Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.

wadau huu ujumbe si kwa dpp wala werema,unaenda kwa watu wengi sana,na hii ni ishara kuwa hawa wanasiasa wanawaudh sana wanasheria wanaotambua wajibu wao
 
Poleni magamba. Tegemeo lenu kuu lilikuwa ni polisi na mahakama. Lakini mahakama ndo hiyo tena! Sasa mmebakiza polisi. Hadi kufikia 2015 hata hao polisi wakuwa wamewachoka!
 
gharama zote walizoingia ,Pamoja na kupotezewa muda, inabidi wafungue kesi ya madai.
 
Tukipata Majaji Kumi kama hawa, nchi hii watu tutaheshimiana
 
''Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine. '' HAYA MANENO NINAANDIKA KATIKA GARI YANGU ,, yameniosha sanaa na iwe kauli mbiu ya CDM

...kumbuka ata mzee Nelson Mandela huko Afrika kusini makaburu walimfunga kwa kesi ya gaidi...
 
''Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine. '' HAYA MANENO NINAANDIKA KATIKA GARI YANGU ,, yameniosha sanaa na iwe kauli mbiu ya CDM

One man's terrorist is another man's freedom fighter. Perfect. Lakini Mwigulu au big baby Nape wanaweza kuelewa hili?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.
 
Ama kweli mwisho wa ubaya ni aibu. Hasa CCM kwa kuumbuka hivi wanajionyesha wapi tena. Kuna haja ya watuhumiwa kulindwa endapo huyu DPP hatendi haki. Mfano hapa ilipaswa walipwe fidia kwa namna walivyotendewa.
 
Ahsante Sana Jaji
Sikupongezi kwa sababu ya hukumu maana kama Mwanasheria hukumu nilishaiona kitambo kwa kufuatilia tu mwenendo wa kesi. Nakupongeza kwa somo ulilotoa kwa hao waendesha mashtaka wanaopoteza muda na Rasilimali za Taifa kufungulia watu kesi zisizo na Kichwa wala miguu. Na sasa waelewe kabisa nakunuu,,,ANAYEWEZA KUWA GAIDI KWAKO LABDA NI MPIGANIA UHURU KWA MWINGINE..
Naamini wamekusikia na wamekulewa,,,CHADEMA ni mpango wa Mungu wandugu

Kinachohitajika sasa ni kumfungulia mashitaka dpp kwa kuchezea kodi zinazokamuliwa kutoka kwa walalahoi kwa kufungua na kuendesha kesi za kijinga kama hizi!!
Not sure kama hii kitu inawezekana kisheria... lakini, nothing is impossible under the sun! Mikakati iwekwe na wanasheria makini ili huyu mtu afunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi... hatuwezi kuwa tuaaangalia tuu jamaa wanachezea kodi tunazolipa kwa kutekeleza maelekezo ya chama mfu!!
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.

Hivi huyu DPP Elieza Feleshi anatenda hivi akiwa PHD holder je angekuwa bado ana digrii moja angekuwaje?
 
Kama ningekuwa na uwezo, nisingeruhusu kodi yangu itumiwe na hii ofisi ya DPP. Ni hasara ya jumla. Kama taifa hatupati chochochote kutoka kwenye ofisi hii.
 
Back
Top Bottom