Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.

The Priest

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,029
256
Breaking news,hivi punde Katibu wa wizara ya nishati na madini Bwana,David Jairo amesimamishwa kazi,taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu kiongozi philemon Luhanjo ,amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma anazokabiriwa nazo.source ITV breaking news.
 
jairo anatakiwa nikumwambia jk anajiuzlu na sio kusubiri mtu asiyeweza kutoa hiyo burn..
 
Ok, then what? Kwanini asisimamishwe kazi pamoja na kushitakiwa kwa kitendo cha kutumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhongea? Hivi hiyo bilioni moja ingefanya mangapi ya kusaidia kuokoa tatizo la mgao wa umeme? Tunataka Jairo ashitakiwe na akiwa mahakamani atutajie wabunge waliochukua huo mlungula ili waturudishie tufanyie mambo mengine ya maendeleo kwa taifa.
 
amesema nini kuhusu ngeleja na watu wake, hiyo cabinet itafanya vipi kazi chini ya ngeleka kama mkuu wa wizara.!? Hili ni changa la macho wangestep down wote afu ndo uchunguzi ufanywe..
 
Ni Serikali ya mataahira tu ndio inaweza kufanya uamuzi wa kipumbavu kama huu. Huyu inabidi kufukuzwa kazi haraka sana na pia kupandishwa kizimbani kwa kutumia pesa za walipa kodi ili kutoa rushwa kwa Wabunge kuhakikisha bajeti ya Nishati inapitishwa.
 
Breaking news,hivi punde Katibu wa wizara ya nishati na madini Bwana,David Jairo amesimamishwa kazi,taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu kiongozi philemon Luhanjo ,amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma anazokabiriwa nazo.source ITV breaking news.

Huu niuonezi wa wazi! Sikubaliani kabisa na uamuzi wa serikali....hivi Jairo alichokuwa anafanya sikilikuwa na baraka za waziri na naibu waziri wake? Iweje rungu limwangukie yeye? I hate Tanzania.
 
Hawajasema lolote,eti amepisha uchunguzi jukumu alilokabidhiwa CAG,kwanini hajafukuzwa kazi kabisa?
amesema nini kuhusu ngeleja na watu wake, hiyo cabinet itafanya vipi kazi chini ya ngeleka kama mkuu wa wizara.!? Hili ni changa la macho wangestep down wote afu ndo uchunguzi ufanywe..
 
huyu Anna Makinda ndiyo anatakiwa aondoke pale ..... nchi itaendelea kupiga mark time .....
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi ni birds of one feather kamwe hawatatengana kwa mapenzi yao wenyewe. Hawa ni lazima wapewe talaka ya lazima. Wana kitu kinaitwa uhusiano wa kisymbiotic.
 
Ok, then what? Kwanini asisimamishwe kazi pamoja na kushitakiwa kwa kitendo cha kutumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhongea? Hivi hiyo bilioni moja ingefanya mangapi ya kusaidia kuokoa tatizo la mgao wa umeme? Tunataka Jairo ashitakiwe na akiwa mahakamani atutajie wabunge waliochukua huo mlungula ili waturudishie tufanyie mambo mengine ya maendeleo kwa taifa.
Unaijua sheria ya kazi au unaongea kishabiki tu?
 
Ataje wale waliochukua hicho kitita. Hiyo bank account imefunguliwa kisheria? Au ni zile zinaitwa SLUSH FUNDS kwa kimombo?
 
Wachunguze 'upitishaji' wa budget kwa wizara zote sio hii ya Nishati na Jairo peke yake.
Barua yake Jairo ya mchango imetumia maneno "kama ilivyo kawaida" what kawaida?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom