Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Jaji atoa Somo la UGAIDI kwa DPP na Wanasiasa

Hivi huyu Feleshi au Fresh udokta wake ni wa kupewa kama wa JK au wa kusomea?
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.

Ahsante Sana Jaji
Sikupongezi kwa sababu ya hukumu maana kama Mwanasheria hukumu nilishaiona kitambo kwa kufuatilia tu mwenendo wa kesi. Nakupongeza kwa somo ulilotoa kwa hao waendesha mashtaka wanaopoteza muda na Rasilimali za Taifa kufungulia watu kesi zisizo na Kichwa wala miguu. Na sasa waelewe kabisa nakunuu,,,ANAYEWEZA KUWA GAIDI KWAKO LABDA NI MPIGANIA UHURU KWA MWINGINE..
Naamini wamekusikia na wamekulewa,,,CHADEMA ni mpango wa Mungu wandugu
 
Baadhi ya majaji wameshasoma alama za nyakati. Na sasa wameamua kutumikia taaluma yao.
 
Huyo jaji amewapa vidonge vyao,safi sana warudi darasani kwanza make wamevuliwa nguo mchana kweupe.
 
A big up justice Lukelelwa; DCI cum DPP Lameck "Savimbi" Mwigulu Nchemba sina uhakika kama amekuelewa vizuri maana kama anaweza kusahau umri wake mwenyewe (1978 - 2013 = 38yrs!!) hatuna sababu ya kuamini somo hilo la siku moja kama atakuwa ameelewa au amepita kama kuingiza n'gombe kweye josho lisilo na dawa ya kupe!!

ana fake umri, sio kuwa alisahau, unaweza sahau umri wako!
 
Kifo cha nyani miti hutereza, ccm kazi mnayo kila mwenye akili anakaa pembeni damu za watanzania zinawageuka taratibu.
CHEZEA MAMBO MENGINE SIO DAMU. NA BADO KILA M2 ATAWAGEUKA!
 
Hivi Feleshi alipata ile Laptop yake au bado kwani inaoonyesha ndio ilikuwa na Notes zilizompa uanasheria!!!
 
Baadhi ya majaji wameshasoma alama za nyakati. Na sasa wameamua kutumikia taaluma yao.
hii ndio hali halisi kweli kabisa wapo majaji wamebadilika kabisa maana wameona chama kilichopo madarakani kina dalili zote za kuwa chama cha upinzani 2015
 
Yule bwana Tesha aliyemwagiwa Tindikali iltoka juu kama mvua, hakuna mtu aliyehusika, over.
Wachaga noma kwa Rushwa.
 
Ukiwa gamba hata kama una phd unakuwa kilaza tu eg prof j4 wa mwanga.
 
Leo Jaji Simon Lukelelwa amefutilia mbali makosa ya ugaidi kwa washtakiwa watatu wanachama wa CHADEMA katika mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Pamoja na kutoa uamuzi huo Jaji Lukelelwa alichukua nafasi hiyo kutoa somo juu ya sheria ya UGAIDI kwa wanaotayarisha hati za mashtaka na kwa wanasiasa wanaoshabikia kutumia tuhuma za UGAIDI kama mbinu za kushindana kisiasa.

Jaji Lukelelwa alisema suala la kushabikia tuhuma za ugaidi limeshika kasi lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayaelewi madhara yake na mapana yake. Utalii na.uchumi utaathirika. Inaweza kuleta madhara kwa nchi pasipo kuwa na ulazima wowote.

Aliongeza kusema kuwa tafsiri ya neno Gaidi haiko wazi. Anayeweza kuwa gaidi kwako labda ni mpigania uhuru kwa mwingine.

Jaji Lukelelwa aliwalaumu waendesha mashtaka kwa kuandaa mashtaka na kuingiza ugaidi bila lazima pasipo kuzingatia makosa yaliyo kwenye hati ya mashtaka. Siyo kila kitakachotokea kati ya wanasiasa kiwe ugaidi.

Ni vizuri waandaa mashtaka wajifunze namna ya kuandaa hati za mashtaka, na jaji amewapa waendesha mashtaka vifungu vinavyowaelekeza namna ya kuandaa mashtaka.

Jaji Lukelelwa alisisitiza kuwa sharia ya UGAIDI inaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa walioko madarakani, na akaongeza kuwa hii ni hatari sana kwa Taifa.

Na mwishoni alisema kwenye hati ya mashtaka hakuna chochote kinachoonesha nia ya ugaidi.


Ni furaha kubwa kwa wananchi wote Tanzania wanaopenda amani, kwani akina Mwigulu Nchemba ambao ni waasisi wa vurugu hadi kumwagia tindikali kada wao kwa ku- sacrifice madaraka, hukumu yao ni Mungu pekee ataitoa. Mwigulu usidhani mwisho wa dunia haupo, la hasha upo subiri hukumu hiyo. Kijana wa watu ukamtoa kafara ionekane kamwagiwa tindikali na wanachama wa Chadema wakati ukijua fika ni mbinu zako za kisiasa, kisha ukamfanya ni mtaji wa kisiasa kule Arusha unamsimamisha jukwani kijana ambaye wewe unajua ndiye uliyemsababishia ulemavu ule, unajifanya kulia ili kubeba sympathy ya wananchi kumbe unalia kutokana na dhambi na hukumu itakayokukabili siku yako ukifa, hakika wala usidhani igizo hili la kulia halitatokea lipo utalia sana!!!
 
Ni aibu kwa watendaji wetu kuwa vibaraka wa wanasiasa.
 
Back
Top Bottom