Jairo asimamishwa kazi

Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Katika dunia ya leo tunayoishi ya sayansi na teknologia hakuna kitu chochote ambacho rais anaweza kukifanya
akiwa hapa nchini lakini hawezi kukifanya akiwa nchi zingine. kuna video conference,kuna conference call na njia
nyingine nyingi ambazo zinamwezesha kufanya kazi yake kama yuko DSM. kuwaambia watu wasubiri mpaka
arudi ni moja ya mikakati yake ya ku buy time ili akusanye mawazo ya kuweza kumuokoa mshikaji wake wa karibu.

Mkakati mmoja wapo ni kuunda tume ya uchunguzi ili kukusanya ushahidi na kuwapata wahusika woooote wote kabisa
ili serikali ichukue hatua, It sounds good hee! lakini kuna trick nyuma yake nayo ni kuiachia what so called tume muda
ichunguze kwa miaka kabla ya kumfikishia rais report na rais akiona mambo ni mabaya basi atamtonya rafiki yake atangaze
kustaafu ili akusanye mafao yake yote serikalini kama walivyofanya kwa lowassa. kumbukeni kusimamishwa siyo kufukuzwa
tena anaweza kuwa anaendelea kulipwa bado.

Nini alitakiwa kukifanya JK ??
kama ni kiongozi serious angetakiwa kumtumia waziri mkuu kuthibitisha uhalali wa barua ile kwa jairo akikubali kuwa ni ya kwake
basi hiyo ingetosha kumfukuza kazi kwa sababu barua yenyewe ni self explainatory ktk kile alichotaka kukifanya.
 
Taarifa ilitolewa ni kuwa amepewa likizo ya malipo ie atapumzika huku analipwa
 
Du bongo noma nitarudi nchini nifanye nitafute kazi serekalini
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Pinda: Hatima ya Jairo iko kwa Rais
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 21 July 2011 08:54 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

AWEKA WAZI MAAGIZO MAPYA, KAAMBIWA ATULIE HADI MWENYEWE ATOKE AFRIKA KUSINI
Leon Bahati, Dodoma
dogojk.jpg
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameyaweka hadharani maagizo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema amemwambia kwamba atashughulikia suala hilo yeye mwenyewe atakapotoka ziarani Afrika Kusini.
Juzi, Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali bungeni, aliliambia gazeti hili kwamba alipewa maagizo na Rais juu ya kushughulikia tuhuma za kutenga zaidi ya Sh moja bilioni, kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

Hata hivyo, jana alipoulizwa nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu maelekezo hayo ya Rais, Pinda, alijibu: "Mheshimiwa Rais amesema atakuja kulishughulikia akirudi."

Pinda ambaye siku ya tukio hilo alionekana kuhamaki bungeni na kusema kwamba kama angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi Jairo, jana alionekana mwenye subira huku akisisitiza kuwa: "suala hilo halina uharaka."

Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambaye alisema mtendaji huyo mkuu wa wizara alitoa dokezo kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kutoa Sh50 milioni ili kufanikisha bajeti kupita bungeni hatua ambayo iliibua hasira miongoni mwa wabunge hasa ikizingatiwa hali ya nishati ya umeme ilivyo kwa sasa nchini.

Shellukindo katika tuhuma zake alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.

Kabla ya ufafanuzi huo wa Pinda, jana mchana kulikuwa na tetesi zilizozagaa katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mitandao ya intaneti zikidai kwamba Jairo ameandika barua ya kuomba kujiuzulu. Akizungumzia tetesi hizo Pinda alisema: "Sina taarifa hizo," na kuongeza Pinda na kukiri kwamba hata yeye amezipata lakini haelewi chochote kuhusiana na hilo.

Jumatatu wiki hii, baada ya Shellukindo kuibua tuhuma hizo bungeni, Pinda aliahidi kuwa angewasiliana na Rais siku hiyo baada ya kutua kutoka kwenye ndege kwa ajili ya kumchukulia hatua za kinidhamu... "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema haijui chochote kuhusu mawasiliano hayo ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda, kuhusu hatua za kushughulikia jambo hilo. Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga alisema hadi jana mchana, kurugenzi hiyo haikuwa na taarifa yoyote juu ya tuhuma zinazomhusu Jairo wala mawasiliano baina ya Waziri Mkuu na Rais.“Kama (Waziri Mkuu Pinda kumpigia Rais Kikwete), atakuwa amempigia siyo lazima sisi tujue,” alifafanua Kibanga.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Inalipa kuwa karibu na JK na dogo R1. Kuna mtu ameimba singo akimwomba dogo aseme na mshua halafu kuna mtu amesema anabadili jina lake ili liishie na Mrisho Kikwete; hawa nafikiri wameona mbali sana.
Kwa mfano huyu jamaa kwa raha zake anakwenda likizo (sijui ulaya) na haki zote. Ungekuwa wewe na mimi sasa hivi unany** debe wakati ukisubiri upelelezi
 
Ni Serikali ya mataahira tu ndio inaweza kufanya uamuzi wa kipumbavu kama huu. Huyu inabidi kufukuzwa kazi haraka sana na pia kupandishwa kizimbani kwa kutumia pesa za walipa kodi ili kutoa rushwa kwa Wabunge kuhakikisha bajeti ya Nishati inapitishwa.

