Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Nimeshaanza kumkumbuka Severe wa mali asili na utalii.

Ama kweli Nakupenda Tanzania
 
Mh Bitte Shelukindo alisema baada ya kuomba Mungu amsaidie atacho sema, aliombwa sana asiseme!? Sasa sijui mgao wa 1bn ulimpitia mbali au aliulamba na kama sivyo labda alikuwa mzalendo kweli kiasi cha kukataa na kulipua BOMU, swali mnisaidie, aliipatapataje nyaraka adimu vilee? Maana angekua mnyika kaitoa ungesikia mala mmepta wapi nyaraka za selikari hata ka ni HARAMU!
 
Nyie vibaya hvy siye watoto wake tutaishi vipi hapa town inamaana hakuna tena magari ya kutembelea na mkwanja
 
Waziri Mkuu hana uwezo huo na kitu cha kushangaza zaidi hakujua mipaka yake. Hilo jambo liko chini ya Mkuu wa Utumishi wa Umma (Katibu Mkuu Kiongozi) ambaye atatoa mapendekezo kwa Rais kuhusu namna ya Kushughulikia jambo hilo kuanzia Uchunguzi hadi utoaji adhabu.
mbona Lowasa akiwa wazr mkuu alifanya maamuzi kadhaa yaliyoshangaza umma, ikawemo kufuta mkataba wa "dawasco" if not mistaken, pamoja na kufuta mkataba wa kinyonyaji wa mto nile, na mengine mengi!! Leo iweje Pinda ashindwe kumsimamisha kaz katibu mkuu wa wizara!"AJABU KUBWA HII"
 
Ni Serikali ya mataahira tu ndio inaweza kufanya uamuzi wa kipumbavu kama huu. Huyu inabidi kufukuzwa kazi haraka sana na pia kupandishwa kizimbani kwa kutumia pesa za walipa kodi ili kutoa rushwa kwa Wabunge kuhakikisha bajeti ya Nishati inapitishwa.

mwalimu Nyerere alikuwa anakufilisi unaachwa na kitanda cha banco tu.
 
Hiyo Ndio matokeo ya siasa Uchara maana lazima mbuzi wakafara apatikana ila Vinara wao wako mbali kama vile hawajui vile, hii ilitakiwa wote na Ngeleja wafukuzwe haraka na mafao yao yote pamoja mali zao zote wazikamate zirudi serikalini.
 
Huyu ni perege tu, papa na nyangumi ndiyo wanatakiwa kuwajibishwa! Ngeleje na Malima ndiyo wahusika wakuu, katibu mkuu katolewa kafara tu.
 
Anasubiri kuenguliwa na Rais.

Niliwahi kusema humu kuwa utamaduni wa kufukuzana kazi hatuna hivyo wale mnaoota kuwa jamaa kibarua kitaota majani mtaumiza nafsi zenu tu. Sana sana anatafutiwa kitaulo kingine. Sisi yetu macho
 
Kama mtu anaharibu kiasi hicho then wampa likizo,unategemea nini tena..
Niliwahi kusema humu kuwa utamaduni wa kufukuzana kazi hatuna hivyo wale mnaoota kuwa jamaa kibarua kitaota majani mtaumiza nafsi zenu tu. Sana sana anatafutiwa kitaulo kingine. Sisi yetu macho
 
Mtasikia kesho Bungeni pongezi kwa JK zitazavomiminika kutoka wabunge wa CCM! Au hiyo tayari?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom