Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Nimeipenda sana hii ya nape, kumbe anaitwa "big baby". Ila huyu jaji hapati cheo tena kwa kikwete.

Dunia ya Tz haiishi vibweka. Kumbe kuna ma big baby? Basi ma small baby hayatakosekana kabisa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hiyo credit kubwa kwa CDM.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mimi nilisema mara nyingi sana hapa jamvini kuwa maccm yanashindwa kutofautisha ugaidi na jinai yaani terrorism na crime. Sasa wao walikimbilia ugaidi sababi halina dhamana.maccm nima pinda sana.basi tuu..huyu kikwete amalize muda wake ajiondokee hana maana yoyote.
 
Hivi hawa waendesha mashtaka, wanapokea maagizo kutoka kwa nani? DPP au MWIGULU?
 
Somo gani sasa ambalo limetolewa.

Somo kuu hapo ni kwamba tafsiri ya neno gaidi ni pana sana. Tusi itane tu haraka haraka gaidi. Unayemuita wewe gaidi kwa wenzako anaitwa mpigania uhuru au ukombozi. Kuna wakati Mzee Nelson Mandela aliwahi kuitwa gaidi na serikali ya makaburu!
 
You are right! Miaka ya '60 ANC iliwahi kutangazwa kama kundi la kigaidi. Japo kilianzishwa Mwaka 1912 ilidaiwa kwamba "ugaidi" wa ANC ulianza mwaka 1961 na kama sikosei ni kipindi hicho Nelson Mandela alikatiwa kifungo cha maisha jela kabla ya kuachiwa miaka ya '90 na hatimaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini mwaka 1994.

Taarifa zaidi kuhusu UGAIDI wa ANC zinapatikana hapa: Terrorist Organization Profile - START - National Consortium for the Study of Terrorism and Responses to Terrorism
 
Na bado hatujapata katiba mpya itakayoainisha njia bora za kuwapata majaji. Watakoma wenyewe
 
Nashindwa kuelewa kwanini DPP anakosa uelewa wa sheria. Nina mashaka na elimu yake.
 
Jaji alifanya maamuzi yake kwa kufuata sheria,lakini akae akijua nchi hii huwa viongozi wake hawataki kusikia ukweli hivyo ajue wakati wowote ama atapoteza kazi yake au ataingia kwenye hujuma kubwa ya afya yake.ushauri wangu ajilinde sana.
 
nawalaani wamwagia watu tindikali. huo ni uovu mbaya sana unaopaswa kukemewa kwa hali zote

Tindikali na ugaidi wapi na wapi, walaaniwe magamba wanao ongoza kuchafua nchi yetu kwa maslahi yao binafsi, walianza na udini, ukabila, ukanda na sasa wamehamia ugaidi, believe me haya yote yatawarudia
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.
Asante sana jaji kwa kusimamia ukweli Mungu akulinde lakini sina imani na maccicciemu maana hata kuua yapo tayari ili mradi yabaki madarakani
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.

Hivi unammwagia bnadamu mwenzako acid unasema huo sio ugaidi,unaratibu kumtesa mtanzania mwenzako napo unasema sio Ugaidi?Sheria inaweza pindishwa kwa nguvu ya mawakili waliopo bt ukweli utabak pale pale wats goes around,,,,,,,,,,,,!
 
Kuna majinga yatakuja kujipa moyo humu, tulishinda kwa rwakatare, tumeshinda tabora ,tulishinda arusha,na tutashinda daima, kamwe haki ya mtu haipotei,ccm bye bye.
 
Back
Top Bottom