Naunga mkono hoja kwa asilimia 100 kwa 100, tena siyo yeye tu, Ngereja naye angetimuliwa arudi kwa Rostam wakaanze upya!
 
Wachunguze 'upitishaji' wa budget kwa wizara zote sio hii ya Nishati na Jairo peke yake.
Barua yake Jairo ya mchango imetumia maneno "kama ilivyo kawaida" what kawaida?

Napenda watu wanaokwenda into details....hii ni sahihi kabisa inapaswa kuangaliwa kwa makini......Maana rahisi ni kwamba ni utamaduni na utaratibu wao kwa kila siku, na hii is kwa wizara ya Nishati na Madini bali mpaka kwingineko.
 
mbona Lowasa akiwa wazr mkuu alifanya maamuzi kadhaa yaliyoshangaza umma, ikawemo kufuta mkataba wa "dawasco" if not mistaken, pamoja na kufuta mkataba wa kinyonyaji wa mto nile, na mengine mengi!! Leo iweje Pinda ashindwe kumsimamisha kaz katibu mkuu wa wizara!"AJABU KUBWA HII"
Tunazungumzia Utumishi wa Umma, una misingi yake hakuna Siasa hapa.
 
Issue ya Jairo inasubiri raisi arudi aongee na wabunge wa CCM, then aongee faragha na Shelukindo. Baada ya hapo raisi ataunda tume huku Jairo akiendelea kupokea mshahara; then kitakachotokea kwenye taarifa ya tume itakua another history. Tukubali tu JK ni mzigo, tunachotakiwa kufanya ni kujadili jinsi ya kuutua huu mzigo before 2015.
 
Mh Dr Jakaya Mrisho Kikwete hajawahi kutoa maamuzi yeyote ya maana,Kwa urafiki wao tangu akiwa IKULU anaweza kumpa kazi katika balozi zetu nje anajua akimwa nguvu ya umma itamkosesha raha
 
Wakubwa wamekasilika ni kwanini? Vita ndio kwanza inaanza lakini ni lazima mmoja ashindwe.Si lazima alaumiwe aliyefikwa nayo usoni.Manake mwindwaji akuwepo ila kila aliyekaribu yake ni kualibu tu.Pole sana mlaumiwa ungefanya nini ili umma ujue tendo lile sio sawa hata kidogo.Mungu anapenda sana mtu akijitanabaisha kiasi kuwa hata ukisema chochote hakuna wa kukulaumu kwa kuwa wanajua ni haiba yako.Na ukweli unakuondoa kwenye utumwa.Next time kaa kimya usiongee ya ndani manake utawakasilisha wakubwa wako.

EEEEEEEhhhe likizo na malipo mpaka hapo itakapothibitika ndio au la.Eeeeeeeeeeehhe kwani ni lazima hii ni ajari ya kisiasa tu.
 
Mambo ya bongo ni kama maigizo, Kweli mungu awape amani na upendo, la sivyo tutotoana macho.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Pinda: Hatima ya Jairo iko kwa Rais[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 21 July 2011 08:54[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

AWEKA WAZI MAAGIZO MAPYA, KAAMBIWA ATULIE HADI MWENYEWE ATOKE AFRIKA KUSINI
Leon Bahati, Dodoma
dogojk.jpg
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameyaweka hadharani maagizo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema amemwambia kwamba atashughulikia suala hilo yeye mwenyewe atakapotoka ziarani Afrika Kusini.
Juzi, Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali bungeni, aliliambia gazeti hili kwamba alipewa maagizo na Rais juu ya kushughulikia tuhuma za kutenga zaidi ya Sh moja bilioni, kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

Hata hivyo, jana alipoulizwa nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu maelekezo hayo ya Rais, Pinda, alijibu: "Mheshimiwa Rais amesema atakuja kulishughulikia akirudi."

Pinda ambaye siku ya tukio hilo alionekana kuhamaki bungeni na kusema kwamba kama angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi Jairo, jana alionekana mwenye subira huku akisisitiza kuwa: "suala hilo halina uharaka."

Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambaye alisema mtendaji huyo mkuu wa wizara alitoa dokezo kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kutoa Sh50 milioni ili kufanikisha bajeti kupita bungeni hatua ambayo iliibua hasira miongoni mwa wabunge hasa ikizingatiwa hali ya nishati ya umeme ilivyo kwa sasa nchini.

Shellukindo katika tuhuma zake alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.

Kabla ya ufafanuzi huo wa Pinda, jana mchana kulikuwa na tetesi zilizozagaa katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mitandao ya intaneti zikidai kwamba Jairo ameandika barua ya kuomba kujiuzulu. Akizungumzia tetesi hizo Pinda alisema: "Sina taarifa hizo," na kuongeza Pinda na kukiri kwamba hata yeye amezipata lakini haelewi chochote kuhusiana na hilo.

Jumatatu wiki hii, baada ya Shellukindo kuibua tuhuma hizo bungeni, Pinda aliahidi kuwa angewasiliana na Rais siku hiyo baada ya kutua kutoka kwenye ndege kwa ajili ya kumchukulia hatua za kinidhamu... "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema haijui chochote kuhusu mawasiliano hayo ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda, kuhusu hatua za kushughulikia jambo hilo. Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga alisema hadi jana mchana, kurugenzi hiyo haikuwa na taarifa yoyote juu ya tuhuma zinazomhusu Jairo wala mawasiliano baina ya Waziri Mkuu na Rais.“Kama (Waziri Mkuu Pinda kumpigia Rais Kikwete), atakuwa amempigia siyo lazima sisi tujue,” alifafanua Kibanga.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

hii imekaaje

[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="class: kaziBody, align: left"]KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, amepewa likizo kuanzia leo ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili na kupata ukweli kabla ya hatua zingine kuchukuliwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, alisema jana mjini Dodoma kwamba, yeye ndiye mwenye mamlaka ya nidhamu na kwa kuwa tuhuma zinazomhusu Jairo ni za fedha, amemteua Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kumpa siku 10 afanye uchunguzi wa awali.

Luhanjo alisema, ndani ya siku kati ya mbili na tatu, atakuwa amemteua mtu wa kukaimu nafasi hiyo, wakati Jairo akiwa katika likizo hiyo ambayo ni ya malipo. “Siku mbili, tatu mtasikia nani nimemteua,” alisema Luhanjo.

Katibu Mkuu Kiongozi alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari na kusema tuhuma dhidi ya Jairo ni nzito hali ambayo imemlazimu kuamua aende likizo licha ya kwamba Sheria namba 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za utumishi wa umma za mwaka 2003, inaruhusu mtuhumiwa kuendelea na kazi wakati uchunguzi ukifanywa.

Kwa mujibu wa Luhanjo, tuhuma zinazochunguzwa ni zilizotolewa na baadhi ya wabunge wakati wakichangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini.

Baadhi yao ni pamoja na kuzitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya wizara hiyo, zichangie Sh milioni 50 kila moja, ili fedha hizo zitumike kulipa wabunge na kufanikisha mawasilisho ya makadirio hayo.

Tuhuma zingine ni za kulipa masurufu ya safari watumishi walio chini ya wizara hiyo na taasisi zake, ambao tayari walishalipwa na wizara na taasisi hizo.

“Hataendelea na kazi kipindi cha uchunguzi. Hatua zaidi zitategemea uchunguzi huo wa awali… nimeamua niseme, msianze kubashiri, kwamba tunamsubiri Rais aliyemteua, mimi ndiye mwenye mamlaka … nikipata taarifa ya uchunguzi wa awali, nitampa notisi ya matokeo ya awali,” Luhanjo aliwaambia waandishi wa habari.

Uamuzi wa kusisitiza kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka, unatokana na vyombo vya habari jana kuchapisha taarifa zikimkariri Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa uamuzi juu ya Jairo unamsubiri Rais Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari ambao Luhanjo alifuatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo na waandishi wa Waziri Mkuu, Luhanjo alitoa somo kwa waandishi wa habari juu ya utaratibu wa kushughulikia tuhuma dhidi ya mtumishi wa umma.

Luhanjo alisema kulingana na Sheria namba 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za utumishi wa umma za mwaka 2003, mwenye mamlaka ya nidhamu kwa mtumishi yeyote wa umma anayetuliwa na Rais kasoro wanasiasa, mawaziri na wakuu wa mikoa, ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Alisema katika kushughulikia tuhuma zinazomkabili mtumishi wa umma, lazima uchunguzi wa awali ufanyike kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma, ili kubaini kama mtumishi husika ametenda kosa la kinidhamu.

“Katika kipindi cha uchunguzi, mtumishi anayetuhumiwa, anaweza kupewa likizo ya malipo ili kupisha shughuli za uchunguzi au akaruhusiwa kuendelea na kazi wakati uchunguzi ukifanywa,” alisema Luhanjo.

Alifafanua kwamba kama uchunguzi wa awali dhidi ya Jairo, utabaini makosa ya kinidhamu, Mamlaka ya Nidhamu itampa taarifa za tuhuma ambazo zitaambatana na hati ya nashitaka, itakayoelezea kwa ufupi kosa alilotenda na ni lini anapaswa awe amejibu tuhuma husika. Mtuhumiwa anapaswa asimamishwe kazi na kulipwa nusu mshahara.

“Mtuhumiwa atatoa maelezo yake kwa mujibu wa hati ya mashitaka aliyopewa. Anaweza kukataa au kukubali. Akikubali, Mamlaka ya Nidhamu itaendelea kutoa adhabu kulingana na uzito wa kosa. Adhabu inaweza kuwa kufukuzwa kazi, kupunguzwa cheo au kupunguzwa mshahara ama adhabu nyingine iliyoelekezwa na Sheria ya Utumishi wa Umma.

“Iwapo atakana mashitaka, Mamlaka ya Nidhamu itaunda Kamati ya Uchunguzi itakayopewa hadidu za rejea ambazo pamoja na mambo mengine, zitaeleza muda wa uchunguzi huo kukamilika. Taarifa ya kamati itawasilishwa kwa Mamlaka hiyo, ikiwa na mapendekezo.

Ikumbukwe kuwa Kamati hii haitoi adhabu kwa mtuhumiwa isipokuwa inatoa mapendekezo tu,” Luhanjo alisisitiza. Baada ya taarifa ya kamati ya uchunguzi, Luhanjo alisema Mamlaka itaendelea kutoa adhabu kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati hiyo. Kama adhabu itakuwa ni kuvuliwa madaraka, Mamlaka ya Nidhamu itawasiliana na Mamlaka ya Uteuzi kuhusu kutekeleza suala hilo.

Hata hivyo, Luhanjo alisema iwapo mtuhumiwa hajaridhika na uamuzi unaoishia kwa Mamlaka ya Nidhamu, sheria zinampa fursa ya kukata rufaa kwa Rais. “Rais ana mamlaka ya kuthibitisha au kukataa uamuzi wa Mamlaka ya Nidhamu,” alisema.

Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa Julai 18 bungeni na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM). Jana katika maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdallah (CUF) alihoji sababu za uamuzi wa kumwajibisha Jairo kumsubiri Rais Kikwete wakati yupo Makamu wa Rais anayefanya kazi kwa niaba yake.

Mbunge huyo alisema kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ambayo katika Kifungu cha 47 (1) (c) ana mamlaka ya kufanya kazi zote za Rais anapokuwa amesafiri nje ya nchi. “Ulitoa kauli bungeni kwamba huna mamlaka ya kumwajibisha Katibu Mkuu, unamsubiri Rais. Je huoni kwa kufanya hivyo umekiuka kanuni za Katiba?” alihoji Abdallah.

Akijibu, Pinda alisema kulingana na Katiba, si kila jambo wanaopewa dhamana wanapaswa kutoa uamuzi.

Alisema pamoja na kwamba Katiba inaelekeza pia Waziri Mkuu kupewa mamlaka iwapo Makamu wa Rais hayupo, wana kikomo cha madaraka. “Tusitafsiri kipengele hiki kwamba Rais akiondoka ndio sasa umepewa unga,” alisema Pinda.

Pinda aliwaambia wabunge kuwa suala hilo angeliwasilisha kwa Rais Kikwete aliyekuwa ziarani Afrika Kusini kwa kile alichosema ndiye mwenye uamuzi, kwa kuwa ndiye aliyemteua.

Juzi Waziri Mkuu akawaambia tena waandishi wa habari kuwa alipowasiliana na Rais, alimwambia asubiri arejee nchini ndipo uamuzi utolewe kuhusu sakata hilo.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Text, align: left"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]Ikulu yagwaya kumtimua David Jairo
• Ushauri wa Pinda wawekwa pembeni

na Waandishi wetu
Tanzania Daima


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
OFISI ya Rais (Ikulu), imepata kigugumizi cha kutekeleza ushauri uliotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wa kumtimua kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayekabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili ya kazi, Tanzania Daima limebaini.

Badala yake, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Ikulu imeamua kumsimamisha kazi kwa siku 10 ili kumpa fursa, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kumchunguza.

Akitangaza hekima hiyo mpya ya Ikulu ambayo haijawahi kutumiwa kwa viongozi wengine waliopata kukabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili ya kazi, Luhanjo alisema hatua atakazochukuliwa Jairo zitategemea matokeo ya uchunguzi huo.
“Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua.

“Kutokana na uzito wa jambo hili, nimelazimika kumwamuru CAG, Ludovick Utuoh, kufanya uchunguzi ndani ya siku 10 na iwapo itabainika kuwa ana kosa, hatua nyingine za kisheria zitafuata,” alisema Luhanjo.

Pasipo kusema kwamba alikuwa akitekeleza maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa karibu kikazi na Jairo kwa miaka mingi, Luhanjo alisema likizo hiyo itakuwa ni ya malipo.

Kauli hiyo ya Luhanjo inakuja ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu Waziri Mkuu Pinda akaririwe akisema kuwa alikuwa amepewa maelekezo tofauti na Rais Kikwete baada ya kuwasilisha kwake malalamiko ya wabunge dhidi ya Jairo.

Pinda alitoa kauli hiyo juzi ikiwa ni siku moja tu baada ya kulitangazia Bunge kwamba iwapo suala hilo lingekuwa katika mamlaka yake na si ya Rais, angeshakuwa amemtimua kazi Jairo.

Akizungumzia tuhuma ambazo Jairo anakabiliana nazo, Luhanjo alirejea hoja zilizotolewa na wabunge ambao walitaka afukuzwe kazi kwa kosa la kuandika barua yenye maelekezo ya kukusanya kiasi cha fedha kinachofikia shilingi milioni 50 kutoka kwa kila taasisi iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

“Kama mnavyofahamu, Julai 18 mwaka huu wakati wa majadiliano ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, baadhi ya waheshimiwa wabunge wakati wakichangia hotuba hiyo walimtuhumu Jairo kuhusika na tuhuma mbalimbali.
“Baadhi ya tuhuma zinazomkazili ni kuzitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya wizara hiyo zichangie shilingi milioni 50 kila moja, ili fedha hizo zitumike kuwalipa masurufu ya safari watumishi walio chini ya wizara na taasisi zake ambao tayari walishalipwa na wizara na taasisi zao,” alisema Luhanjo.

Alisema lengo la kufanya uchunguzi huo ni kutaka kumpa fursa ya kujitetea kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma.

“Katibu Mkuu alituhumiwa na wabunge, na yeye hana nafasi ya kujitetea ndani ya ukumbi wa Bunge, na ni lazima tuhuma zipate maelezo ya upande wa pili na hapa ndipo sheria hii ya utumishi wa umma inachukua nafasi yake,” alisema.

Akieleza kuhusu sheria za utumishi wa umma, Luhanjo alisema wakati wa kipindi cha uchuguzi, mtumishi wa umma anayetuhumiwa anaweza kupewa likizo ya malipo, ili kupisha uchunguzi au akaruhusiwa kuendelea na kazi wakati uchunguzi ukifanywa.
Alisema baada ya uchunguzi huo kukamilika na kama utabaini makosa ya kinidhamu, mamlaka ya nidhamu itampa mtumishi taarifa za tuhuma ambayo itaambatana na hati ya mashtaka na kwamba wakati huo mtumishi atasimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara.

Mzimu wa Jairo wamtesa Pinda

Katika hatua nyingine mzimu wa Jairo jana uliendelea kumtesa Pinda bungeni baada ya kubanwa kutokana na kushindwa kumwajibisha.
Akiuliza swali la papo hapo, mbunge wa Tumbe, Rashid Ally Abdallah (CUF), alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais ana mamlaka ya kufanya kazi za Rais endapo Rais hayupo, hivyo Pinda aliposema alikuwa hana mamlaka ya kumwajibisha Jairo ni kwenda kinyume na Katiba hiyo.

Akijibu swali hilo, Pinda alikiri kupata mtihani ambao hakuwa akiutarajia na akasema ni ukweli kwamba wanapokuwa viongozi wajuu wawili, Rais na makamu wake hawapo, hata yeye angeweza kuchukua mamlaka ya kufanya kazi za Rais.

“Mheshimiwa Abdallah kanipa mtihani wala sikutegemea. Ni kweli Rais asipokuwapo na hata Makamu wa Rais, mimi naweza kukwaa mamlaka hayo, lakini kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo si kila jambo tuna mamlaka ya kuchukua hatua. Kwa mfano hatuwezi kutoa msamaha wa wafungwa. Tuna kikomo cha mamlaka,” alisema Pinda.
Alisema kuwa hata Makamu wa Rais anaweza kuchukua majukumu mengine ya Rais, endapo tu atapata ushauri wake (Pinda) wakati Rais hayupo.
Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alisema kwa mtazamo wake suala la Jairo si zito, hivyo kushauri kufanyika marekebisho ya Katiba ili viongozi hao wawe na mamlaka hiyo.
Aliposimama kulijibu swali hilo, Pinda hakutaka kuingia kwa undani zaidi ya kusema, “Naheshimu mawazo yako, naomba majibu yake yabaki yale yale.”
Mbunge wa kwanza kuibua tuhuma hizo dhidi ya Jairo alikuwa ni mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo (CCM), ambaye ndiye aliyeionyesha barua ambayo inadaiwa kuandikwa na Jairo kwenda kwa taasisi 21 zilizo chini ya wizara yake kuomba wachangie kufanikisha bajeji yake.

