Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
0
Katika Kile kinachoonekana kuwa Uadilifu katika Tanzania sasa ni msamiati katika kila Mhimili, Jaji Mkuu Chande Othmani ameghushi umri ili abaki katika ajira hadi mwaka 2016.

Jaji Chande Othman, alihitimu Shahada ya kwanza ya Sheria mwaka 1974, na kwa mujibu wa taarifa za sasa zinaonyesha kuwa alizaliwa mwaka Januari 1, Mwaka 1952. Kama Takwimu hiyo ni ya kweli, maana yake Jaji Mohamed Chande Othmani alianza darasa la kwanza mwaka 1956 akasoma darasa la nane mwaka 1963, Mwaka 1964 hadi 1967 alimaliza Sekondari (O'level), ambapo kwa hesabu za miaka ile, 1968 alianza kidato cha Tano na Sita na kumaliza mwaka 1970, na Mwaka 1971 akahudhuria Jeshi kwa mwaka mmoja (JKT). na 1972 hadi 1974 ndo akahitimu shahada ya sheria.

Tujiulize yafuatayo:
Je inawezekana Mtu akaanza darasa la kwanza akiwa na miaka minne?.

Tumefuatilia habari zake Kitivo cha Sheria chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hatujapata taarifa zozote za Darasa zima lililohitimu 1974, taarifa zote zimefichwa. Lakini baadhi ya majaji wenzake waliosoma nao darasa moja wanastaafu rasmi mwakani.

Tuwaulize wanadarasa wenzake tujue sakata hili, Prof Costa Rick Mahalu, sio jaji, ila Majaji wenzake ni Dr. Bwana ambaye atastaafu 2013, Jaji J. Msofe, Jaji Masati, jaji B. Luanda, wote watastaafu mwaka 2013. Wengine ambao alisoma nao ambao wameshastaafu ni R. Sheikh, na V.K. Lyimu.

Lakini pia Utata unazidi kwanini habari za darasa zima Kitivo cha Sheria mwaka 1974 Zikawa hazipatikani
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,809
2,000
Vyeo vitamu jamani alishajua wapi pa kuficha data zake maana anataka afie pale pale kwenye kidonda!!
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
24,082
2,000
Kuna uwezekano mkubwa ila cha kushangaza sekta zote mhimu hapa nchini undugu umejaa
 

bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,572
1,250
Chanzo cha taarifa ya Jaji huyo hakiwezi kuwa Chuo kikuu peke yake, hata shule ya msingi alikosoma zipo, shule ya sekondari, High school kote unaweza kupata taarifa hizo.

Mtoa uzi kama angekuwa makini asingeishia chuo kikuu kitivo cha sheria peke yake.
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,576
1,195
ukishanga hiko litakuja lingine la ajabu zaidi ya hapo Tanzania ni kisiwa cha ubakaji wa haki na wenye nacho watabaki kuwa nacho
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,540
2,000
namhukumu kwenda jela miaka mitano, akitoka viboko kuingia viboko kumi, kutoka viboko kumi na viwili akamuonyeshe mkewe heeeuuuuuuuiiiiii ndio nchi yetu tutafanyaje!!!
 

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
0
asungwilemwaifunga, tunapoleta mjadala kwenye JF, tunategemea wewe kama unatoka Kijiji alichosoma Jaji Mkuu, au kama upo mahalai alipozaliwa unasaidiwa watanzania wengine kujua.

Huu utaratibu wa kufikiri kuwa mpaka mtu aende kila mahali unakuwa hauna maana, nimeenda UDSMA, HAKUNA, WEWE ULIYEKO KIJIJI ALIKOZALIWA, AU WEWE ULIYESOMA NAYE AMBAYE HABARI ZENU SASA NI SIRI, NJO jamvini waambie watanzania Jins Jaji Mkuu alivyoanza darasa la kwanza akiwa na miaka 4, je kwa nyakat zile iliwezekana.
 
Last edited by a moderator:

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Nilifikiri umri wa kustaafu wa jaji mkuu ni miaka 5 zaidi ya hawa wengine wa rufaa.

Sidhani kama utakuwa sahihi, umri wa kustafu kwa jaji mkuu ni sawa na majaji wa mahakama ya rufaa. Hakuna ziada ya miaka 5 kwa jaji mkuu ndugu yangu.
Ukitaka kujiridhisha fuatilia umri wa jaji mkuu mstaafu wa hivi karibuni, Augustino Ramadhani.
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Kuna kila dalili za ukweli kuhusu hili.
Kuna jamaa wa TISS kanitonya hiyo issue ipo na Usalama wa taifa walikuwa wanatafuta namna ya kuificha sana tangu Lissu alipoanza kufumua uozo wa baadhi ya majaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom