Katibu wa CWT adai ana Mkataba wa Ajira ya Kudumu katika Chama cha Walimu Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Japhet Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika ya Wilayani Temeke, kumezuka maswali iwapo ataendelea kusalia katika uongozi wa CWT au la.

Mwalimu Japheth Maganga ameulizwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha kama utamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT?

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, Mwalimu Maganga amenukuu Ibara zilizopo ndani ya Katiba ya CWT akisema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT, hivyo ni Mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu.

Mwalimu Maganga ameendelea kwa kusema kuwa, kwa muujibu wa Katiba ya CWT, Toleo la Mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa Mwanachama wa CWT, hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

"Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu Januari 1, 2018. Niligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT nikitokea Idara ya Uhasibu CWT- Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani," anasema.

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ktiba ya CWT Toleo la Mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya Mwaka 2014, mimi ni mwanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, Ibara ya 30 (e) ya Katiba ya inathibitisha hilo."

Itakumbukwa kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Desemba 16, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa kisheria wa kuendelea kusalia madarakani kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT anautoa wapi ikiwa tayari ameshasimamishwa kazi, Mwalimu Maganga amesema:

"Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014."

Taarifa iliyotolewa Alhamis Desemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya viongozi.

Pia soma
= Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake
= Katibu mkuu CWT asimamishwa, ni yule aliyekataa uteuzi wa Rais Samia
 
Mara baada ya taarifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)...
Huyo fala amechanganyikiwa, hicho kinachoitwa mkataba amejitengenezea mwenyewe. Kwanza hana akili hata ya kuazimwa, yaani sisimizi km hilo ni la kushindana na serikali? Hakuna rangi hataona
 
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Japhet Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika ya Wilayani Temeke, kumezuka maswali iwapo ataendelea kusalia katika uongozi wa CWT au la.

Mwalimu Japheth Maganga ameulizwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha kama utamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT?

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, Mwalimu Maganga amenukuu Ibara zilizopo ndani ya Katiba ya CWT akisema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT, hivyo ni Mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu.

Mwalimu Maganga ameendelea kwa kusema kuwa, kwa muujibu wa Katiba ya CWT, Toleo la Mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa Mwanachama wa CWT, hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

"Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu Januari 1, 2018. Niligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT nikitokea Idara ya Uhasibu CWT- Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani," anasema.

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ktiba ya CWT Toleo la Mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya Mwaka 2014, mimi ni mwanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, Ibara ya 30 (e) ya Katiba ya inathibitisha hilo."

Itakumbukwa kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Desemba 16, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa kisheria wa kuendelea kusalia madarakani kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT anautoa wapi ikiwa tayari ameshasimamishwa kazi, Mwalimu Maganga amesema:

"Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014."

Taarifa iliyotolewa Alhamis Desemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya viongozi.

Pia soma = Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake
 
Lakini serikali nayo iache udhalimu kwa wananchi wake. Kwani kawakosea nini hasa hadi wamtafutie visa?
Maganga akili mingi.
Huko sirikalini machawa yana akili kiduchu kama ndezi.
Jamaa kawaacha wakurupuke ulipofika wakati muhafaka kawapiga na kufingu kizito cha katiba ya CWT.
Sema nini janjaro Japhet Maganga waachie lichama lao wata kutengenezea kesi ya ubadhirifu ukiwa muhasibu au karibu wa CWT.
 
Sakata hili ndiyo mjue huko Manispaa na Halmashauri kumejaa watu waliokosa sifa.
Maganga kawaumbua mkurugenzi na mwanasheria wa Manispaa.
Kawaumbua wasaidizi wa mteuzi wa ukuu wa wilaya.
Wanataka kumkomoa wakati hawajui sheria.
Japhet nenda zako kafanye biashara mtaani kwa amani waachie chama lao la waalimu.
 
Aisee umeuaaaaaaa
 
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Japhet Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika ya Wilayani Temeke, kumezuka maswali iwapo ataendelea kusalia katika uongozi wa CWT au la.

Mwalimu Japheth Maganga ameulizwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha kama utamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT?

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, Mwalimu Maganga amenukuu Ibara zilizopo ndani ya Katiba ya CWT akisema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT, hivyo ni Mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu.

Mwalimu Maganga ameendelea kwa kusema kuwa, kwa muujibu wa Katiba ya CWT, Toleo la Mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa Mwanachama wa CWT, hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

"Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu Januari 1, 2018. Niligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT nikitokea Idara ya Uhasibu CWT- Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani," anasema.

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ktiba ya CWT Toleo la Mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya Mwaka 2014, mimi ni mwanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, Ibara ya 30 (e) ya Katiba ya inathibitisha hilo."

Itakumbukwa kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Desemba 16, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa kisheria wa kuendelea kusalia madarakani kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT anautoa wapi ikiwa tayari ameshasimamishwa kazi, Mwalimu Maganga amesema:

"Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014."

Taarifa iliyotolewa Alhamis Desemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya viongozi.

Pia soma = Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake
Kwa akili ya kawaida kabisa ya mtanzania mpiga kura wa kawaida kunaonekana hapo CWT pana asali tamu sana ambayo ukiilamba mara moja tu basi hubanduki,,,alikataa teuzi January,September aliambiwa arudi kazini akakataa,,wamemfukuza kazini kwa kufata sheria ya utumishi wa umma Bado anasisitiza CWT ni Chaka lake na ataendelea kuwa katibu Sasa kwa akili ya kawaida kabisa utamu unapatikana CWT ndo maana hajabanduka hapo.

Hoja nyingine ya msingi kibali cha kuazimwa na cwt alikuwa anakiomba kwa miaka iliyopita na alikuwa akipewa na muajiri Sasa kwanini imekuwa ngumu kurudi kazini pale alipokataliwa kupewa kibali kipya??,,jibu Ni rahisi kabisa,,Hakuna taaamu Duniani kama ASALI
 
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Japhet Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika ya Wilayani Temeke, kumezuka maswali iwapo ataendelea kusalia katika uongozi wa CWT au la.

Mwalimu Japheth Maganga ameulizwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha kama utamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT?

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, Mwalimu Maganga amenukuu Ibara zilizopo ndani ya Katiba ya CWT akisema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT, hivyo ni Mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu.

Mwalimu Maganga ameendelea kwa kusema kuwa, kwa muujibu wa Katiba ya CWT, Toleo la Mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa Mwanachama wa CWT, hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

"Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu Januari 1, 2018. Niligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT nikitokea Idara ya Uhasibu CWT- Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani," anasema.

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ktiba ya CWT Toleo la Mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya Mwaka 2014, mimi ni mwanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, Ibara ya 30 (e) ya Katiba ya inathibitisha hilo."

Itakumbukwa kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Desemba 16, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa kisheria wa kuendelea kusalia madarakani kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT anautoa wapi ikiwa tayari ameshasimamishwa kazi, Mwalimu Maganga amesema:

"Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014."

Taarifa iliyotolewa Alhamis Desemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya viongozi.

Pia soma
= Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake
= Katibu mkuu CWT asimamishwa, ni yule aliyekataa uteuzi wa Rais Samia
Serikali inayoendeshwa na wahuni hufanya mambo ya kipuuzi sana
 
Back
Top Bottom