Baada ya taasisi hizo kupata kiwango hicho cha fedha, zilitakiwa kuingizwa katika akaunti ya Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye akaunti namba 5051000068 iliyopo benki ya NMB, tawi la Dodoma.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka: “Kama ilivyo wakati wa kuwasilishwa hotuba ya bajeti, maofisa mbalimbali wa wizara na taasisi zilizo chini yake huambatana na viongozi waandamizi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala yanayojitokeza wakati wa mjadala wa hotuba hiyo.

“Ili kukamilisha mawasilisho ya hotuba hiyo, unaombwa kuchangia jumla ya sh 50,000,000. Fedha hizo zitumwe Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye akaunti namba 5051000068 iliyoko benki ya NMB, tawi la Dodoma. Baada ya kutuma fedha hizo, wizara ipewe taarifa kupitia ofisi ya DP,” alisema.

Wakati CAG akimchunguza Jairo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) nayo ilitangaza kuanza uchunguzi kama huo dhidi ya Jairo sambamba na ule unaomgusa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge.

Mkurugenzi wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini , (TAKUKURU), Dk. Edward Oseah, amesema kuwa ofisi yake imeanza kuchunguza tuhuma zilizoibuliwa bungeni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, alikusanya shilingi bilioni 1 kutoka idara mbalimbali za wizara hiyo kwa ajili ya kutoa rushwa kuwezesha bajeti ya wizara hiyo kupita .

Pia wanamchunguza mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge kutokana na kumiliki kiasi kikubwa cha fedha nje ya nchi ingawa alisema kuwa kwa suala la rada hawawezi kumhusisha nalo kwani suala hilo lilitendeka nchini Uingereza (mhhh! Mbona yule Mahalu aliiba akiwa Italy na bado alipandishwa Kizimbani!?) na wahusika walishakiri hilo hivyo kwa sasa kinachojadiliwa ni namna ya kurudisha fedha hizo nchini.

Aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Naural Spring ambapo TAKUKURU wameandaa semina ya siku mbili kwa wahihiri wa habari.

Dk. Oseah alisema kuwa masuala hayo wanayachunguza na anatarajia kutoa taarifa mapema mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
“Suala la Chenge kuhusika kwenye rada naomba niungane na DPP imeonekana hakuhusika kwani suala hilo halikufanyika hapa nchini bali lilifanyikia nchini Uingereza na wahusika waligawana fedha hukohuko ndiyo maana kampuni ya BAE Systems imekubali kurudisha fedha hizo nchini na majadiliano yanendelea juu ya namna ya kuzirejesha.

“Hili la Chenge kuwa na vijisenti hilo tunalichunguza, kwa kuwa na vijisenti vingi kuliko inavyotarajiwa nje ya nchi hili tunalifanyia uchunguzi ukikamilika tutawapa taarifa,” alisema mkurugenzi huyo wa TAKUKURU .

Hivi karibuni mbunge wa Kilindi , Beatrice Shellukindo alilipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo, kwa kutumia zaidi ya sh bilioni moja kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.

Tuhuma hizo nzito zinakuja kipindi ambacho tayari wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wakiwa wameibua tuhuma kama hizo za baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa na maofisa wa wizara hiyo, ili kurahisisha upitishaji wa bajeti ndani ya kamati.

Ilidaiwa kuwa Jairo alisambaza barua kwenye idara mbalimbali za wizara hiyo akiagiza wachangie shilingi milioni 50 kila moja kwa ajili ya kusaidia bajeti ya wizara hiyo kupitishwa ambapo pamoja na suala la mgao mkali wa umeme unaoendelea nchini ulisababisha waziri mkuu, Mizengo Pinda kutoa hoja ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa wiki tatu .

Waziri Mkuu alisema kuwa alikuwa akisubiri Rais Jakaya Kikwete afike Afrika ya Kusini alikokwenda katika ziara ya kiserikali ili aweze ‘kumshtaki’ Katibu Mkuu huyo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake kwani hawezi kuchukua hatua dhidi yake kwani kwa mujibu wa sheria, mamlaka ya uteuzi ndiyo inayoweza kuchukua hatua dhidi yake.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Mwanza , Aishieli Sumari, ambaye alikuwa kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari aliwataka wananchi kuacha kuwapelekea fedha mahakimu ambapo alishauri ni vema TAKUKURU wakatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waepukane na vitendo hivyo vinavyochochea kuendelea kwa rushwa .

Aidha aliishauri serikali iwape watumishi wa umma stahiki zao zinazoweza kukidhi mahitaji yao jambo litakalowawezesha kukataa kupokea rushwa kwani watakuwa wamekidhi mahitaji yao kutokana na mishahara yao .

Jaji Sumari aliwataka TAKUKURU kubadili utaratibu wa kushughulikia tatizo la rushwa kwenye idara ya mahakama badala ya kufanya kazi ya kuwakamata watumishi wa mahakama wakipokea rushwa wawaelimishe kuacha kupokea rushwa ambapo alisema kuwa kwa semina waliyowapa wameanza kujenga mshikamano katika kupambana na rushwa.
FemAct watoa tamko

Nao Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea usawa wa jinsia, haki za binadamu, demokrasia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) umemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwachukulia hatua za kinidhamu wote waliohusika na tuhuma za kuchangisha fedha za kuwahonga wabunge.

Akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti ya Femact, Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ussu Malya alisema mambo hayo yamefanyika kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

“Tunamtaka Rais Kikwete awafute kazi watendaji hao mara moja na kuwachukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu,Waziri,Naibu wake kwa pamoja na watendaji wengine waliohusika ili iwe mfano kwa wahalifu wengine waliojificha katika ajira za serikali,” alisema Mallya.

Alieleza kuwa sema katika marekebisho ya bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati Serikali ilete mikakati sahihi ya kulimaliza tatizo la umeme nchini.
Alisema kwao wao kama wanaharakati wanaona kuwa kitendo hicho ni ishara ya mambo makubwa zaidi yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu yanayosababisha kuendeleza ufukara na umaskini wa taifa letu na watu wake.

“Hali hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa serikali inayoghubikwa na kuendeshwa kwa mfumo wa kuhongana miongoni mwa viongozi na watendaji wenye mamlaka ya kufanya maamuzi katika mihimili mikuu ya dola, ni serikali ya hatari na isiyostahili kuendelea kuwa madarakani,” alisema Mallya.
Alieleza kuwa tatizo la umeme halikuanza leo kwani limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu, Serikali imekosa mbinu na mikakati sahihi hadi kufikia hatua ya kutaka kubinafsisha Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).
Aliongeza kuwa mikataba mingi michafu imeingiwa na Serikali kwa kutumia makampuni makubwa ya nje kama IPTL, Agreco, Songas, Richmond, Dowans na NetGroup Solutions.
Alisema Muungano wao unaamini kuwa kuna sababu nyingine inayolazimisha Serikali kujaribu kutoa rushwa ili kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ni mfumo mzima wa mikataba, uwekezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli za madini na gesi asilia hapa nchini ambao hauna uwajibikaji; na uwazi wake una mashaka na hivyo kuhalalisha vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kauli ya January Makamba

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba (CCM) amewataka wanasiasa kujisafisha na kuacha kutumia muda mrefu kwa kurushiana maneno.
Akizungumza katika tamasha la vijana lililofanyika katika ukumbi wa Kanisa la ATN lililopo Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam, Makamba alisema kuwa hiyo ni moja ya changamoto inayowakabili viongozi kwa sasa ambapo hushindwa kufanya shughuli ngingine za maendeleo.
Alisema inawapasa viongozi kujitazama upya na kuhakikisha wanakuwa na roho safi ili kufikia malengo ya kimaendeleo kuliko kuendelea kurushiana maneno.
“Hata mkitazama magazeti mtagundua wazi kuwa viongozi wanatumia muda mrefu kurushiana maneno …huyu anagombana na yule vitendo ambavyo havimpendezi Mungu,” alisema.
Makamba alisema kuwa jamii imejengwa katika misingi ya ustaarabu ndiyo maana imekuwa ikipuuza vitendo hivyo ambavyo vimekuwa havionekani ndani ya jamii.
“Viongozi wengi vijana kama mimi tunatazamiwa kuwa viongozi zaidi mbeleni kwa kuwatumikia wananchi hivyo inatupasa kuepuka majibizano na kuhakikisha tunapigania maendeleo ya nchi yetu kuliko kuendeleza malumbano,” alisema.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na vijana hao likiwemo suala la umeme, Makamba alisema kuwa wanafahamu kuwa Watanzania wanahitaji umeme wa uhakika hivyo suala la visingizio vya kukosa mvua si vya msingi.
Alisema wataalam walipaswa kuelewa kuwa kuna kipindi cha kiangazi hivyo ni vyema wakatumia mipango iliyoandaliwa ili kuwapatia Watanzania Umeme.
Makamba alisema kuwa suala hilo limewafanya baadhi ya wananchi kuondoa imani walioijenga kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini aliwahakikishia kuwa ataendelea kupigania bila kuchoka hadi umeme wa uhakika upatikane.
“Hapa lazima tukubali kuwa tatizo la kutoweka mipango thabiti ndiyo imetufikisha hapa na nakubaliana nanyi kuwa kuna watu wanatakiwa kuwajibika katika suala la umeme, alisema na kuongeza: “…Kama ningekuwa msimamizi mkuu katika Wizara hiyo ningehakikisha ifikapo Desemba 31 kila mwaka tungeweka utaratibu wa kukutana na yule anayeshughulikia umeme ambapo anatakiwa kufika na barua mbili moja ya kujiuzulu na nyingine ya kufungua miradi ya umeme,” alisema.
Alisema iwapo msimamizi wa suala la umeme atashindwa kuonyesha mradi unaotakiwa kufunguliwa basi ile barua ya kujiuzulu anatakiwa kukabidhiwa pasipo maswali hasa kutokana na kushindwa kuwajibika.
Pamoja na hilo aliwahakikishia Watanzania kuwa hataacha kulipigania suala hilo na wala kuacha kuikosoa serikali katika masuala ya msingi yaliyo na maslai kwa Taifa.
“Mtakumbuka kama ninyi ni wafuatiliaji wa masuala ya Bunge jinsi Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe (CHADEMA) alivyohoji juu ya taarifa niliyoitoa kwa serikali na kushangazwa na kunitaka kujiunga nao,nawaahidi kusimamia ukweli,” alisema.
Aidha Makamba aliwaasa vijana hao kujiepusha na tamaa ya kutaka mafanikio ya haraka kwa kupita njia ya mkato bali wanapaswa kumtumaini Mungu kwa kuwa mafanikio hayaji mara moja. Ataka Bunge kujiuzulu

Sakata la kutopitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini linazidi kutolewa maoni mapya kila siku baada ya mwaharakati katika masuala ya siasa, Kadawi Limbu, kulitaka Bunge la Jamhuri kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo.
Limbu ambaye uchaguzi uliopita aligombea kiti cha ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Temeke, alisema Bunge hilo halina haja ya kuendelea kutokana na barua ya Katibu wa Wizara hiyo, David Jairo, kuwagusa moja kwa moja na wao.
Akinukuu mojawapo ya sehemu ya barua iliyoandikwa na Katibu wa Wizara hiyo, David Jairo, na kusomwa na Mbunge wa Bumbuli, Beatrice Shelukindo, iliyotaka idara zote zilizo chini ya wizara hiyo kuchangia kila moja shilingi milioni 50 kama ilivyo kawaida, ili kufanikisha kupitishwa kwa bajeti hiyo…”
Limbu alisema nukuu ya barua hiyo inaonyesha wazi kuwa huo ndio utaratibu wa Bunge kupokea rushwa hiyo, hivyo haoni haja wabunge hao kuendelea kupoteza muda Dodoma na kufuja fedha za wananchi wakati Bunge lote linanuka rushwa na kuongeza kuwa limeoza.

Aidha mwanasiasa huyu alisema ni vyema wabunge hao wakaachia nyadhifa zao bila kujali vyama walivyotokea na kuitishwa uchaguzi mwingine na wao kukaa kando bila kugombea nafasi yoyote ile.
“Jamani ninavyoona mimi, Jairo anafanywa mbuzi wa shughuli katika sakata hili, kwani barua aliyoaindika inaonekana ni ya kikazi na hajakaa mwenyewe tu na kuielekeza katika idara hizo na ndio maana ikasisitiza kama ilivyo kawaida, yote hii inamaanisha hata katika wizara nyingine ndivyo inavyofanyika.
“Pia tumezoea kuona tuhuma zote zinazowasilishwa na wabunge, Spika kutaka kupelekwa kwa maandishi mezani kwake, mbona hii ya Shulukindo hakutaka apelekewe mezani hata pale mbunge huyo aliposema endapo itakanushwa ataipeleka mezani kwake, ina maana na yeye anajua utaratibu huo kuwa unafanyika ndani ya Bunge lake,” alisema Limbu.
Alienda mbali zaidi kuwa mpaka sasa mihimili mikuu miwili ya nchi ikiwemo Serikali na Bunge wananchi wameshakosa imani nayo kwa kushindwa kuonyesha dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa na barua hiyo ni ushahidi tosha na kutaka iwekwa wazi hata kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuona kile kilichoandikwa humo.
Alisema barua hiyo inaonyesha dhairi kwamba Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikishawishi Bunge kwa fedha ili kupitisha mambo yasiyofaa na mhimili pekee uliobaki ambao bado vithibitisho havijapatikana ni mahakama peke yake. Hata hivyo alitahadharisha kuwa Raisi Jakaya Kikwete asije akadhani atakapomfukuza Jairo, nchi itakuwa salama, kwani serikali yake yote imeoza na dawa ni iliyopo ni kuivunja.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Duh!!!!!!!

"Nimeona niwaambie hili ili tusiendelee kuwaambia wananchi tunamsubiri Rais, wakati mimi mwenye dhamana ya kusimamia nidhamu nipo hapa, nimeshachukua hatua".
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom