Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

Kanyaga twende tutafika tu jamani. Msikate tamaa bandugu

Ni afadhali kudanganya umri kuliko kuforge vyeti, wangapi wamebumburushwa na vyeti feki na hadi leo bado wanadunda, kama kungekua na haki hasa kusingekua na haja ya kua na naibu waziri tulienae, angeshikiwa bango mpaka akaachia ngazi lakin bado anadunda, twendeni mbele kwa sababu nyuma hakurudiki tena tumefika mbali
 
Mahakama ya Rufaa wanastaafu wakiwa na miaka 65 na wala sio 60!

sasa nini kili mfanya adanganye umri wake au anataka awe jaji kwa miaka mingi iwezekanavyo..anabahati amejitoa kesi ya Lema tunge funga kwaajiri yake na boss wake wa magogoni..
 
mkuu NgomaNgumu ndiyo watanzania tulivyo likija jambo tunashadadia siku mbili akipiga chafya kikwete tunaanza kujadili chafya ya kikwete tunaacha hoja ya msingi...hata hili litapita tu
 
Last edited by a moderator:
Asungwile Mwaifunga, tunapoleta mjadala kwenye JF, tunategemea wewe kama unatoka Kijiji alichosoma Jaji Mkuu, au kama upo mahalai alipozaliwa unasaidiwa watanzania wengine kujua.

Huu utaratibu wa kufikiri kuwa mpaka mtu aende kila mahali unakuwa hauna maana, nimeenda UDSMA, HAKUNA, WEWE ULIYEKO KIJIJI ALIKOZALIWA, AU WEWE ULIYESOMA NAYE AMBAYE HABARI ZENU SASA NI SIRI, NJO jamvini waambie watanzania Jins Jaji Mkuu alivyoanza darasa la kwanza akiwa na miaka 4, je kwa nyakat zile mi mbona nlianza std 1 nkiwa na 3yrs hamsemi?
 
Hapa kama anavyosema Jasusi kwamba umri wa kustaafu ni miaka 65 kwa Jaji Mkuu,na kama alizaliwa 1952 basi ana miaka 60 sasa kwa maana hiyo hajafika umri wa kustaafu,ila bado kuna jambo linajificha kama anastaafu 2016 itakuwa anawahi sababu anatakiwa kustaafu 2017.
Je,ilikuwaje aanze shule na miaka miNNE?
Kwanini astaafu mapema kabla ya muda wake?
Kwanini UDSM wanaficha taarifa zao kitivo cha Sheria mwaka huo?
Kama nimekosea mahesabu nipo tayari kukosolewa
 
Last edited by a moderator:
Akamatwe nae maana kwa miaka ile ya zamani kuanza drs la kwanza na miaka 4 ilikuwa ngumu saana labda kama alikuwa mtoto wa Chifu
 
Jaji Chande tumesoma wote Aga Khan Secondary School (Tambaza). Kama ni utafiti basi mnaweza kuanzia hapo. Kama miaka ya kustaafu ni 65 basi Jaji Chande hajafikia umri huo.

mbona unatoa taarifa nusu nusu? Mmemaliza mwaka gani? Mlikuwa sawa au ye alikuwa mdogo kuliko wote?
 
Wakuu kwa mahesabu yangu inaonekana alianza shule akiwa na miaka mitatu!

Kivipi?
Alizaliwa 1952 na akahitimu 1974 chuo kikuu hivyo alihitimu akiwa na miaka 22 yaani (1974-1952), sasa basi;

*Elimu ya darasa la nane(Miaka8)
*Ordinary level(Miaka 4)
*Advanced Level(Miaka 2)
*Mafunzo ya JKT(Mwaka 1)
*Bachelor of Law(Miaka 4)

***Jumla miaka mpaka kuhitimu (8+4+2+1+4)=19

***Miaka ya kuanza shule
(22-19)=3
 
mbona unatoa taarifa nusu nusu? Mmemaliza mwaka gani? Mlikuwa sawa au ye alikuwa mdogo kuliko wote?

Nimefanya makusudi. Nadhani Chande sasa hivi ni 62 years old kwa hiyo bado ana miaka mitatu kabla ya kustaafu. Does that help?
 
27th December 2010

JajiMohamed.jpg



The new Chief Justice Mohamed Chande Othman

President Jakaya Mrisho Kikwete has appointed Judge Mohamed Chande Othman the new Chief Justice with effect from tomorrow.

The appointment follows the retirement of Chief Justice Augustino Ramadhani which becomes effective today.
Before his new appointment, Judge Othman, 58 (pictured) served as judge in the High court of Tanzania and the court of appeal for seven years.

He is a reputed independent expert in human rights issues.

He graduated with Bachelor degree in law (LLB) from the University of Dar es Salaam (UDSM) and later earned a Masters in law from the University of Webster, Geneva, Switzerland.

He is currently a senior adviser to the United Nations on Human Rights.

As a former chief of the International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) and ex-prosecutor of East Timor’s UN administration, he boasts of rich international experience and exposure in the management of judicial affairs.
He will be sworn in at 10.00 am today at State House grounds in Dar es Salaam.

Justice Ramadhani, who has attained the official retirement age of 65, was appointed CJ in 2007 UDSM bade him farewell on Friday.

Traditionally, it is the outgoing CJ who recommends three people for appointment from amongst judges of the Court of Appeal to the President, who, in consultation with the National Intelligence and Security Service (TISS) makes his pick.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
1964-67. Ila mimi nilihamia Tambaza 1965 kutokea Bwiru. Nadhani agewise he is a year or 2 younger than me.
Mkuu kama ni hivyo maana yake mleta mada yuko sahihi kabisa, na wewe uliyesoma naye unathibitisha kuwa alisoma O'level kati ya 1964-1967 which exactly ndivyo mleta mada alivyosema.

So now piga mahesabu vizuri kama Chande alizaliwa 1952, akahitimu darasa la nane mwaka1963, Ili aanze O' level 1964, sasa itakuwa alianza shule na miaka mingapi?
 
Mmh kazi ipo JF...

Ina maana huyu Mzee anamzidi Le Mutuz miaka sita tuu?

Naanza kunusa harufu mbaya kwenye kesi ya Lema...
Great Thinkers, connect dots...issue za Lisu na majaji...kuingia na kutoka kwa CJ kweny kesi ya Lema...kuibuka kwa hili kasheshe la Birthday party ya CJ.....

Ni mawazo tu, masela msijenge chuki.....
 
Mkuu kama ni hivyo maana yake mleta mada yuko sahihi kabisa, na wewe uliyesoma naye unathibitisha kuwa alisoma O'level kati ya 1964-1967 which exactly ndivyo mleta mada alivyosema.

So now piga mahesabu vizuri kama Chande alizaliwa 1952, akahitimu darasa la nane mwaka1963, Ili aanze O' level 1964, sasa itakuwa alianza shule na miaka mingapi?
Nadhani tatizo tunalohitaji kufumbua ni, je, alianza shule akiwa na umri gani? Mimi nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka saba. Huenda yeye alianza akiwa na umri wa miaka 5 au 6. Hapo ndipo kwenye kitendawili.
 
good research
isishie kwa jaji mkuu pekee
ihusishwe na viongozi wengine ili serikali
ijue umuhimu wa transparency ktk utendaji wake
 
Back
Top Bottom