Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.
Mikakati ya kisiasa ya CCM pamoja na propaganda zao zimeshindwa kutimiza lengo lake. Pamoja na hayo, UONGO, na NIA OVU, katika kesi hizi zinawafanya watu wenye integrity yao kuonea aibu kuwa ndani ya chama kinachoendeshwa kwa UONGO na NIA OVU.
 
A big up justice Lukelelwa; DCI cum DPP Lameck "Savimbi" Mwigulu Nchemba sina uhakika kama amekuelewa vizuri maana kama anaweza kusahau umri wake mwenyewe (1978 - 2013 = 38yrs!!) hatuna sababu ya kuamini somo hilo la siku moja kama atakuwa ameelewa au amepita kama kuingiza n'gombe kweye josho lisilo na dawa ya kupe!!
 
Huyu Dr Eliezer Feleshi ni janga la kidunia, anaidhalilisha sana hiyo ofisi ya Mwendesha mashtaka. Kwa kuwa hakutegemea kama atapata hiyo kazi na huenda alitumia ushirikina kuipata, anajikuta hawezi kukataa kitu akiambiwa na Mwigulu Nchemba. Nashindwa kuelewa hiyo PhD aliisomea ya nini kama anashindwa hata kuelewa definition ya neno ughaidi, cha kushangaza juzi walikuwa Dodoma wanagawana posho kwenye mkutano wa kujadili kwa nini wanashindwa kesi kibao mahakamani. Eliezer Feleshi anaingia katika kundi la watanzania wa kuchekesha zaidi kwenye fani yake, he is a JOKE DPP. Sidhani kama anaweza kuwaambia wanae kuwa mimi ni mwendesha mashtaka mkuu wakati hajui definition ya Ughaidi, aibu aibu aibu kwa wasomi wa nchi hii kuendeshwa na wanasiasa. Yote sababu ya njaa na insecurity.
 
nawalaani wamwagia watu tindikali. huo ni uovu mbaya sana unaopaswa kukemewa kwa hali zote
 
Hii nchi bwana ndio maana wakati mwingine inabidi mtu uwe kimya tu maana ukifikiria sana unaweza kupata stress za ajabu inaonyesha ccm kuna vihiyo wengi sana wameshindwa hata jinsi ya kushauriana, hakuna wanasheria kabisa? ujinga kama huu utaendelea mpaka lini?
 
Somo siyo uingie darasani. Kuna elimu ya aina tatu, ile ya kupata darasani, duniani na ......Tafakali.......!
 
Huyu jaji anaonekana kaenda shule na kuelewa. Sio kama yule wa kesi ya Lema. Ujinga wa akina Mwigulu wa kushabikia ugaidi bila kujua maana yake ndio unaoharibu sifa ya nchi hii. Sijui ni nani aliamua kuidharaulisha CCM kwa kumpa cheo nyeti mtu kama Mwigulu. Badala ya kufanya kazi za chama yeye amekuwa mtengeneza mikanda ya ugaidi na kushinikiza kesi zisizokuwa na miguu wala kichwa.
 
Safi sana. Liserikali limejigeuza kuwa genge la wajinga hayo ndo matokeo yake; kila kesi mnayofungua mahakamani mnagalagazwa tu. waswahili walisema kweli, wajinga ndio waliwao.
 
Ofisi ya DPP imenajisiwa kwa hizi kesi za kubambikia watu
 
Back
Top Bottom