifa iliyokamilika bila ya kuacha kipengere chochote. Tusizungumzie ushabiki, tuzungumzie uchambuzi unavyopaswa kuwa. Tusitoe maada yenye mapengo tukitumainia watu wengine kuziba. Mchango wangu katika maada ni kumwonyesha mtoa maada vyanzo vingine vya taarifa anakoweza kutoa ili kuikamilisha maada kiutafiti zaidi. Mtu anayedhani kuwa hizi ni lawama hajangalia kwa maana ya academic criticism anachukulia kama personal attack jambo ambalo sio sahihi. Sitoki nyumbani kwa Jaji Chande Omari wala sijasoma naye lakini pia sikuwa na nia yoyote ya kufuatilia maisha yake. Maadam mtoa maada kaitoa humu jamvini nimevutiwa nayo ndiyo maana nikamshauri atafute taarifa zaidi kutoka kwenye vyanzo vingine ili kuipa uzito, mvuto na ukweli zaidi bila ya kuacha nafasi kwa msomaji ya kuhoji au kupendekeza jambo lolote. Nimependekeza kwa sababu Uzi wake unatoa mwanya wa kufanya nilivyofanya. Ugomvi unatoka wapi? Nadhani mtoa uzi na waungaji mkono wa uzi huu walitegemea kila mtu apokee taarifa hii pasi na kuhoji kama walivyoipokea wao. Hapana
 
Asungwile Mwaifunga, tunapoleta mjadala kwenye JF, tunategemea wewe kama unatoka Kijiji alichosoma Jaji Mkuu, au kama upo mahalai alipozaliwa unasaidiwa watanzania wengine kujua.

Huu utaratibu wa kufikiri kuwa mpaka mtu aende kila mahali unakuwa hauna maana, nimeenda UDSMA, HAKUNA, WEWE ULIYEKO KIJIJI ALIKOZALIWA, AU WEWE ULIYESOMA NAYE AMBAYE HABARI ZENU SASA NI SIRI, NJO jamvini waambie watanzania Jins Jaji Mkuu alivyoanza darasa la kwanza akiwa na miaka 4, je kwa nyakat zile iliwezekana.

Usijeshangaa utakapo ambiwa alikuwa na akili ya pekee ndiyo maana wazazi wake walimwahisha shule akiwa na miaka minne wakishindwa kabisa pa kutokea...Ama kwabusara tulizonazo tuliona hakuna binadamu mwingine Tanzania anayeweza kuishika hiyo nafasi maana ni nyeti sana na wenye uwezo wa kuitumikia ni wachache sana hivyo kati ya hao yeye kwa wakati huu ndiyo ana qualify....Hiyo ndiyo nchi yetu ambapo akili pekee ya kuvumbua ni ya mambo yanayohusiana na uovu!
 
Hapo ndo huwa namkubali JK. Anakupa cheo huku anajua unanuka mavi, ukimzingua tu anakuanzishia soo..! Hapo ni nidhamu mwanzo mwisho..! Aliweza kum-set EL sembuse jaji mkuu..?

Duuh hii kali aise (CDM tena nini? Huuhh! huyu Lema kafanyaje tena? Just thinking loudly!)....Acha na wao wakome kwanini wanakubali kubebwabebwa bila kuangalia uhuru wao utaingiliwa kwa kiasi gani kwakukubali favours zenye strings za kukuvuta pale utakapo taka kuwa free katika profession yako?

Wake up Tanzanians....Hiki chama ndiyo maana katika nafasi nyeti inaweka watu ambao wanajua issues zao za kuwabana na wakitaka ku-default tu ndiyo hapo utasikia fulani si raia, mwingine fisadi ooh ana account Swis etc..Lakini tujiulize ni kwafaida ya nani hasa? Sisi raia kila siku mwendo wa kubadilishiwa tu tamthilia hatuchoki? Ifike wakati hivi vitu tuviwekee kikomo few people cannot destroy the peace and harmony of this country...

Its just a matter of seconds not even minutes I smell a great fall of mibuyu mikubwa!
 
jamani nyosheni maelezo kuwa kipindi hicho kuanza la kwanza ukiwa na miaka 4 ilikuwa haiwezekani kwani hata miaka ya 80 ulikuwa ukitaka kuanza unaambiwa ushike mkono sikio kwa kupitisha mkono wako kichwani..kifupi kama huna mika nane na kuendelea ilikuwa haiwezekani..tumchunguze hata jk utakuta naeyumo maana tuliambiwa ni kijana mwenzetu..
 
kuna jitu linaleta ubishi wa kijinga eti halinatabia ya kudandia uzi wa watu na uzi huu siyo wake..kama hunapoint za kumtetea huyo mme wako baki msomaji maana unaandika maelezo mengi halafu ni kinyesi kitupu na jina lako kinyesi kitupu..
 
Tunatembea kipindi kigumu lakini tusipoogopa mateso ,vifo, na yote yanayoweza kutupata kwenye bonde la uvuli wa mauti tutashinda,maana hakuna amani kwa mwovu.Wataficha takwimu lakini hawataushinda muda wa historia kusema ukweli!
 
TISS wataficha mpaka lini wakati ndiyo huu na ukweli utajulikana
 
Jaji Chande tumesoma wote Aga Khan Secondary School (Tambaza). Kama ni utafiti basi mnaweza kuanzia hapo. Kama miaka ya kustaafu ni 65 basi Jaji Chande hajafikia umri huo.
 
Back
Top Bottom