Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.

Kwa maoni yangu naona kama alidhamilia kumtukana DPP hivyo sitashangaa nikisikia lolote limempata huyu Jaji
 
Jaji , wewe ni mtenda HAKI ambayo ndiyo msingi wa AMANI , Mwenyezi Mungu akulinde , tusije ambiwa kwamba umeokotwa PORINI .
 
''Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine. '' HAYA MANENO NINAANDIKA KATIKA GARI YANGU ,, yameniosha sanaa na iwe kauli mbiu ya CDM
 
wewe judge wewe, haya shauri yako , yaani ina maana pickup inavuta HDV Yenye mzigo
 
Hivi Feleshi alipata ile Laptop yake au bado kwani inaoonyesha ndio ilikuwa na Notes zilizompa uanasheria!!!

Nadhani akili yake yote ilipotea na ile Laptop. Huyu Ngosha anatia aibu sana, kama wangekuwa wanampima kwa kushinda na kushindwa kesi sidhani kama angekuwa ofisini hadi leo. Ona sasa aibu yake hii kikazi, mwenzie Mwigulu Nchemba ni mwanasiasa tu, toka jana kaja na SPIN ya kutetea ajira za vijana
 
daaah kazi kweli kweli ....hawa ndo majaji tunaowataka katika nchi hii
 
Yule bwana Tesha aliyemwagiwa Tindikali iltoka juu kama mvua, hakuna mtu aliyehusika, over.
Wachaga noma kwa Rushwa.
Alimwagiwa na makada wenzake wa CCM baada ya kuwadhurumu mugawo wa rushwa! polisi wanaogopa kuwakamata wahusika kwa kuwa ni wafuasi wa CCM kama ulivyo wewe mwehu!
 
Mungu ampe Maisha marefu huyu jaji; asisakamwe tu kwa kuwa mkweli. na wengine wafuate nyazo hizi;
 
Wanaharibu mali ya umma na kuchezea pesa yetu, utakumbuka watuhumiwa walisafirishwa kwa ndege
 
dpp anaizalilisha saana taaluma yake kwa kukubali kutumika kama ndomu na wanasiasa
 
DPP, CCM na wenzao wanapaswa kuwalipa kina Kileo fidia kwa kuwabambikia kesi ya uongo na kuwapotezea muda.
 
Back
Top Bottom